Kwanini Idara ya maji haina kitengo cha Dharula (Emergrncy)?

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
24,688
26,795
Hivi kwanini shirika la maji kusingekuwa na kitengo cha emegency kama tunavyoona Tanesco au Zimamoto kwa mfano moto ukiwaka sehemu fasta tunaona fire inafika kwa wakati au umeme nao yunaona ike emegency ya tanesco inafika.

Upande wa maji kuna sehemu unaweza pita ukakuta maji yanamwagika mengi tena kwa presure kiasi kwamba kama ni hasara hawa Dawasco wanaipata sana na inachukua muda/siku kuja kutengeneza hapo hadi mtu unajiuliza sehemu nyingine kuna uhaba wa maji lakini sehemu nyingine yanamwagikia chini tena mamlaka husika hata hawashughulikii.

Wakati mwingine unakuta maji yanamwagika (kwa mfano daresalam)
ukiwapigia labda bomba sehemu fulani maji yanamwagika wao wanakujibu hilo ni magomeni au ni kimara ndio wahusika unakuta maji zaidi ya siku 2,3mpaka wiki yanamwagika tuu.

Maoni yangu:
Hii idara iunde kitengo ambacho ni cha emegency kiasa kwamba popote ndani ya mko huu sehemu yeyote kama ni bomba lao kuna shida washughulikie hii itasaidia upotevu wa maji.hata wakipanga kikanda kama tunavyoona tanesco sio mbaya alimradi hili tatizo lishughulikiwe kwa wakati.
 
Back
Top Bottom