Simiyu Yetu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2013
- 18,949
- 4,645
Mkuu we hewa kweli ambacho sijui nini hapo nilijua utatoa data unazojua lakini umetokwa povu tu.Hujui kitu. Kuzindua mradi hadi mwenge? Ina maana mwenge ukizimwa huwa hakuna miradi? Hivi wajua mwenge ukiwashwa hadi kuzimwa unatumia sh. ngapi ukimbizwa mikoa yote au ni wachache kupata posho.?
Kwanini CCM wanaupenda Mwenge wa Uhuru? Fikiri kwanza kuhusu faida na hasara yake
Mkuu umepinga nini na umekubari nini,sioni kama kuna gharama zozote za kuendesha mwenge ukilinganisha na faida zinazopatikana.Mkuu naamini kwa sasa mtu yeyote yule ambaye sio fisadi lazima atachukia mbiovza mwenge,hivi unajua ni kiasi huwa kinakimbiza huu mwenge,zamani tuliambiwa ulikuwa unamulika ili kutuletea tumaini,hakika kwa sasa sijaona tumaini lolote linaloletwa na mwenge,sijui kama ulishawahi kusoma post moja ililetwa hapa kuonyedha gharama za kukimbiza mwenge katika kawilaya kamoja tu kama sikosei,ni aibu mkuu.......Mwenge umekuwa uchochoro wa vifisadi vya CCM vinavyochipukia huko mikoani,wilayani na kwenye vitarafa,si ndio sifa ya CCM.....kikweli mwenge umepoteza hadhi yake ipo haja ya kuangalia utaratibu wa kukimbiza hii kitu kama ipo haja ya kufanya hivyo.
Mkuu hawa bavicha wanahitaji shule kubwa kuyaona haya,lakini tusichoke kuwapa shule.CCM is just preserving one among the national emblems, Uhuru torch was introduced symbolically to shine the country and across the borders, to bring hope where there is despair, love where there is enmity, and respect where there is hatred!! we race it across the country to remind us of our roots as a nation...sasa kama unapingana na haya mawazo chanya, nitashangazwa na uzalendo wako.
Ukiona mtu anatafuta manufaa binafsi huyo ni mbinafsi na mchoyo hapaswi kuwepo kwenye jamii ya kistarabu.Wewe binafsi jiulize huo mwenge unakusaidia nini?
hili liko wazi chadema ni wapinga maendeleo hatushangai kupinga maendeleo yanayofanywa na serikali.