Kwanini CHADEMA kimevuka mwaka 2012 bila kusambaratika?

Kwanini CHADEMA kimevuka mwaka 2012 bila kusambaratika?

Makala Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2011
Posts
3,395
Reaction score
1,112
Habari za mwaka 2012 wanabodi! Ningependa tujadili matukio hatari kwa upinzani mwaka 2012.

1.MGOMO WA MADAKTARI; Nakumbuka CHADEMA kiliunga mkono mgomo huo ambapo watanzania wengi walipoteza maisha.Lengo lilikuwa ni kuishinikiza serikali itatue kero katika sekta ya afya ili migomo isijirudie mara kwa mara.Serikali ilichukizwa na msimamo wa CHADEMA na kuanza kuwatumia mashushushu kusambaza ujumbe eti CHADEMA wanafurahia vifo.

Hata Dr.Ulimboka alipotekwa,kuteswa na kutupwa mabwepande; Serikali ya CCM ilianza propaganda eti Ulimboka alitekwa na WANACHADEMA waliovalia magwanda ili wananchi kuichukia serikali.Mwishowe ukweli ulisimama pahala pake,CHADEMA kilisimama.

2.MBIO ZA M4C ;Chama kiliendesha vuguvugu la mabadiliko ili kuhimiza umma kuunga mkono upinzani.CCM kiilianza hujuma.Bila shaka mtakumbuka vifo Iramba,Morogoro na Iringa.Lengo ni kuihusisha freemasonry na CHADEMA eti damu inamwagika wananchi wakiogope chama hicho.CHADEMA kimeshinda majaribu, Je CCM hakitajutia jambo hili?
 
Habari za mwaka 2012 wanabodi! Ningependa tujadili matukio hatari kwa upinzani mwaka 2012. 1.MGOMO WA MADAKTARI; Nakumbuka CHADEMA kiliunga mkono mgomo huo ambapo watanzania wengi walipoteza maisha.Lengo lilikuwa ni kuishinikiza serikali itatue kero katika sekta ya afya ili migomo isijirudie mara kwa mara.Serikali ilichukizwa na msimamo wa CHADEMA na kuanza kuwatumia mashushushu kusambaza ujumbe eti CHADEMA wanafurahia vifo.Hata Dr.Ulimboka alipotekwa,kuteswa na kutupwa mabwepande; Serikali ya CCM ilianza propaganda eti Ulimboka alitekwa na WANACHADEMA waliovalia magwanda ili wananchi kuichukia serikali.Mwishowe ukweli ulisimama pahala pake,CHADEMA kilisimama. 2.MBIO ZA M4C ;Chama kiliendesha vuguvugu la mabadiliko ili kuhimiza umma kuunga mkono upinzani.CCM kiilianza hujuma.Bila shaka mtakumbuka vifo Iramba,Morogoro na Iringa.Lengo ni kuihusisha freemasonry na CHADEMA eti damu inamwagika wananchi wakiogope chama hicho.CHADEMA kimeshinda majaribu, Je CCM hakitajutia jambo hili ?
hebu rejea sehemu zenye bold nyekundu kisha uweke wazi kama umeziandika hivyo kwa bahati mbaya au kukusudia.
 
[QUOTE=betlehem;...Hakuna kiliandikwa kwa bahati mbaya labda kama hukuwepo nchini na umeingia JF December,2012. Msimamo wa CHADEMA ni kwamba rasilimali za nchi ziwanufaishe wananchi, hivyo hata kipindi cha mgomo wa madaktari msimamo wa chama ulikuwa kuitaka serikali iwasikilize na kutekeleza madai yao kwa manufaa ya wananchi wote.Nina wasiwasi,hukuyajua madai ya madaktari ndiyo huelewi haraka. Suala la watu kufa halina mjadala,nakumbuka kipindi hicho ccm kilikuwa kinaadhimisha miaka 35 jijini Mwanza na Mhe.Kikwete alikuwepo licha ya kwamba hakulizungumzia kabisa suala la mgomo.Bugando huduma haikuwepo na kuna wakati maaskari walizuia waandishi kupiga picha eneo la hospitali. Kuhujumiwa kwa M4C hakuna asiyejua hata mwanaccm. Mfano siku CHADEMA wanazuiwa mkutano Iringa kwa kisingizio cha zoezi la sensa, ccm walizindua kampeni za uchaguzi mdogo,Bububu Zanzibar.Kuhusu propaganda za kuhusisha CHADEMA na vifo Nape Nnauye (ccm) alinukuliwa akisema M4C ni movement for Death.
 
Sabuni ina watu makini wanaoweza kutegua mitego ya CCM kiulaisi sana!!
 
Wana JF heshima kwenu wakuu!!
Ukweli ni kwamba CHADEMA tulianza na Mungu na tutamaliza na Mungu. Hivyo wanafiki wote na magamba yao wameshindwa,wanashindwa na wataendelea kushindwa. CHADEMA tumesimama imara.
 
Chadema ni ngùvu ya umma kweli c utani ,Chadema wanachokifanya 1,wanakingeja chama chao na kuwakabidhi wanachi tofauti kabisa na wenzetu magamba chama chao wanakabidhi kwa viongozi wao tena wa ngazi za juu hivyo chama walishakihamisha kwa umma 2,Chadema wayanenayo ni yale tu yanayoigusa jamii tofauti kabìsa na magamba wao wanahubiri matusi hilo liko wazi
 
Huwezi shindana na wana wa Mungu....... Palipo na Mungu kuna Mungu tu.
 
Ni kweli bila shaka kulikuwa na mkono wa Mungu,kama CCM hawakuwa na mpango wa kukizima CHADEMA,ilikuwaje mtu kama Wassira aseme msajili wa vyama vya siasa akifute CHADEMA? Hata Tendwa naye alicheza ngoma ya CCM ambapo CHADEMA iliwalazimu kusimamisha kufanya kazi pamoja na Tendwa (siyo ofisi ya msajili wa vyama vya siasa).Kwa mwendo huu kwanini tusijiulize,kwanini CHADEMA kimevuka mwaka 2012?
 
sabuni ina watu makini wanaoweza kutegua mitego ya ccm kiulaisi sana!!

na madhara yameanza kuonekana kwao ccm...rejea zomewazomea dhidi ya kinana na wenzake mikoani,maandamano ya lindi na mtwara ambazo zilikuwa ngome zao,ccm kutothubutu mtu kuvaa nguo zao na kudunda mitaa ya sumbawanga ambazo ndo zilikuwa ngome zao kuu(ukivaa unakula kichapo wanaitwa msaliti wa mabadiriko),ushindi wa kesi ya kihistoria ya mh. Lema,kuvurugika kwa masalia kama kundi wakilishi la magamba ndani ya cdm .............duh!!!!!mengi sana ongeza mengine.............................................................................................
 
na madhara yameanza kuonekana kwao ccm...rejea zomewazomea dhidi ya kinana na wenzake mikoani,maandamano ya lindi na mtwara ambazo zilikuwa ngome zao,ccm kutothubutu mtu kuvaa nguo zao na kudunda mitaa ya sumbawanga ambazo ndo zilikuwa ngome zao kuu(ukivaa unakula kichapo wanaitwa msaliti wa mabadiriko),ushindi wa kesi ya kihistoria ya mh. Lema,kuvurugika kwa masalia kama kundi wakilishi la magamba ndani ya cdm .............duh!!!!!mengi sana ongeza mengine.............................................................................................
Kwa mazingira haya,wajiandaye kuondoka kiulaini!
 
TUKUTUKU said:
Ni kweli Demokrasia inawataka waondoke kwa amani, lakini macho ya akina Steven Wassira,Mwigulu Nchemba na January Makamba yamejaa damu ya uroho wa madaraka kwa kuwa wanaamini watatawala milele, Je wataachia kilaini?
 
Nakwetu said:
Walikwepa uchaguzi upi mkuu,maana Arumeru CCM kilipigwa mtama,Kule Igunga CCM kilishinda kwa shida tena kwa hujuma za kugawa vyakula,kutishia wapiga kura kwa bastola na kueneza propaganda chafu kwamba CHADEMA wameingiza makomando toka Libya kwa ajili ya kuvuruga uchaguzi.Kati ya masuala hayo yalipelekea kutenguliwa kwa ushindi wa CCM.Je,kwa idadi ya kura na mazingira ya uchaguzi, tuamini bado CCM kina mvuto kwa wananchi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom