Good idea!!!siku tifu linalipuka ni kuwafuata New Habari Corporation na RA na kuwapa kipigo humohumo ofisini mwao
Nani mwenye nguvu ya kumfungia ROSTAM AZIZ
Gazeti la rai katika toleo lake la leo limeendelea kuandika habari zinazomhusisha mgombea wa chadema katika nafasi ya urais (dk slaa) na maaskofu.
Eti sasa wanadai wabunge waislamu wa chadema walimsusia dk slaa kwenye mikutano yake baada ya kuchukua fomu. Habari hii ya kutungwa ni ya hatari sana kwani inaweza kuchochea uhasama wa kidini na kulitumbukiza taifa letu kwenye machafuko.
Gazeti hili linaloendelea kupoteza umaarufu kwa kasi kubwa linamilikiwa na mtu anayesadikiwa kuwa ni raia wa iran aitwaye rostam aziz. Huyu hana uchungu na nchi hii kwani anajua sio nchi yake, hivyo hata yakitokea machafuko atakimbilia kwao.
Ni matumaini yangu kuwa waziri wa habari, afande mkuchika ameliona hili na atachukua hatua za haraka kulifungia gazeti hili haraka. Tunasubiri.
Dr. W.P. Slaa pekee
CCM imekosa sera. Nyerere aliwahi kusema kuwa mtu akishakosa sera anakimbilia kwenye ubaguzi; nakubaliana kabia na mzee yule. Utaona mtu anajinadi kwa wapiga nkura akisema tusimchague fulani kwa sababu ni Mpemba, tusimchague fulani kwa vile ana asili ya bara, tusimchague fulani kwa vile ni mnyamwezi. Ubaguzi mwingi wa aina hiyo umekuwa hauna nguvu sana nchini kwetu kutokana na misingi imara iliyoachwa na Nyerere, na vile vile wingi wa makabila yetu kiasi kuwa hatuna vuta nikuvute ya dominance ya kabila moja. Hata hivyo tukishaanza kubaguana kwa mtindo wa dini, kwa vile hiyo itakuwa inahusu block kubwa sana ya watu, na ni jambo ambalo ni explosive sana, basi nechi inaweza kuwaka moto. Sijui kama serikali ina viongozi kweli kwa sababu hili ndilo jambo la kitaifa la kukekemea zaidi kuliko kukemea kuwa waziri akizungumzia ngono asiandikwe.
Mwanzoni mwa utawala wake Kikwete aliwahi kuzungumzia kurudisha misingi ya utaifa iliyojengwa na Nyerere ikiwa ni pamoja kuimarisha mfumo wa elimu isiyojali dini wala kabila kama yeye alivyosomea kwenye shule za wakatoliki akiwa mwislamu. Sasa naona kwa vile karata hiyo ya udini inaweza kumsaidi kisiasa, huenda serikali yake ikakaa kimya kuhusu hilo.
sijaliona bado ila ni kitu kibaya sana ktk nchi hii, akumbuke kua cuf hawakupata mbunge hata mmoja bara baada ya kuanza kuleta za namna iyo, ina maana anaanza kutuambia kua wakristo wote kumbe waanze kuangalia viongozi wa kuwachagua kwa dini zao maana kumbe wa dini ya kiisalma hawatamchagua slaa kwa sababu ni mkristo? je kwa kauli yake ina maana sasa makristo irrespective of chama waanze kuchagua wakristo wenzao si kwa sababu ya uwezo au vigezo vingine ila ni dini tu? maana kwa habari iyo theme kubwa ni suala la dini, maana hajazumgumzia suala lolote la kisiasa bali dini! this is terrible, tunaenda wapi, to be honest i never knew wako desperate kiasi ichi kumzima slaa! wao si wanauhakika na kucheka wao, si wasubiri!
...Eti sasa wanadai wabunge waislamu wa chadema walimsusia dk slaa kwenye mikutano yake baada ya kuchukua fomu. Habari hii ya kutungwa ni ya hatari sana kwani inaweza kuchochea uhasama wa kidini na kulitumbukiza taifa letu kwenye machafuko...
.