Kwanini hawajui hili....??

Kwanini hawajui hili....??

sarawati

Senior Member
Joined
Dec 19, 2011
Posts
121
Reaction score
33
Kwa mda mwingi huwa nawashangaa wabunge wa CCM na hii mawaziri kwa kulalamikia kua wapinzani hasa CHADEMA wanatumia bunge kama sehemu ya kujipatia umaarufu.. Ila nimejaribu kufatilia kwa umakini nikagundua kua kuna kitu muhimu ambacho hawakijui.

Hawajui kua wabunge wa CHEDEMA wametumwa kutetea maslahi ya wananchi na kwakua hali ya maisha ya watanzania wengi si nzuri kabisa inapelekea wabunge wa upinzani kuponda au kukosoa mwenendo wa serikali wa kuendesha nchi. Hapo ndipo sisi wananchi tunapowakubali .

Na kwakua hapo hapo katika kutetea maslahi hayo wanajikuza kisiasa. Sasa hakuna kingine ambacho CCM inaweza kurudisha imani kwa wananchi kama wabunge wake wasipokubali kupitisha kila hoja mbovu ambayo inapitshwa na serikali
kwa kuipigia makofi...huku ikizomea hoja nzuri za kujenga na muhimu katika taifa hili.

Wabunge wa CCM watete wananchi sio wale wanaowanyonya wananchi kwanini, hawajui jambo dogo kama hili, watawezaje kujua yale makubwa yaliojificha? Hivi kurudia kusahihisha mitihan ya form 4 ndo kusaidia ukuaji wa elimu Tanzania? Mbona mambo mengne hayahitaji hata tunguli kuyatatua.

Nawakilasha...
 
Back
Top Bottom