Kamukhm
JF-Expert Member
- Aug 30, 2015
- 2,799
- 4,200
Soko la hisa la DSM (DSE) linaendelea kukua kwa kujikongoja ukilinganisha na Masoko ya Nairobi(NSE), Johannesburg(JSE) na Kigali (RSE); wakati uwekezaji nchini ukiendelea kukua steadily. Shida ni Nini?
Kwa wale wataalamu wa maswala ya Masoko ya Dhamana, Je, hakuna uhusiano wowote kati ya ongezeko la uwekezaji na ukuaji wa masoko ya mitaji na dhamana!?
Mawazo binafsi.
Taratibu Dhaifu za kimamlaka katika kusimamia miliki, za Ardhi na vibali vya uendelezaji miji zinachangia kwa sehemu kubwa kuondoa mazingira rafiki kwa wawekezaji wazawa na wageni, kwa ujumla.
Mfano; katika eneo la Ardhi, swala la Serikali kufuta miliki, kila inapojisikia hasa kwenye maeneo yenye uvamizi, inaathiri "Imani" Kati ya wawekezaji na Mifumo ya Usimamizi wa Serikali; ambayo nadhani inayo athari ya moja kwa moja na hali ya uwekezaji nchini.
Kuna scenario nyingi ambazo ukizifikiria unakosa majibu;
Mtanzania anadunduliza pesa anajinyima.. ananunua ekari 500 kwa ajili ya Kilimo. Serikali inammilikisha baada ya kukamilisha taratibu zote. Anaanzisha Kampuni anaingia ubia na kampuni nyingine kukuza mtaji wanaanza uzalishaji na kusogeza miundombinu muhimu Kama maji, umeme na Barabara.
Hapo eneo hilo ambalo awalo lilikuwa shamba pori; linaanza kupata thamani, mara (Kupe) wanaanza kuvamia. Miaka mitano tayari wamejaa.
Mwenye mali anafika awaondoe kupanua operation, Wananchi Hawa(kupe) wanakimbilia kwa viongozi wa kisiasa, ghafla muwekezaji analazimishwa kugawa sehemu ya Ardhi yake, (aliyonunua kihalali na kuaminishwa na serikali kuwa anaweza kuitumia kwa miaka 66/99) kwa wananchi bure(kisa tu ni wapiga kura).
Hii inahuzunisha na Inaathiri uzalishaji na mipango ya baadae ya makampuni na uwekezaji kwa ujumla.
Nadhani hii kutokuwa na hakika ya kesho kwa uwekezaji hasa kwenye eneo la Ardhi na kutokuwa na mifumo inayoweza kutabirika kunayo athari ya moja kwa moja na ukuaji wa soko la dhamana na mitaji nchini.
Kwa Kenya katika hili wametuacha sana, Kama ilivyo kwa South Afrika na Rwanda nao wameamka na tunaona toka wametoka kwenye vita wanapiga kasi nzuri na ni kwa kusimimamia mifumo sio kudekezana.
Mwisho: Naomba kusikia kutoka kwa wajuvi, manguli wa mada hii. Lakini kwa wale watetezi wa kupe nitoe Rai..ukivamia shamba la mtu au kiwanja huo ni wizi. Flat out. Ukitetea ujue unatetea wizi.
Ahsanteni.