casaNostra, nivema ungeweka hayo uyasemayo kwa ujazo ili nami nipate kujifunza kutoka kwa yale utakayo yaleta jamvini.
Ingependeza zaidi iwapo utatufafanulia hicho unacho mipango ya kuangusha serikali 1983 kama unalivyo ahinisha.
Jaribio/ Njama/ Uasi wa Jeshi, yote hayo yalimlenga Mwalimu.
Na sitaki kuamini kwamba haya yalitokea pasipo sababu, na hapa ndipo napata kuamini kwamba Jk ndie aliekua sababu mpaka kupelekea haya kutokea.
Kingine naona ume mention matukio haya mwaka 1983 na 1964. Je, hapakuwahi tokea tukio kama hilo au lakufanana na hayo katika wakati tofauti na 1983, 1964?
Nikirudi kwenye lengo kuu la kuleta Uzi huu hapa ni:-
Kwanini matukio haya hayakuwekwa kwenye vitabu vya historia?
Kwanini hatukufundishwa mashuleni walau tupate kujua yalio tokea kwenye historia ya nchi yetu?
Kwanini kama sio kweli serikali haujawahi kukanusha?
Kwanini matukio haya yalifichwa?