Tatizo ni jinsi ya kuachana, wengi tunaachana kimabavu mabavu tu ndio maana tunaishia kuitana kauli chafu chafu tena na kuibuliana madhaifu ambayo tuliyafumbia macho kipindi kile cha mahusiano yetu...
Wengi wa wapenzi ambao wako kwenye mahusiano huwa ni vigumu sana kuambiana madhaifu nyeti wanapokuwa kwenye relation, tabu huja pale wanapokuwa wameachana hasa kwa mmoja kumtenda mwenzie vibaya, hapo ndipo mambo yanaibuka tena ya soni kabisa!
I suggest, kama binti huna mpango nae, haina haja ya kuishi nae miaka mingi sana, huko ni kupotezeana muda tu!