Mkuu, malengo ya syndicate ya Elon na wahuni wenzake ni meusi kuliko unavyodhani.
Kamwe katu usiipime nia ya mtu kwa kigezo tu cha kujificha kwenye huduma za jamii.
Ni kweli utawala wa Trump unafanya vizuri kwa sasa, licha ya kelele nyingi za wapinzani na waliokamatika plus vitisho na hasara za Tesla anazopata Elon.
Nadhani kumwelewa Elon vizuri ni lazima mtu aelewe movie kama The Blacklist - Raymond Reddington anaiteka serikali ili kusaidia kupambana na maadui wake na kuendelea kutanua kwa uhuru ufalme wake wa kihalifu.
Huyo ndiye Elon Musk.
Kuna mabwanyenye wachache wanaitaka Marekani yote na dunia nzima iwe mikononi mwao, bila kubugudhudhiwa na yeyote.
Maamuzi watakayofanya wao ndiyo maamuzi ya wote - wanafanya maamuzi kwa niaba ya umma.
Hili ndilo lengo lao kubwa namba moja - utii usio na swali katika jambo lolote waamualo!
Unadhani kwa nini kuna harakati za kuhamia Sayari ya Mars?
Kama tuna uwezo wa kuifanya sayari nyingine kudumisha uhai, kwa nini tusiifanye dunia (inayosemekana kuelekea kufa) iweze kuendelea ku-support uhai?
Hivi si kwamba kuna mpango wa siri wa ^kuisafisha^ dunia???
Elon Musk ni nani na anafanya kazi chini ya mwavuli na kanuni na malengo gani hasa?
Haya ndiyo maswali ya msingi kwetu kujiuliza kwa kina.