Kwa jina naitwa Michael Luoga (chuma masofa ) mzawa wa Songea mkoani Ruvuma
Mimi ni mtoto wa kwanza wa familia ya watoto 5 mimi ni mtoto wa familia ya kipato Cha chini nimezaliwa mwaka 2000 nikapata elimu ya msingi katika Shure ya msingi madizini Songea mwaka 2015 nikahitimu na mwaka 2016 nikajiunga na Shule ya Sekondari Rondoni Songea maisha ya Shule yalikuwa mazuri nikamaliza mwaka wa Kwanza mwaka wa pili ulipoanza nkaendelea na masomo ila ilipo fika mwenzi wa nne niliacha shule
Sababu zilizonifanya niache shule
1. Niliona walio na elimu wakihangaika mtaani na hasa alikuwa binamu yangu alie kuwa kasomea masuala ya ardhi anazurula mtaani
2. Hali ya kimaisha ya familia yalikuwa magumu sana hivyo mahitaji ya Shure mzazi akuweza kukizi japo aling'ang'ana nsome tu ivyo ivyo nakumbuka niko form one nilienda Shure kiugumu sana na naingia form two mdogo wangu anaenifuata naye anaingia form one dah nikaona game hili gumu nikaamua kujivua japo nilipingwa Sana
3. Nilipima nikaona elimu ya mtaani inalipa kwa haraka endapo kama ntakuwa makini na serious na maisha
Maisha baada ya kuacha shule
Nilianza harakati za kutafuta hela ili nkajifunze udereva nilipoanza hizo harakati nakumbuka kulikuwa kuna kanisa linajengwa kata ya lizaboni songea nkapta ajila ya kumimina zege lakini mungu si asmani siku ya pili alifika kaka yangu mtoto wa mama mkubwa na tokaongea akanichukua nkaenda kujifunza kutengeneza sofa na safali nyingine ikaanza Apo
Maisha kuanza kwenye ufundi yalikuwa na changamoto nyingi na majalibu ila nlikomaa nayo na atimae nkawa fundi lakin lavel ya kiasi tu pale nkaanza pata fedha kidogo kidogo ndipo bahadae kidogo nkapata chansi ya kwenda wilaya ya mbinga kufanya kazi kwenye ofisi za Uncle Sam furniture TZ nkafanya kazi kwa mda wa mienzi kazaa lakin nako nkafel tena nlikosa malipo ya mda wote nlio fanya kazi zaid ya posho tu dah ikawa changamoto tena mahana nilitegemea mda nlio fanya kazi pale ile pesa ndo ingekuwa mtaji wa jufungua ofisi yangu lakn nkaangukia pua dah kwa leval ya ufundi niliyo kuwa nayo ilikuwa ndogo basi nikajitosa tena kwenda kujifunza zaidi nkaenda kujifunza kazi tena kwa novath samwel mmiliki wa bravo sofa sets
Mwanzo maisha nlio ishi na jamaa zangu kina novath yalikuwa mazuri na Wala sikujutia swala la kujifunza zaidi tukaenda enda lakini mbele ikawa changamoto tena kama kutengwa na kila lafiki wa mwanzo wa ofisi nlizo kuwa nafanya kazi na watu wa karibu na pia ikafika kipindi hata hao watu niliokuwa nao kwa muda huo nao kutoelewana nao na kufikia mwaka 2019 ikabidi niondoke nkaja zangu mafinga pasipo kujua namfata Nani wa ndugu wa jamaa wa kalibu
Maisha ndani ya mafinga yakawa magumu tofauti na nlivyo talajia nlicho amini nimeumbwa Wala sijajiumba ivyo maisha ni mzunguko iko siku nitapata tu nkasonga kibishi na baada ya miezi miwili nkafanikiwa panga chumba na baada ya hapo nkakutana na kampani ya kamkopo nikafungua ofisi na mbaka sasa naendelea vizuri na ninapata umaarufu wa kazi nzuri za fanicha co now nmewashika na wengine mkono wengine hata siwajui lakini naishi nao tukisaka chapaaa
Ushauli
Ukiona elimu aifai usilazimishe kwa kumlizisha mzazi au mwalimu fanya lengo lako kwa wakati na pia malufuku kukata tama mahana ukikubali kushindwa bas utaludi nyuma mala kumi zaidi lakini sikushauli uache shule apana soma Kwanza
Na kingine riziki yako inavyo kuja basi huvuta misili ya akili ielekee uko ukijiona unafaa basi na wanadam watakuona unafaaa so thanks I love u
With Michael luoga chuma ...meneger c.m.f sofa sets mafinga
Support vijana kwanza... Luck angel crew dancer
Saport pinga ukatili ..nasoma kwanza
View attachment 1541054