Kwanini CCM wanafurahiria Prof Lipumba kutaka kurudia uongozi CUF?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,252
8,003
Wakuu hili jambo linawafurahisha sana wanachama wa CCM ambao ni wapinzani sugu wa UKAWA, kuna nini hapo? Kinachowafurahisha CCM hasa ni nini juu ya mambo ya CUF?Wananufaikaje hapo?

HAPA YAWEZEKANA KUNA MAWILI MATATU;
1.Kuchochea mgogoro ndani ya CUF ili chama kipasuke vipande vipande CCM kupenya vizuri?
2.Kwenda kuvuruga UKAWA ambao wameendelea kua wamoja?
3.Kujua nini kinaendelea ndani ya chama hasa kuhusu mgogoro wa Zanzibar kwa manufaa yake binafsi au chama?
 
Ni haki yake ya kidemokrasia
 
MAHANJU hukumbuki issue ya zitto na Chadema jinsi CCM walivyokuwa wanam-support zitto.

Lipumba kashachelewa sana hakuna vyama vya msimu siku hizi labda aende UDP
 
Lipumba kwa kutunza heshima yake alikuwa akubali yaishe tu, abaki kuwa mwanachama wa CUF au atafute chama chengine,
Hizi siasa anazofanya anajiweka level ya Mrema, Hamad Rashid, na wengine wengine, nahisi ana deserve better than this kama anajitambua
 
Mkuu, nadhani pia ungejiuliza, kwa nini CHADEMA wanapinga Prof Lipumba kurejea uenyekiti CUF wakati hayo ni mambo yao ya ndani!
 
Mkuu, nadhani pia ungejiuliza, kwa nini CHADEMA wanapinga Prof Lipumba kurejea uenyekiti CUF wakati hayo ni mambo yao ya ndani!
Umewahi kuona Chadema wakitoa tamko lolote wakimpinga Lipumba? Matamko yote yanatolewa na viongozi wa CUF, sasa Chadema wanaingiaje hapo? Hata wakihusika kutoa ushauri kuna tatizo gani ilihali wote wameunganishwa na UKAWA?
 
No haki yake kumeza matapishi?kumbe PhD za siku hizi hazimpi mtu uwezo wa kutafakari?
PhD sio kitu siku hizi mkuu! Ni ukiwa na masters ukaongeza vimiaka vitatu na viutafiti kidogo tayari we ni Dr, Ukiwa senior kidogo unakua Prof. Wewe hukumwona Mwakyembe akimshambulia Sugu huku akidai hakumaliza shule. Unaweza kuamini kua Mwakyembe ni PhD holder kweli kwa jinsi alivyo?
 
Unavyosema "Phd sio kitu SIKU HIZI..."
Kwani huo utaratibu ulioutaja ni wa sikuhizi?
 
Mkuu, nadhani pia ungejiuliza, kwa nini CHADEMA wanapinga Prof Lipumba kurejea uenyekiti CUF wakati hayo ni mambo yao ya ndani!
Umeona wapi Chadema wakipinga, hata hivyo
Chadema wana maslahi na CUF kwa sababu CUF na Chadema ni washirika wa UKAWA,

tuambie CCM mna maslahi gani na Lipumba hadi mnasherehekea yeye kurudi CUF?
 
Wakuu hili jambo linawafurahisha sana wanachama wa CCM ambao ni wapinzani sugu wa UKAWA, kuna nini hapo? Kinachowafurahisha CCM hasa ni nini juu ya mambo ya CUF?Wananufaikaje hapo?

HAPA YAWEZEKANA KUNA MAWILI MATATU;
1.Kuchochea mgogoro ndani ya CUF ili chama kipasuke vipande vipande CCM kupenya vizuri?
2.Kwenda kuvuruga UKAWA ambao wameendelea kua wamoja?
3.Kujua nini kinaendelea ndani ya chama hasa kuhusu mgogoro wa Zanzibar kwa manufaa yake binafsi au chama?

na nyie mbona mmekuwa wanachama wa CUF ghafla , kutaka pro asirudi kwenye chama chake
 
ni aibu kwa Msomi kama Lipumba kutumika kama karatasi nyepesi inayotumika baada ya mtu kuwa amekula futari nyiiiingi na kisha kuhitaji kwenda kugawana na mende!
 
Kujua kwa nini CCM wanapiga debe la nguvu la kushinikiza CUF wampokee tena Profesa Lipumba kwenye nafasi ya uenyekiti, tujikumbushe kidogo kile kikao cha October mwaka jana kilichofanyika pale hotelini Peacock ambapo alitangaza kujivua Uenyekiti kwa madai ya kutoafikiana na ujio wa Lowassa kwenye Ukawa, wakati siku chache kabla alionekana kwenye vyombo vya habari akishangilia ujio wa Lowassa!

Tujikumbushe pia kuwa mara tu alipomaliza kikao hicho pale Peacock alikimbizwa moja kwa moja uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere ambapo alikwea 'pipa' kuelekea Kigali huku akiimbatana na 'bodyguards' kutoka KITENGO.

Vile Vile ilifahamika kuwa gharama zote za hotel alikofikia Profesa Lipumba kule Kigali ziligharimiwa na TI...SS.

Kwa hiyo hapo ndipo unapata jawabu ni kwa nini Chama Cha Majipu kinashangilia sana jaribio la Lipumba la kutaka kurejea CUF kwa nafasi yake ya Uenyekiti.
 
Back
Top Bottom