Kwanini binadamu wengine huzaliwa wakiwa na mkia?

Heci

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
3,483
5,815
mkia-3.jpg

Kila binadamu aliumbwa akiwa na mkia mdogo ambao hufyozwa na kutoweka tangu siku za mwanzo za uhai wake tumboni kwa mama.

Mkia huo ni miongoni mwa viongo ambavyo vipo ndani ya mwili wa binadamu lakini havina kazi yeyote.

Binadamu akiwa katika hatua ya kijusi, huwa na mkia ambao sio wa kudumu na hutengenezwa kati ya wiki ya 5 au ya 6 ya ujauzito na huwa na pingili kati ya 10 hadi 12 za uti wa mgongo.

Mkia-2.jpg

Japo kuna wanaozaliwa wakiwa na mkia lakini katika hali ya kawaida binadamu hatakiwi kuzaliwa akiwa na mkia kwani hufyonzwa au kupotea wakati wa mabadiliko ya ukuaji ndani ya tumbo ambapo hutengeneza mfupa (Coccyx), unaopotea ndani ya wiki 8 za kwanza za ujauzito.

Hadi sasa wataalamu wamegundua kuwa sababu kuu ambazo hupelekea mtu kuzaliwa na mkia ni, upungufu wa Folic acid kwa mama mjamzito, mabadiliko yasiyo ya kawaida ya taarifa muhimu za mwili pamoja na kushindwa kwa chembechembe nyeupe za damu katika kufyonza mkia wote kwenye wiki ya 8 ya ujauzito.

Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa, imebainika kuwa watoto wa kiume ndiyo wana nafasi kubwa zaidi ya kupatwa na tatizo hili ikilinganishwa na watoto wa kike.

Baada ya kuzaliwa mtoto, huonekana mfupa uliochomoza sehemu ya chini kabisa karibu na kiuno (kwenye makalio), mara nyingi huwa hakuna mifupa ndani yake, isipikuwa mishipa ya fahamu na damu inayozunguka ndani yake.

Matibabu ya tatizo hili huzingatia madhara yanayotokana na uwepo wa mkia huo. ambapo mtoto anaweza kufanyiwa upasuaji wa kuondoa kulingana na vipimo vitakavyo onesha.
 
Ahsante kwa taarifa...

Kwa ubishi wa binadamu wa siku hizi, wapo watakosema hiyo ni photoshop...

Cc: mahondaw
 
Biological; evolution of man, binadamu anaumbwa na mkia ko kipdi cha kukua kwake tangu kwa tumbo la mama nakuwa nao mkia na hata ww au mimi tuna mkia ila haijawa kam ya wanyama au viumbe wengine wenye mikia kutokan sisi hatukazi na hiyo mikia ndio maan haijadevelope, katika case kam hizo, hizo na emergence hata ww au mim ingenikutaa inatokeaga lakin Eventually Sote Binadamu tuna mikia ila haijawa devolped to kutoka na hakuna function na hiy mikia ki biologyia tunaitaaa..vestigial structures
 
Kwanini mkia haukukatika?
 
View attachment 1265578

Kila binadamu aliumbwa akiwa na mkia mdogo ambao hufyozwa na kutoweka tangu siku za mwanzo za uhai wake tumboni kwa mama.

Mkia huo ni miongoni mwa viongo ambavyo vipo ndani ya mwili wa binadamu lakini havina kazi yeyote.

Binadamu akiwa katika hatua ya kijusi, huwa na mkia ambao sio wa kudumu na hutengenezwa kati ya wiki ya 5 au ya 6 ya ujauzito na huwa na pingili kati ya 10 hadi 12 za uti wa mgongo.

View attachment 1265579

Japo kuna wanaozaliwa wakiwa na mkia lakini katika hali ya kawaida binadamu hatakiwi kuzaliwa akiwa na mkia kwani hufyonzwa au kupotea wakati wa mabadiliko ya ukuaji ndani ya tumbo ambapo hutengeneza mfupa (Coccyx), unaopotea ndani ya wiki 8 za kwanza za ujauzito.

Hadi sasa wataalamu wamegundua kuwa sababu kuu ambazo hupelekea mtu kuzaliwa na mkia ni, upungufu wa Folic acid kwa mama mjamzito, mabadiliko yasiyo ya kawaida ya taarifa muhimu za mwili pamoja na kushindwa kwa chembechembe nyeupe za damu katika kufyonza mkia wote kwenye wiki ya 8 ya ujauzito.

Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa, imebainika kuwa watoto wa kiume ndiyo wana nafasi kubwa zaidi ya kupatwa na tatizo hili ikilinganishwa na watoto wa kike.

Baada ya kuzaliwa mtoto, huonekana mfupa uliochomoza sehemu ya chini kabisa karibu na kiuno (kwenye makalio), mara nyingi huwa hakuna mifupa ndani yake, isipikuwa mishipa ya fahamu na damu inayozunguka ndani yake.

Matibabu ya tatizo hili huzingatia madhara yanayotokana na uwepo wa mkia huo. ambapo mtoto anaweza kufanyiwa upasuaji wa kuondoa kulingana na vipimo vitakavyo onesha.
Aisee
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom