Kwani tunaukubali UNGO huu wa CCM?

Kwani tunaukubali UNGO huu wa CCM?

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2008
Posts
1,941
Reaction score
1,011
Nimekuwa mara nyingi nasoma na kusikia watu mbalimbali wakisema kitu ambacho sikubaliani nacho labada mnijulishe vinginevyo kuwa "CCM imetutawala miaka 49 ama CCM imetutawala toka UHURU hadi sasa". Nani kathibitisha kuwa kauli hiyo ni ya kweli?

Ninachojua na ambacho ni UKWELI ni kuwa CCM ilizaliwa 5/2/1977 baada ya kufa rasmi(kuunganishwa) ASP na TANU. Je! Toka 1977 hadi leo ni miaka mingapi?
Hivi mmi nikiwa ni mgogo ambaye mama yangu ni mkaguru aliyechanganya damu ya mgogo(bibi) na mhehe(babu) na ikiwa wakati nazaliwa baba alikuwa na miaka 25 na sasa nina miaka 24, je! inamaanisha mimi ni mgogo kwa miaka 49?

Huo ninauita uongo wa CCM ilikionekane kuwa ni chama kilichotukuka kwa kukaa madarakani miaka mingi. Maana hata leo nikaamua kumuuliza KIngunge N Mwiru umekuwa mwanachama wa CCM kwa miaka mingapi? Akinijibu, kipumbavu, atasema kwa miaka 49 lakini , kwa hekima, atasema miaka 33.

Nawasilisha.
 
Kwa kifupi mzee, hata kama watakuwa wametawala miaka elfu, Lakini hakuna chama kingine kilichotawala kwa kureplace CCM,

Lakini chamsingi zaidi ni wametupeleka wapi? au ndo kuyumba yumba tu, na kujidai wanlinda amani
Kitu ambacho ni kiini macho -Intangible na huwezi kuelezea.
Miaka yao kukaa madarakani yawezekana ndo inathiboitisha kuwa wanahitaji mbadala wao wapumzike kidogo
na sasa kipo hoi kinaelekea bondeni kwa speedi ya 200km/h
waache wajidai na kuongeza miaka yao japo hata hiyo siyo CCM hii tuionayo sasa ndo imeanza. ingekuwa ndo hii ingekuwa ishan'oka siku nyingi, na wakoloni wangerudi kama wanavojisogeza kijanja sasa.
 
Umeongea nikacheka mkuu lakini point tupu mkuu! kimeshindwa kutekeleza yale yaliyokusudiwa na waanzilishi wake.
 
Back
Top Bottom