KERO Kwanini DAR haina maji ilihali mto RUVU umefurika? Wakazi wa Kimara, Mbezi, Tabata, Tegeta, Kunduchi, n.k hatuna maji mwezi wa tatu sasa!

KERO Kwanini DAR haina maji ilihali mto RUVU umefurika? Wakazi wa Kimara, Mbezi, Tabata, Tegeta, Kunduchi, n.k hatuna maji mwezi wa tatu sasa!

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mkono Mmoja

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2019
Posts
3,958
Reaction score
7,697
Tulitangaziwa mgawo wa maji toka mwezi wa 10 chanzo kikubwa kikiwa ni upungufu wa maji katika mto Ruvu. Cha ajabu na kushangaza ni kuwa Mto Ruvu hivi sasa umejaa maji mpaka juu kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika vyanzo vyake ila mpaka sasa hali ya upatikanaji wa maji imekuwa ni ya kusikitisha na ya tabu mno.

Tunakaribia mwezi wa tatu hivi sasa wanaishi pasi na upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama. Dumu moja la lita 20 itakupasa umlilie bodaboda shilingi 1,200 ili akakuchotee kitu kinachopelekea hali ya maisha kuwa ngumu kwasababu hakuna maisha pasipo na maji.

Wakazi wa Mbezi, Kimara, Tabata na maeneo mengine ya mkoa wa Dar tunaitaka Serikali ieleze tatizo ni nini linalofanya huduma ya maji isipatikane.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso anapotoa matamko kuwa upatikanaji wa maji utarejea, huwa anatuma wachunguzi wake wafuatilie kama maji yanatoka kweli?

Bili za maji bado mnatuletea kama kawaida halafu maji hayatoki, tunashangaa hizi bili ni za nini?

Wakuu tumechoka na hii KERO....ukiishi Kimara, Mbezi na Tabata itakupasa ukaogee Beach au nje ya mkoa wa Dar-es-salaam.

Waziri Aweso toka ofisini uone matatizo ya Maji katika Jiji la Dar-es-salaam yalivyo makubwa.

Msije na kauli kuwa mto Ruvu hauna maji ilihali tunapita hapo Daily na tunauona mto umejaa maji.

Nawasilisha.
 
Serikali ilioua watu iliodhaifu na kuua watu haiwezi fanya jambo la muhimu kwa raia then imeona haitoshi imeona njia nyingine ni kupitia kwenye maji
wa mama na watoto wanahaha kusaka maji bila ya mafanikio yoyote...hii hali inauma sana
 
Hii ni tiketi ya watu kutoka road sema Tanzania sio Kama Kenya kule wakenya waliachana na ng'ombe zamani mno wapo wamesoma na wengi mno wapo nje wanajitambua. Yaani tz bado sana ndio kwanza watu wametoka porini na wengi bado wapo vichakani wanachunga ng'ombe
hatujielewi tunataka nn
 
Hii ni tiketi ya watu kutoka road sema Tanzania sio Kama Kenya kule wakenya waliachana na ng'ombe zamani mno wapo wamesoma na wengi mno wapo nje wanajitambua. Yaani tz bado sana ndio kwanza watu wametoka porini na wengi bado wapo vichakani wanachunga ng'ombe
una uhakika haujapotea thread? Maana ulichokiandika hata hakieleweki!
 
Dar gani haina Maji? We uko matombo huko unajuaje ya Dar?
 
Tanzania ya malalamiko. Viongozi wanalalamika, wananchi wanalalamika ni full malalamiko.

Basi sawa.
 
Back
Top Bottom