Kwanini Jamhuri iliyomshitaki kijana Issack isimshitaki mke wa waziri huyu?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,671
149,858
Baada ya kijana Issack wa Arusha kutuhumiwa kumtukana Rais Magufuli mtandaoni,Jamuhuri ilichukua jukumu la kumshitaki kijana yule na hivi sasa kesi iko mahakamani.

Katika kusimamia haki na usawa, ninatarajia mke huyo wa waziri kupandishwa kizimbani bila kuchelewa kwa tuhuma za kutoa lugha za matusi kwa askari polisi alieko kazini na pia kunaweza kuwa hata na kosa la pili la kujaribu kumzuia askari asitimize wajibu wake(wanasheria watatusaidia).

Hata hivyo,kwa mtazamo wangu, naomba nikiri kuwa Rais teyari ameshaweka mazingira magumu kwa mke huyu wa waziri kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Nasema hivi kwasababu,iwapo mama huyu ataifikishwa mahakamani na baadae mahakama ikamuona mama huyu hana hatia,basi uamuzi wa Rais wa kumpandisha cheo askari anaehusika na tukio hili utakua umeingia dosari tena dosari kubwa tu na unaweza hata kuibua utata.

Kwahiyo ukitizama kwa makini,uamuzi huu wa Rais unaweza kuleta tafsiri mbili tofauti.Tafsiri ya kwanza inaweza kuwa ni kuweka mazingira magumu kwa mama huyu kushitakiwa popote pale baada ya uamuzi huu wa Raisi na pili inaweza kuonekana ni kujaribu kumfariji na kumpoza askari husika kwa kumpandisha cheo ingawa teyari ametukanwa kama inavyodaiwa.

Hata hivyo,nakiri uamuzi huu wa Rais kwa nchi kama yetu ni jambo ambalo si la kawaida kwani Rais angeweza kukaa kimya tu kama ilivyozoeleka na hakuna lolote ambalo lingeweza kufanyika kwani sidhani kama askari huyo au hata Jamuhuri ingethubutu kumshitaki mke wa huyo waziri.

Vile vile,ingekuwa ni katika awamu zilizopita, askari huyo japo yeye ndio katukanwa kama inavyodiwa, angeweza kabisa kuadhibiwa yeye ama kwa kuvuliwa utraffic au hata kushushwa cheo kwa kujibishana na mke wa waziri na hapa ndio Raisi Magufuli anapoonekana kafanya jambo lisilo la kawaida ingawa nae bado hayuko sahihi sana katika uamuzi wake huu.

 
Mkuu Salary slip your absolute right kwa mujibu wa sheria hakuna mtu aliye juu ya sheria, alichofanya mke wa waziri ni criminal offence ilitakiwa ashitakiwe period
Raisi huwa anaagiza watu wachukuliwe hatua ila hapa kafanya vice versa.
 
Hivi wewe unaelewa kinachoendelea?Umesoma vizuri nilichoandika?

Nimekuuliza swali, jibu swali.

Ningekuelewa ni singekuuliza.

Sikuelewi kabisa unapojaribu kuhusisha mada ya Rais wa Tanzania kutukanwa na askari kupandishwa cheo kwa kutukanwa.

Kuna uhusiano upi?
 
Nimekuuliza swali, jibu swali.

Ningekuelewa ni singekuuliza.

Sikuelewi kabisa unapojaribu kuhusisha mada ya Rais wa Tanzania kutukanwa na askari kupandishwa cheo kwa kutukanwa.

Kuna uhusiano upi?
Mahakama gani imethibitisha kuwa askari huyo katukanwa?
 
Unaandika kama vile wote wanaopitia JF wanaelewa huyo Isaac ni nani na huyo mke wa Waziri kamtukana nini huyo askari au ni mke wa Waziri yupi.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?

Ni kweli kabisa Dada yangu, watu wanaanzisha thread bila kujua hadhira (audience) wanaelewa mwanzo wa stori ya mke wa waziri au hata huyo Isaac, kupashana habari tuzingatie uandishi 'rahisi' kwa kuzingatia zile ''W 5'' za uandishi-bora -ulio- rahisi ili watu waweze kujadili vizuri . Si bure nimeona mara nyingi wasomaji wa JamiiForums wakiomba ''Thread ijaziwe nyama'' ,''tupia picha'', ''video'', ''Linki Rais Magufuli: Askari wa Usalama Barabarani aliyetukanwa na Mke wa Waziri apandishwe cheo '' n.k ili waelewe.

Katika kuanzisha mjadala au kupashana habari tuzingatie hizo W- Tano za uandishi WHO (nani), WHAT (Vipi), WHERE (wapi), WHEN (Lini), WHY (Kwa nini /sababu) na W ya sita ni msomaji.

Mfano: Je hadhira au wasomaji inafahamu / ina kumbukumbu la tukio la mke wa waziri? Mke wa Waziri jina ni nani? Lini kafanya tukio? Wapi tukio lilitokea, Kwa nini mke wa waziri alianzisha tukio? n.k

Hivyo hivyo kuhusu wahusika wote ktk thread yako tujiulize inatimiza angalau W 3 kati ya W5 au 6 za uandishi-rahisi-bora? Wahusika '' Rais'', ''Askari'', ''Mke wa Waziri'', ''Mahakama'', ''Sheria''
 
Back
Top Bottom