Hiki ulichokiandika kinathibitisha yale niliyoandika hapo juu kuhusu "Tanzania Bara" kuwa ya wote (sote) na Zanzibar kuwa na yale yake-haya ndio nimeyaita mazingahombwe. Ni serikali tatu tu ikiwapo ya Tanganyika ndio zitaondoa zengwe hili.
Nikiwa kama mmoja wa Wananchi wa Tanzania niliyefurahia wazo la kurejeshwa kwa Serikali ya Tanganyika lililopendekezwa katika Rasimu ya Katiba Mpya,Nimeshangazwa na baadhi ya Watanzania hasa wale wanaokipenda Chama Tawala kutokufurahia wazo la kurejeshwa kwa Serikali ya Tanganyika,Najiuliza ni kwanini CCM hawaitaki Tanganyika yetu irudi?