Kwanini Jerusalem ni mji Mtakatifu?

Kwanini Jerusalem ni mji Mtakatifu?

Daah umeniwahi sana kuanzisha huu uzi nilikuwa nawaza jambo hili tangu juzi...
nimekuwa nasoma biblia kila siku na najaribu kutafakari je kuna kitabu kingine chochote kikongwe duniani zaidi ya biblia?
kama hakuna kinachobishaniwa ni kipi?
sabbu mipaka ya Taifa la Israel imewekwa bayana katika biblia na ikiutaja Yerusalem kama Mji ndani Ya Israel. Sasa ubishani unatoka wapi?
kama viongozi wote wanaapa kwa kupitia Mungu huyu aliendikwa katika biblia na Mungu huyu huyu ndie aliyetoa mipaka ya urithi wa Taifa alilolichagua kuwa teule kwake!
iweje kuwe na kukataa kwa maelekezo ya mipaka ya Taifa hilo na miji yake?

Je waislam hawaamini katika Biblia au maandiko yaliyo katika biblia..?
kama wanaamini je hawasomi kuhusu mipaka ya Israel na miji yake?
Kama wanasoma je mipaka hiyo iko sawa ama haiko sawa?

Jelusalem ni Mji mkuu wa Israel hizo nyingine kwa mtazamo wangu ni mbwembwe tu za kisiasa.

Umeelewa ulivyochambuliwa??
Au wewe ndio unaeleta SIASA
 
Umeungana na ndugai
Daah umeniwahi sana kuanzisha huu uzi nilikuwa nawaza jambo hili tangu juzi...
nimekuwa nasoma biblia kila siku na najaribu kutafakari je kuna kitabu kingine chochote kikongwe duniani zaidi ya biblia?
kama hakuna kinachobishaniwa ni kipi?
sabbu mipaka ya Taifa la Israel imewekwa bayana katika biblia na ikiutaja Yerusalem kama Mji ndani Ya Israel. Sasa ubishani unatoka wapi?
kama viongozi wote wanaapa kwa kupitia Mungu huyu aliendikwa katika biblia na Mungu huyu huyu ndie aliyetoa mipaka ya urithi wa Taifa alilolichagua kuwa teule kwake!
iweje kuwe na kukataa kwa maelekezo ya mipaka ya Taifa hilo na miji yake?

Je waislam hawaamini katika Biblia au maandiko yaliyo katika biblia..?
kama wanaamini je hawasomi kuhusu mipaka ya Israel na miji yake?
Kama wanasoma je mipaka hiyo iko sawa ama haiko sawa?

Jelusalem ni Mji mkuu wa Israel hizo nyingine kwa mtazamo wangu ni mbwembwe tu za kisiasa.

Daah umeniwahi sana kuanzisha huu uzi nilikuwa nawaza jambo hili tangu juzi...
nimekuwa nasoma biblia kila siku na najaribu kutafakari je kuna kitabu kingine chochote kikongwe duniani zaidi ya biblia?
kama hakuna kinachobishaniwa ni kipi?
sabbu mipaka ya Taifa la Israel imewekwa bayana katika biblia na ikiutaja Yerusalem kama Mji ndani Ya Israel. Sasa ubishani unatoka wapi?
kama viongozi wote wanaapa kwa kupitia Mungu huyu aliendikwa katika biblia na Mungu huyu huyu ndie aliyetoa mipaka ya urithi wa Taifa alilolichagua kuwa teule kwake!
iweje kuwe na kukataa kwa maelekezo ya mipaka ya Taifa hilo na miji yake?

Je waislam hawaamini katika Biblia au maandiko yaliyo katika biblia..?
kama wanaamini je hawasomi kuhusu mipaka ya Israel na miji yake?
Kama wanasoma je mipaka hiyo iko sawa ama haiko sawa?

Jelusalem ni Mji mkuu wa Israel hizo nyingine kwa mtazamo wangu ni mbwembwe tu za kisiasa.
 
Jerusalem is my favorite city
 
Wana bodi salam.

Naomba kujuzwa zaidi historian ya mji wa yelusarem in nani hasa anastahili kuwepo ktk mji huo kati ya wayahudi na waislaeri na nini hasa chanzo cha mgogoro wao?
 
mhh..rais wa dunia Trump kishasema 'yelusarem ni ya waislaeri'
 
Badilisha Kwanza Hyo Avatar Ndo Uulize Historia Ya Mji Mtakatifu,,,,
 
Trump amekosea nini kutangaza kuitambua Jerusalem kama makao makuu ya Israeli?
 
Ahadi za Mwenyezi Mungu ni takatifu na huwa hazibadiliki, hata binadamu afanyeje kamwe hataweza kubadilisha ahadi hizo. Hata wapange vita ya mabomu ya atomic mtashindwa tu kwani mnapambana na Mungu.
 
Mkuu mbona chato haijaidhinishwa kama mji muhimu kikatiba ila vipaumbele vingi kwa sasa vinaelekezwa huko? Nionavyo tuachane na Israel, wapambane nayo wayahudi sisi tumbane Ngosha ze don astawishe makao makuu ambayo ni Dodoma kikatika badala ya chato!
Chato inajengwa kwa fedha kutoka mfukoni mwa MTU mmoja
 
Mengi sana yataongelewa,lakini ukweli ni kwamba Mungu mwenyewe ndiye aliyeutenga mji huo kuwa mji mtakatifu,kwa malengo yake.Amefanya hivyo kwa kuwa ametaka kufanya hivyo,hakuna wa kumhoji.Hivi chungu kimuulize potter kwa nini umenitengeneza hivi kweli,nadhani haiwezekani.Tumuache Mungu awe Mungu,we can never understand his ways.

Matatizo yote yanayoendelea kuhusu Jerusalem ni harakati za Shetani za kujaribu kufisha mpango wa Mungu mwenyewe wa kuufanya Jerusalem kuwa makao yake makuu hapa duniani after the millenium,kama alivyoshindwa vibaya katika jaribio la kumfanya Bwana Yesu asiangikwe mtini.He thought kwa kumuwamba Yesu mtini that would be the end of the salvation plan,kumbe infact alikuwa anafanikisha mpango wa kumuokoa mwanadamu.

Shetani bado hajajifunza.Vurugu zote hizi hatimaye zitaishia kwenye kulijenga hekalu la tatu na la mwisho la Wayahudi,in which the so called Jewish Messiah,who will infact be the Antichrist au Dajjal kwa wengine, will rule humanity for a while,seven years to be exact.Baada ya hapo mfumo huo ambao utakuwa wa kipepo proper,utasitishwa by binding the Devil for a thousand years by God himself,in which period Jesus Christ will rule from the holy city of Jerusalem!After the 1000 years which will be of complete peace and tranquillity,Satan will be unbound for a while,but will again collude with humanity to attack the holy city of Jerusalem.God will not withstand this nonsense anymore.He will engulf Satan with eternal fire where with his followers(evil angels and evil humanity)will be tormented for ever.

The present heaven and earth will be completely obliterated,and he will create a new heaven and earth.God will then descend a new Jerusalem to exactly the same spot where the present Jerusalem stood and will live there with His holy people for ever.So you see, this is why Satan is creating all sorts of conflicts so as to derail Gods' plan.This is a conflict between good and evil.

But as I have said,he will fail,just as he failed in preventing Gods' plan for Salvation.Praise God.

Friend,having heard of this magnificent plan of God, why don't you surrender your life to Jesus,so that you can be part of Gods people in the holy city.Just say this simple prayer loudly and you will have received salvation:

Dear Jesus,I have understood your magnificent plan for the holy city of Jerusalem.I know that If I will have lived to the day when Satan's army would destroy your holy City,I would be part of the army to destroy your holy city.I today believe that you died for me on the cross and through the shedding of your blood on the cross, my sins are forgiven.I also believe that you are the son of God.I accept you as my Lord and saviour.Amen.

If you have prayed this simple prayer,believe that you are saved and that you are now a son of God.Find a Church which truly believes in Jesus Christ and participate in daily services.
 
Nitasujudu,nikilikabili hekalu lako takatifu,nitalishukuru jina lako. (Acheni tuone Mungu wa Israel kama kweli yupo,tutajua tu.) Sidhani kama Elia alikosea kumuita akitaka mungu Baali ajipambanue.
 
ilikua zamani saivi huo mji hauni hiyo dadhi tena.
Kumekuwa na mzozo wa muda mrefu kuhusu udhibiti wa mji wa Jerusalem kati ya Waisraeli na Wapalestina.

Mji huo kwa sasa huwa umegawanywa mara mbili, Jerusalem Mashariki na Jerusalem Magharibi.

Jerusalem ya Magharibi hutazamwa na Israel kama mji wake mkuu nayo Jerusalem Mashariki hutazamwa kuwa mji mkuu wa taifa la Wapalestina (litakapoundwa), ingawa eneo hilo bado kwa kiwango kikubwa limetawaliwa na Israel tangu vita vya 1967.

Tangu wakati wa vita hivyo, Israel imejengwa nyumba za walowezi wa Kiyahudi takriban 200,000 ambao huishi Jerusalem Mashariki, hatua iliyoshutumiwa na jamii ya kimataifa. Eneo hilo huishi Wapalestina takriban 370,000.

Israel ilitangaza 1980 Jerusalem yote kuwa mji wake mkuu wa milele, lakini nchi nyingi duniani hazikubali azimio hilo.

Hivyo basi, balozi za nchi za kigeni katika Israel ziko nje ya Jerusalem, katika mji wa Tel Aviv.

Mzozo huo umefufuliwa tena kutokana na hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani kutarajiwa kuutambua mji huo kama mji mkuu wa Israel.

Mataifa mengi ya Kiarabu yameshutumu hatua hiyo ya Bw Trump na kusema itazidisha uhasama Mashariki ya Kati.

Lakini ni kwa nini mji huu huzozaniwa hivyo? Mwandishi wa BBC Erica Chernofsky anachambua.

Dini tatu
Mji huu huwa na umuhimu mkubwa kwa dini tatu kuu - Ukristo, Uislamu na Uyahudi. Dini zote tatu humuangazia Abraham anayetajwa kwenye Biblia na Koran kama mmoja wa waanzilishi au mababu wa imani.

Ni mji ambao umedhibitiwa na dini hizo kwa vipindi mbalimbali katika historia.
Kwa Kiebrania, mji wa Jerusalem hufahamika kama Yerushalayim na kwa Kiarabu al-Quds. Kwa Kiswahili, jina lake halisi ni Yerusalemu. Mji huo ni miongoni mwa miji ya kale zaidi ambayo ipo hadi sasa duniani.

Ni mji ambao umetekwa, ukabomolewa na kuharibiwa na kisha kujengwa tena.

Kila sehemu ya ardhi yake ukichimba kwenda chini hufichua enzi fulani katika historia yake.

Ingawa umekuwa chanzo cha ubishi na mzozano kati ya dini mbalimbali, dini zote huungana kwa pamoja kuungama kwamba ni eneo takatifu.

Ndani yake kuna Mji Mkongwe, ambao una njia nyembamba, vichochoro na nyumba za kale. Kuna maeneo manne makuu na kila eneo, majengo huwa tofauti. Kuna eneo la Wakristo, Waislamu, Wayahudi na Waarmenia.

Eneo hilo huzungukwa na ukuta mkubwa wa mawe. Hapo, kunapatikana baadhi ya maeneo yanayoaminika kuwa matakatifu zaidi duniani.

Kila eneo kati ya maeneo hayo manne (unaweza kuyaita mitaa) huishi watu wa aina moja. Wakristo wana maeneo mawili, kwa sababu Waarmenia pia ni Wakristo. Eneo lililotengewa Waarmenia, ambalo ndilo ndogo zaidi kati ya hao manne, lina vituo vya kale zaidi vya Waarmenia duniani.

Jamii ya Waarmenia imehifadhi utamaduni wake wa kipekee ndani ya Kanisa la St James na nyumba kubwa ya utawala. Maeneo hayo mawili yamechukua sehemu kubwa ya mtaa huo wa Waarmenia.

Kanisa
Ndani ya mtaa wa Wakristo, kuna Kanisa Kuu la Kaburi na Ufufuo wa Yesu Kristo, ambalo ni muhimu sana kwa Wakristo kote duniani.

Hupatikana katika eneo ambalo lina umuhimu mkubwa katika kisa cha kusulubiwa, kufariki na kufufuka kwa Yesu.

Kwa mujibu wa utamaduni wa Kikristo, Yesu alisulubiwa hapo, katika Golgotha, au mlima wa Calvary. Kaburi lake linapatikana ndani ya kanisa hilo la kaburi na inaaminika kwamba hapo ndipo alipofufuka.

Kanisa hilo husimamiwa kwa pamoja na madhehebu mbalimbali ya Kikristo.
Sana huwa ni wahudumu wa kanisa la Kiothodoksi la Ugiriki, watawawa na mapadri wa Francisca kutoka Kanisa Katoliki la Roma na wengine kutoka kanisa la Waarmenia.

Kuna pia wahuudmu kutoka kanisa la Waothodoksi kutoka Ethiopia, Coptic na Syria.

Ni eneo ambalo mamilioni ya mahujaji wa Kikristo husafiri kila mwaka kwenda kuliona kaburi wazi la Yesu na kutafuta ufunuo na kuomba katika eneo hilo.

Msikiti
Mtaa wa Waislamu ndio mkubwa zaidi kati ya maeneo hayo manne na ndani yake kunapatikana madhabahu ya Dome of Rock (Kuba ya Mwamba) na Msikiti wa al-Aqsa kwenye eneo linalofahamika na Waislamu kama Haram al-Sharif, au Mahali/Hekalu Patakatifu.

Msikiti huo ndio eneo la tatu kwa utakatifu katika dini ya Kiislamu na husimamiwa na wakfu wa Kiislamu ambao hufahamika kwa Kiarabu kama Waqf.

Waislamu huamini kwamba Mtume Muhammad alisafiri kutoka hapo hadi Mecca usiku na aliomba pamoja na roho za manabii wengine wote. Hatua chache kutoka hapo kunapatikana Dome of the Rock (Kuba ya Mwamba) ambapo kuna jiwe la msingi. Waislamu huamini kwamba ni kutoka hapo ambapo Mtume Muhammad alipaa mbinguni.

Waislamu hutembelea eneo hilo takatifu kila wakati katika mwaka, lakini kila Ijumaa wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, mamia ya malelfu ya Waislamu hufika kuomba kwenye msikiti huo.

Ukuta
Katika mtaa wa Wayahudi, kunapatikana Kotel, au Ukuta wa Magharibi ambao ni masalio ya ukuta wa nje uliozunguka lililokuwa Hekalu Takatifu.

Ndani ya hetalu hilo kulikuwa na Patakatifu pa Patakatifu, eneo takatifu zaidi katika dini ya Kiyahudi.

Wayahudi huamini kwamba hapo ndipo kulikuwa na jiwe la msingi ambapo kutoka kwake dunia iliumbwa.

Kadhalika, wanaamini ni hapo ambapo Abraham alikuwa amejiandaa kumtoa kafara mwanawe Isaac. Wayahudi wengi huamini kwamba Dome of the Rock ndipo lilipokuwa eneo takatifu zaidi ndani ya hekalu lililofahamika kama Patakatifu pa Patakatifu.

Leo hii, Ukuta wa Magharibi ndilo eneo la karibu zaidi ambalo Wayahudi wanaweza kufanya maombi yao.

Husimamiwa na Rabbi wa Ukuta wa Magharibi na kila mwaka hutembelewa na mamilioni ya mahujaji.

Wayahudi kutoka kila pembe ya dunia hutembelea eneo hilo kuomba na kukumbuka utamaduni wao, hasa nyakati za siku kuu za kidini.

Ukuta huo pia hufahamika kama Ukuta wa Maombolezo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom