Kwani nchi hii haina watu wenye akili?

Kwani nchi hii haina watu wenye akili?

pureman2

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2019
Posts
1,491
Reaction score
2,563
Wakati mkiendelea na zoezi la sensa nawaomba watanzania mje na mjibu swali hili ambalo nimedhani litatuongezea upeo wa kutafakari.

Uchumi umekua kama jinamizi ambalo linaondoa usingizi wa wananchi wengi wakubwa na wadogo. Wakiteswa na njaa, magonjwa, ukosefu wa huduma za jamii za msingi ikiwemo makazi duni na kazi zisizo na staha.

Elimu duni inayopelekea wahitimu kupoteza muda shuleni na gharama kubwa licha ya wakihitimu kumaliza elimu zao pasina kuwa na maarifa na ujuzi wenye manufaa unoweza kutatua changamoto za maisha. Hili pia ni zigo ambalo kama taifa hatuna jawabu.

Mmomonyoko mkubwa wa maadili unaolitafuna taifa. Sio vijana wala wazee wote hakuna wa kumfunga kengele mwenzie. Kiwango kikubwa cha utumiaji wa vilevi na madawa, ndoa kuvunjika, uzinzi na uchangudoa, utoaji mimba na mengine kama hayo yanazidi kuliteketeza taifa.

Uongozi mbovu na ufisadi bado vinazamisha meli yetu ya maendeleo na kama taifa simuoni mwenye akili wakutusaidia kushinda changamoto hizi. Hajui ni sifa zipi kiongozi anapaswa kuwa nazo, viongozi kutamani kutumikiwa na sio kutumika, rushwa Ili kuwa kiongozi na ubadhilifu wa Mali za umma ni matatizo ambayo jamii yetu bado inatapatapa pasina majawabu

Je, hatuna wenye akili katika jamii zetu wakutupa solution za changamoto hizi?

Historia inaweka kumbukumbu ya philosopher waliowahi kuishi na kwa matumizi mazuri ya akili zao walizisaidia jamii zao. Je sisi hatuna watu kama hawa wenye ufahamu na akili nzuri ya kuleta majawabu? Je jamii yetu inawatambua watu wa namna hii, je kuna mifumo ya kuwabaini na kuwawezesha kufanya kazi hii ya kufikiri na kuja na majibu ya kimikakati?

Wako wapi philosopher hawa ambao wataanzisha community schools Ili wawaendeleze follower wao. Usinishawishi kuwa hawa philosopher ni akina Mtume Mwamposa, Mtalemwa, Jo Davie, Mzee wa Upako au askofu Mwingila?

Nauliza tena je jamii zetu hazina watu wenye akili?

Karibuni.
 
Ukiona vyaelea vimeundwa. Ukikuta kuna walakini kwa watu angalia uongozi mzima uko vipi.
Yangu miye haya hapa:

Muda wa mapinduzi vyamani ni sasa

Tunahitaji viongozi bora wa kuwaongoza si bora viongozi.
"Kiongozi mlamba asali, mwoga, mwizi, fisadi au mnafiki amkomboe nani vipi.

Ninakazia "asilaumiwe dobi kaniki ni rangi yake." Bila kusahau "mtoto umleavyo ndivyo akuavyo."
 
"Yani nikipata lile docho nitapiga pesa ya maana" ikiwa tu graduate anakuwa tayari na maono hayo we unatarajia nini?
 
Mleta mada hoja yako ni ya msingi sana.

Ukweli ni kwamba wenye akili wako, tena wengi tu. Tatizo ni taasisi iliyojimilikisha nchi inayoitwa CCM.

Kwa mujibu wa katiba yetu mbovu ni kwamba ili uweze kusimama kwenye ulingo wa siasa na kutoa kile unachoamini ni lazima uwe na kivuli cha chama cha siasa.

Ccm imetumia katiba mbovu tuliyonayo kuvidumaza kabisa vyama pinzani vya kisiasa.

Sasa, ili mwananchi msomi nguli mwenye nia ya dhati kabisa ya kuleta mapinduzi ya kifikra na kisiasa katika nchi hii aingie kwenye huo ulingo, mlango pekee ulio wazi ni kupitia CCM.

Ndani ya CCM, kabla hujatoa unalolijua kwa wananchi, ni lazima uiambie kwanza hii taasisi wakukubali au wakukatalie na kukupangia ya kuongea/kufanya.

Kwa mtindo huo inakuwa aliyesoma na asiyesoma wote wanakuwa kitu kimoja ndani ya CCM.
Hapo ndipo hii hoja yako inapoonekana wazi kwamba nchi haina wasomi, ukweli ni kuwa wasomi wapo ila wamenyang'anywa uwezo/elimu yao na mfumo wa CCM.

Jambo la kufanya hapa ni wananchi wote waliojitambua kupiga kelele kudai katiba mpya.
 
Mkuu hili swala ni la kidunia

Jibu ni Kwamba

" TUNAO WATU WENYE AKILI NA WENYE AKILI NDO WAMETUFIKISHA HAPA".
Naomba nikitulia nije nifafanue how and why?
 
Tatizo la watu wenye akili nyingi siyo majasiri kama wale vilaza. Na kwa bahati mbaya ujasiri wa wale vilaza ndiyo unaowapa nafasi ya kuaminiwa na jamii yenye vilaza wengi zaidi, na mwisho wa siku wanapata madaraka!

Na baada ya hapo, wenye akili hugeuka na kuwa mabubu, na watu wa kulalamikia chini kwa chini. Maana wakijaribu tu kuwakosoa hao vilaza kupitia maandiko yao, basi wanakiona cha myema kuni. Mfano mzuri ni yule mwandishi nguli wa Nigeria Wole Soyinka, Ben Saanane wa Tanzania, nk.
 
Wakati mkiendelea na zoezi la sensa nawaomba watanzania mje na mjibu swali hili ambalo nimedhani litatuongezea upeo wa kutafakari.

Uchumi umekua kama jinamizi ambalo linaondoa usingizi wa wananchi wengi wakubwa na wadogo. Wakiteswa na njaa, magonjwa, ukosefu wa huduma za jamii za msingi ikiwemo makazi duni na kazi zisizo na staha.

Elimu duni inayopelekea wahitimu kupoteza muda shuleni na gharama kubwa licha ya wakihitimu kumaliza elimu zao pasina kuwa na maarifa na ujuzi wenye manufaa unoweza kutatua changamoto za maisha. Hili pia ni zigo ambalo kama taifa hatuna jawabu.

Mmomonyoko mkubwa wa maadili unaolitafuna taifa. Sio vijana wala wazee wote hakuna wa kumfunga kengele mwenzie. Kiwango kikubwa cha utumiaji wa vilevi na madawa, ndoa kuvunjika, uzinzi na uchangudoa, utoaji mimba na mengine kama hayo yanazidi kuliteketeza taifa.

Uongozi mbovu na ufisadi bado vinazamisha meli yetu ya maendeleo na kama taifa simuoni mwenye akili wakutusaidia kushinda changamoto hizi. Hajui ni sifa zipi kiongozi anapaswa kuwa nazo, viongozi kutamani kutumikiwa na sio kutumika, rushwa Ili kuwa kiongozi na ubadhilifu wa Mali za umma ni matatizo ambayo jamii yetu bado inatapatapa pasina majawabu

Je hatuna wenye akili katika jamii zetu wakutupa solution za changamoto hizi?

Historia inaweka kumbukumbu ya philosopher waliowahi kuishi na kwa matumizi mazuri ya akili zao walizisaidia jamii zao. Je sisi hatuna watu kama hawa wenye ufahamu na akili nzuri ya kuleta majawabu? Je jamii yetu inawatambua watu wa namna hii, je kuna mifumo ya kuwabaini na kuwawezesha kufanya kazi hii ya kufikiri na kuja na majibu ya kimikakati?

Wako wapi philosopher hawa ambao wataanzisha community schools Ili wawaendeleze follower wao. Usinishawishi kuwa hawa philosopher ni akina Mtume Mwamposa, Mtalemwa, Jo Davie, Mzee wa Upako au askofu Mwingila?.

Nauliza tena je jamii zetu hazina watu wenye akili ?

Karibuni.
Mkuu! Umeongea vema! Watu unaowataka wenye akili, busara, maarifa na maono juu ya jamii tuliyomo na hatari inayotukabili huko mbeleni kama tutaendelea hivi, tupo! Mmojawapo ni mimi! Ila mfumo umetutema! Utaanzia wapi?
 
Wapo wengi sana sema kwa sasa jamii kutokana na kuharibika kwa familia imekuwa ni sehemu inayotengeneza raia vilaza sana.

Ila watu wenye hekima, busara, na wenye maamuzi ya utulivu wapo. Tuendelee kuipambania jamii kwa kila namna irejee katika standards.

Kuna philosopher m'moja alishasema kuwa Duniani uovu unazidi si kwasababu hakuna watu wazuri wa kupambana nao ila ni kwasababu watu wazuri wamekaa kimya kwa kutulia wakiwatazama watu wabaya wakiharibu dunia bila kuwadhibiti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nachotaka hao wenye akili wazionyeshe akili zao kwa kuanza kutoa mafunzo kwenye jamii. Ili watu wazione hizo filosofia zao .
 
Mkuu! Umeongea vema! Watu unaowataka wenye akili, busara, maarifa na maono juu ya jamii tuliyomo na hatari inayotukabili huko mbeleni kama tutaendelea hivi, tupo! Mmojawapo ni mimi! Ila mfumo umetutema! Utaanzia wapi?
Ebu tumia platform hii utuonyeshe wapi tunakwama na tunatokaje
 
Tatizo la watu wenye akili nyingi siyo majasiri kama wale vilaza. Na kwa bahati mbaya ujasiri wa wale vilaza ndiyo unaowapa nafasi ya kuaminiwa na jamii yenye vilaza wengi zaidi, na mwisho wa siku wanapata madaraka!

Na baada ya hapo, wenye akili hugeuka na kuwa mabubu, na watu wa kulalamikia chini kwa chini. Maana wakijaribu tu kuwakosoa hao vilaza kupitia maandiko yao, basi wanakiona cha myema kuni. Mfano mzuri ni yule mwandishi nguli wa Nigeria Wole Soyinka, Ben Saanane wa Tanzania, nk.
Mkuu sasa tufanyeje kama taifa ?
 
Mleta mada hoja yako ni ya msingi sana.

Ukweli ni kwamba wenye akili wako, tena wengi tu. Tatizo ni taasisi iliyojimilikisha nchi inayoitwa CCM.

Kwa mujibu wa katiba yetu mbovu ni kwamba ili uweze kusimama kwenye ulingo wa siasa na kutoa kile unachoamini ni lazima uwe na kivuli cha chama cha siasa.

Ccm imetumia katiba mbovu tuliyonayo kuvidumaza kabisa vyama pinzani vya kisiasa.

Sasa, ili mwananchi msomi nguli mwenye nia ya dhati kabisa ya kuleta mapinduzi ya kifikra na kisiasa katika nchi hii aingie kwenye huo ulingo, mlango pekee ulio wazi ni kupitia CCM.

Ndani ya CCM, kabla hujatoa unalolijua kwa wananchi, ni lazima uiambie kwanza hii taasisi wakukubali au wakukatalie na kukupangia ya kuongea/kufanya.

Hapo inakuwa aliyesoma na asiyesoma wote wanakuwa wamoja ndani ya CCM.
Ndio hapo inakuja hoja yako, wasomi hawapo nchi hii?

Jambo la kufanya hapa ni wananchi wote waliojitambua kupiga kelele kudai katiba mpya.
Ebu fafanua jinsi tutakavyoitumia iyo katiba mpya kufanya watu wenye akili wanatusaidia kutatua changamoto za jamii
 
Back
Top Bottom