Kwanini Hisa za CRDB hazifanyi vizuri sokoni?

Mulisaja

Member
Apr 21, 2012
32
3
Habari zenu wanajamii forum,
Nimekuwa nafuatilia kwa ukaribu sana hizi hisa za CRDB tokea mwaka 2016 mwezi wa 7 naona hazipandi ila zinazidi kushuka sana.Kwa mfano ukiangalia report ya mauzo ya hisa kwa tarehe 5/7/2016 inaonesha hisa za CRDB iliuzwa kati ya shilingi 295 na 300 kwa hisa moja.Sasa imeendelea kushuka kwa kasi sana na ukiangalia report ya jana tarehe 28/03/2017 hisa moja ya CRDB imeuzwa kwa shilingi 185.Nataka kujua kwa wanaofahamu nini shida ya hisa za CRDB kuwa zinashuka tu badala ya kuapanda.maana ukiangalia hisa za makampuni mengine yanashuka ila sio kwa kasi na kupanda pia.
 
Mimi na hela zangu za manati manati....niliona biashara ya hisa bongo ni kutafuta magonjwa ya presha!

Ila nadhani vile vile Kimei should step down. Khaa...for the past twenty years bado ni DG wa CRDB? Also for CRDB, corporate governance is zero!
 
Kwauelewa wango soko la hisa linafuata zile rules za demand na supply. Kukiwa kunademand ya hisa za crdb ndo bei yake inapanda kwasababu muuzaji atakuwa anaiuza kwa bei ya juu na mnunuaji atakuwa teyari kulipia. Ikitokea hakuna demand pia anayeuza itabidi auze kwa bei ya chini ili amvutie mnunuaji. Hapo ndo panasababisha bei kushuka. Pia soko la hiza linasukumwa na habari zinazotoka kuhusu shirika kwahiyo zikiwa zinakuja habari nzuri pia zinasaidia kuzifanya hisa kuvutia kununuliwa. Kwa kasi ya crdb inaonyesha baada ya uchaguzi watu waliuza sana hisa zao nabado wanauza. Sasa hao waliokuwa wanatoa mahela Yao huko ndo walisababisha kitu kikaporomoka, sijui ndo wale walienda chimbia chini??
 
Moja ya sbb kubwa sana ni composition ya hisa za crdb...yaan kuna majority watu kwa maana ya individuals wenye hisa...tofaut na makapuni mengine ambyo wamiliki wa hisa ni tasisi na serikali....kwa hawa individual huwa wanauza sana hisa zao...yaan wakipata shida kidogo tu wanauza hisa au kwa sababu ya kupata gawio dogo kutokana na hisa zao basi wanazipeleka sokon....hii ni tofaut sana kama hisa nyingi au niseme zote zingekuwa zina milikiwa na makampuni, taasisi au serikali ambapo maamuzi ya kuuza hisa ni mchakato mrefu.

Nasema hii ni mojawapo ya sababu...zinaweza zikawepo nyingine nyingi
 
Well spoken
 
Naona hii itakuwa sababu kubwa pia,Asante sana kwa majibu mazuri
 
Naona hii itakuwa sababu kubwa pia,Asante sana kwa majibu mazuri
Asante sana. Kwa kuongezea tu...kwa mujibu wa taarifa ya shareholder wa crdb kwa mwaka 2016...44% ya share holder( about 28,000) individuals wanamiliki shares chini ya 1%. Hawa kwa maoni yangu ndo wanajazana soko la hisa wakiuza hisa.

Asante.
 
Mabadiliko katika mifumo ya kisiasa na uchumi nayo pia yanachangia sana kushuka kwa bei za hisa hasa kwa mfano misingi mingi mipya katika huu utawala katika masuala ya fedha na ya kibenki kiujumla nayo yamekuwa chachu kubwa katika kushuka kwa bei ya hisa za CRDB.
Mabadiliko katika sera za kiuchumi pia nchini nayo yamekuwa issue kubwa katika kushuka kwa bei kwa hisa za hii benki kama utakuwa mfuatiliaji sera zimeleta mfumuko wa bei na pia kumekuwa na mabadiliko makubwa ya riba katika mabenki ambazo zote zimeleta kubadilika katika magawio ya kibenki na mwishoni ndo hizo impact tunaanza kuziona katika bei za hisa katika hii benki.
 
Back
Top Bottom