Kwani lazima...................?????

sakapal

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
1,804
Reaction score
1,425
Habari zenu wana MMU, poleni na shuhuli za kutafuta shekeli.

Nimejiuliza hili swali baada ya kukutana na accusation flani hivi, naomba wadau mnisaidie nyie mnachukuliaje au mnaonaje
(iko kwenye mfumo wa mfano)
Mr. Y anakaa Mwanza na amepata safari ya kikazi kwenda Tanga, kule kapangiwa hoteli na ofisi na ameleipiwa full menu yaani breakfast lunch na dinner hapohapo hotelini, usafiri upo wa kumtoa hotelini kwenda kwenye semina na bado ana per diem kapewa na ofisi. Huko Tanga anakaa kwa mwezi mmoja baada ya wiki mbili akiwa hotelini na ubusy wa semina na kuchoka anajikuta hajatembea out ya hotel na sehemu ya semina, wakati huohuo mkoani hapo anamarafiki ambao walisoma wote chuo na baadhi ya ndugu wa mbali yaani wale wa kuvuta kwa mamati hata ukiwa unamtambulisha mtu unakuwa na mabano kama matatu hivi, mfano huyu ni mdogo wake na mtoto wa shangazi yake binamu yangu-- yaani binamu yangu anashangazi yake (ambae sio shangazi yangu) sasa huyo shangazi anamtoto ambaye ni binamu wa huyu binamu yangu mimi na huyo binamu anamdogo wake ndo kusema -- sasa Mr. Y anakutana na huyo mdogo wake na mtoto wa shangazi yake binamu yangu(ambaye tuseme anaitwa K, huyo K baada ya kusalimiana na Mr. Y na kujua kuwa yuko hotelini kwa muda wa wiki mbili anamlaumu mbaya na kuanza kumwambia binamu yangu kuwa Mr. Y anajisikia yaani kaja huku Tanga hataki hata kuja kutusalimia na anakaa hoteli wakati kwetu kupo tungempa chumba tu akae anatumia hela vibaya, anajidai anaringa hata kuja kutusalimia basi au kusema kuwa niko Tanga hajatuambia na malalamiko kibao kwa binamu yake Mr. Y.
Hivi hii ni sawa kuwa ukienda mkoa flani lazima uwatafute watu wote wanaokaa mkoa huo unaowajua? na je usipowaambia au kuwatafuta ni kosa?
Karibu unipe mtazamo wako
 
Sio lazima kuwatafuta na sio kosa kama usipowapa taarifa ya ujio au hata kuwasaka baada ya ujio.
 
Ukitaka kujua nani ndugu nani si ndugu subiri Msiba ukukute! Wale unaowaona mpo close watakucha mdomo wazi!
 
Mie huwa siwatafuti kabisaaaa, kisa cha kuharibu ratiba za watu?? hivi mfano imetokea umefanya kazi mpaka usiku wa manane utaweza kweli kugonga nyumbani kwa mtu mida hiyo?? na vile nimekwenda kufanya kazi na sio kutafuta ndugu basi sioni ulazima wa kuwatafuta. Labda niwe nimeagizwa kuwapelekea kitu kinachowahusu.
 
Mr. Y anawajua vizuri sana ndugu zake ndiyo maana hajalalamika.
Na huenda hakupenda kwenda kwao kwa kuwa wanapenda kupiga mzinga.
 
Sio lazima,tunapunguza mawazo ya ujima.Maisha yenyewe haya Kama unaweza okoa bajeti za wenzio
+
 
Ukitaka kujua nani ndugu nani si ndugu subiri Msiba ukukute! Wale unaowaona mpo close watakucha mdomo wazi!

au ufulie then uwalilie shida... Hapo ndipo utamjua nduguyo ni nani.
 
Ni gharama kubwa kuishi kwa mtu ambae kwa namna moja ama nyingine hata kabla hujapata ajira au utotoni mlikuwa hampo karibu ukichanganya na huyo ndugu yako awe hajawahi fanya kazi hizi za kuajiriwa maana siku ukiwa huna hamu ya chakula atakuambia unaringa wakati wewe umeshiba chakula cha workshop
 
Kuwaambia kuwa upo mkoani kwao sio lazima ila ni Uungwana tu. Na kwenda kufikia kwa ndugu,wakati upo kikazi mkoani,hii itategemea jinsi ulivyo na hao ndugu zake na we mwenyewe life styke yako. Wengine tunapenda kuwa huru tukiwa ugenini,ukikaa kwa ndugu inabidi ufate taratibu za pale. Ishu kama kula,muda wa kulala na kuamka,wageni wako binafsi ukikaa hoteli unakuwa huru zaidi. Then kama unamudu gharama kwanin ukakae kwa ndugu,utawatembelea tu jioni siku ukipata nafasi.
 
Kama ni ndugu wa karibu na nafasi ipo siyo vibaya kuwatembelea ila kuishi nao hata kama ni familia ya kaka au mdogo mzaliwa nae siyo ustaarabu na pia unaharibu utaratibu wa kawaida wa familia.
 
Nivizur ukawasms tu kwamba nipo hapa, yanaweza kukupata makubwa ukashindwa hata pakuanzia
 

Unawatafuta ili iwe nini? hao walikuwa wanataka kukupiga mizinga hawana chochote. Ila hako katabia kwenye familia zetu za kiswazi ziko sana. Watajifanya wema ukafikie kwao, baadae utasingiziwa mambo ambayo hayaeleweki. Mimi kama naenda sehemu kwa safari ya kikazi na nina mafungu (nimewezeshwa) huwa sitaki kufikia kwa mtu. Nitaenda kwao kuwasalimia tu na tena nikiwa na muda. Period!
 
watembelee ndugu zakoban! sio ulaya hapo afrika bado ni extended family.jamii haitakuelewa na haipendezi machoni kwa watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…