Kwanini ilinibidi niache Shule

Mkuu London I tulikua wote hapo kwa Mr mng'ong'o
 
Hongera Kamanda kaza buti..check you tubes upate vitu vipya kuvutia wateja .usiishie kwenye Hizo model tu za sofa! Gangamala maisha si lelemama
 
Hao Microsoft ulio was cite nao WALIACHA shule..!!!

#YNWA
Embu acheni kumjaza ujinga.
Hao wa Microsoft hawajaishia form 2.
Hawajaacha shule ilhali kuandika basic vitu vya aeiou hawajui.
Those guys waliacha vyuo.
Na siyo vyuo tu ni Havard huko na Yale.

Sasa wewe unaanzaje kuwafananisha na huyo asiejua kuandika walau sentensi moja ya kiswahili? Asiyejua kujenga hoja akaeleweka.
Sasa anaacha shule anaenda kujifunza udereva wakati home hakuna hata pikipiki ya kupigia deiwaka.

Hata angejua huo udereva nani angemuajiri ikiwa cheti cha form four hana.
Cheti cha form four ni kama vile tunavyojenga nyumba lazima msingi.

Kafika kwenye fenicha kwa kubahatisha tu.

Haikuwa ndoto yake wala lengo lake.
 
My Soulmate, unanishauri nini mwenyewe nataka kuacha shule tu😀
 
Dogo bora ungemaliza hata form 4 tu sababu kuandika tu bado huwezi

All in all kuwa na uhuru wa kipato au uhuru wa elimu bora uwe na uhuru wa kipato hizi elimu kama unazo lakini hazikuingizii chochote ni ujinga tu

Ipi bora_Kuishia form 2 lakini unaingiza pesa nyingi kwa siku na kuwa na Phd lakini mfukoni huna kitu?
 

Best kwa jichofulani huyu ana uafadhari .unawaongeleaje wale wenye degree zao lakini wamebakia kuota kuajiriwa?
Unawaongeleaje wale walokacha shule na wamekuwa vibaka wanaua mtu aondoke na elfu 20? Bora huyu amejiongeza...huyu akiwa amesimama ajipige msasa asome masomo ya jioni Basi itamsaidia Sana! Mie kanibariki aisee
 
Mimi mwenyewe nampongeza kuonyesha uthubutu kuliko angeendelea kung'ang'ana na kitu ambacho hajui mwisho wake utakuwa vipi
 
Sema ulikuwa kiazi tu shule ukakubaliana na ukweli ukaona usipoteze muda. Tusichokijua ni kuwa si lazima na haijaandikwa popote kuwa ni lazima kila mtu asome hadi chuo, jambo ambalo hata huyo ndugu yako aliyesoma ardhi hakulifahamu. Akaenda shule bila kufahamu anahitaji nini huko shule, akahitimu na sasa hajui anaishi ili iweje! Wewe ulitambua kabla hujapoteza muda na visenti vya wazazi wako.
 
Reactions: amu
Angeenda shule asingefika hapo..
Shule imefuta ndoto za watu wengi sanaa.
C.Ronaldo anasema "niliambiwa nikiendekez mpira nikaach shule ningekua maskini ila Leo ni .......""

#YNWA
Unafeli sana kulinganisha elimu ya shule na bonafide kipaji kama cha C Ronaldo.....

Kipaji hasa cha sports huwezi chelewa zaidi ya 19years old...kwahiyo shule lazima isubiri otherwise kipaji kitaishia akiwa kwenye dawati...

Unafananisha na upumbavu wa kuchonga fanicha?

Kua serious ndugu yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…