Kwame Nkrumah, Patrice Lumumba, Bob Marley, Muammar Ghadaffi, viongozi waliouawa baada ya kusisitiza kuungana kwa Afrika

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
KWAME NKRUMAH,PATRICE LUMUMBA,BOB MARLEY,MUAMMAR GHADAFFI, VIONGOZI WALIOUAWA BAADA YA KUSISITIZA KUUNGANA KWA AFRIKA.

Leo 20:30hrs 13/09/2020

Leo hii ndoto ya kuungana kwa Waafrika imepotea kwenye akili za Waafrika wengi,kila mwafrika hivi sasa anaganga njaa ilimradi siku ziende,Wapo Viongozi wachache mfano wa Muammar Ghadaffi wenye maono ya kuliunganisha bara la Afrika kwa kujenga imani kwa Waafrika ya kwamba tunaweza,Rais John Pombe Magufuli ni mmoja wa Marais wa sasa ambae mtazamo wako hautegemei Mchina,Mrusi wala Mzungu,huyu ni Kiongozi Shujaa ambae bado anabeba maono ya Viongozi wetu waliopata kuwa na ushawishi katika bara letu la Afrika waliosisitiza kuungana kwa Afrika.

Mbali na kwamba nchini Tanzania tuna changamoto za hapa na pale ila bado kuna ahueni, Mimi Mtanzania ambaye nimezoea kuamka asubuhi nikaenda kuuza dagaa wangu au nikaendesha bajaji yangu au nikauza magunia yangu ya mahindi na mpunga,nikatoka jioni nikapitia kijiweni nikapata story mbili tatu nikarudi nyumbani,nikakusanyika na kupiga story na familia yangu tukala tukashiba,tukalala bila bughudha,Sasa mimi uniunganishe na msomalia, mnaijeria mkongo, muethiopia, mrundi, na mlibya.

Wengi wa watu kama wa afrika ya kati ambao wengi kukicha hawajui kama giza litaingia akiwa salama, akitoka nje hajui kama atarejea ndani tena, kwakweli jaribu kuwatafakari viongozi kama Rais Museveni wa Uganda,jaribu kuwatafakari viongozi kama Rais Ciril Ramaphosa wa Afrika ya Kusini,jaribu kuzitafakari nchi za Somalia,Sudan,Eritrea,Mali,Gabon,Guinea na Nigeria,jaribu kuzitafakari nchi za kiarabu zilizojipata kwenye ramani ya Afrika Magharibi,nchi ya Algeria,Morocco,Libya na Misri,unaweza kupata jibu ya kwamba kwa upande wa Afrika kuungana ni kuleta dhahama tupu kwa Waafrika tulio wengi, wacha tubaki hivyo tu labda vizazi vijavyo kama vitakuwa vimejitambua itafaa sana ila si kwa kizazi hiki cha leo.

Kwame Nkrumah aliuwawa kupitia mpango wa Wazungu kwa sababu ya kuwa na hoja endelevu ya kuliunganisha bara la Afrika. Alipofika wakati mwaka 1963 baada ya kuunda OAU akataka umoja huo iwe ni serikali ya nchi zote za Afrika,Hii iliichukiza Marekani kiasi kwamba maslahi yake ya kiuchumi yalitishiwa sana, hivyo wakaona kuwa ni heri mtu mmoja auawe ili taifa la Marekani linufaike,Muammar Ghadaffi alijaribu na angeweza ila hao hao walibya wakaamua kumtosa kwa kuwaambia watu wa magharibi wambamize, lakini lengo la Gadafi lilikuwa ni kuitaka Afrika iungane iwe Nchi moja,mpango wa Wazungu ukaingilia kati, kwani alitaka tuwe na bank ya kwetu Afrika, IMF ya kwetu ambapo nchi za Afrika zingekopa bila riba, satellite la Africa tusitegemee masatelite ya magharibi, ikabidi wazungu wamuue maana aligusa maslahi yao.

Ukiliangalia bara la Afrika kwa sasa utaona,masikini wasio na nguvu ya technolojia,waafrika wenye elimu duni,Waafrika wenye imani za kichawi na kishirikina ili waweze kusurvive katika maisha ya leo,utawaona waafrika wenye kukumbatia ukabila na udini, rushwa na majanga mengine lukuki ni hatari zaidi wakiungana kwa influence ya kisiasa mpaka kufikia stage ya kuaminiana kwa dhati kuwa wako pamoja,kipindi cha mpito,transition stage ni kipindi kigumu mno.

Unajua kutoka Misri kwenda Israel kwa miguu ni mwendo wa siku tatu au nne kwa mguu,lakini wana wa Israel walitumia miaka arobaini kutembea kutoka Misri kuingia nchi ya ahadi (kwa mujibu wa Bible), unaweza kujiuliza lengo hasa lilikiwa ni nini, lakini ukichunguza ni kuwa kizazi kilichotoka Misri hakikupaswa kuingia Kaanani nchi ya maziwa na asali kwani bado kilikuwa na mentality za Faraoh vichwani mwao,kwa hiyo akili zao zilikuwa bado zipo kwenye kutawaliwa na farao na mwisho wa siku kupewa wali nyama, so kile kizazi kilibidi kife kipotelee jangwani na kizazi kipya kisichoshuhudia ya Misri wala kumjua farao ndio kiingie kaanani.

Utakubaliana nami hivi sasa,sisi bado hatujatoka kwenye utumwa wa kiakili wa wakoloni wetu ndio maana hivi leo Tundu Lissu atanyanyaswa Tanzania ataenda kusema Marekani,Uingereza,Ujerumani na Ubelgiji,ni dhahiri baadhi yetu sisi Waafrika tupo bize kurudi kwenye Ukoloni, ndio kwanza tunazidi kugawanyika,ni sahihi nikisema akili ya kuunganisha Africa bila Vita haipo, Block la East Africa lijiimarishe kijeshi livamie block la Central Africa, then East na Central livamie Horn of Africa hivyo hivyo mpaka Africa iungane.

Kifalsafa hakuna Muungano wa Afrika unaoweza kutokea kwa hiyari, ni Vita Pekee ndiyo inayoweza kuiunganisha Africa,Issue iko hapa, Watanzania na wakameroun tupo tofauti sana, lakini Watanzania, Kenya, Uganda, Rwanda tusema Afrika ya Mashariki tunaingiliana kwa hiyo ni rahisi kujiunga,kwa namna hiyo hiyo Cameroun, Nigeria, Togo, Ghana nao wanafanana,halafu tunakuja DRC,Congo Brazavile, Gabon, Afrika ya kati nao wanafanana,halafu Sudan, Ethiopia, Djibout, Eritrea, Somalia sasa hizo blocks ziforce kuungana, nchi isiyotaka inavamiwa kijeshi na inaingizwa kwenye muungano kwa lazima.

Pengine Kwame Nkrumah alikuwa sahihi aliposema "Afrika should unite now or perish"lakini alternative yake ipo kwenye falsafa ya Mwalimu Julius Nyerere,aliposema tuanze kuungana taratibu,na hiki tunakiona hivi sasa kuna jumuiya kadhaa za umoja hapa Afrika tukiaanza na hii ya Afrika Mashariki, Kusini (SADC), Magharibi (ECOWAS),Kwa maoni yangu utofauti wa kijamii uliopo sio tatizo hata kidogo kwa mfano hapa nyumbani kuna jamii nyingi tofauti lakini tunaishi kwa amani kabisa.

Msumbiji nako jamii nyingi tofauti lakini wanaishi kwa amani kabisa japo sasa kuna kuingiliwa na magaidi wenye maslahi kwa Mabwana zao Urusi na Marekani, Afrika ya kusini kuna jamii nyingi lakini sijawahi kusikia ukabila ila Ukaburu ndio ulitikisa,tatizo kubwa ni awa wakora wa kimagharibi na baadhi ya Waafrika wenzetu kukubali kutumika na mataifa makubwa kwa maslahi ya mataifa hayo, na mara nyingi viongozi wenye nia nzuri na maslahi ya Afrika huwa hawadumu kwa mfano Thomas Sankara na Patrice Lumumba.

Katika Afrika hii hii kwa sasa kuna nchi zina mafuta, zina gesi na madini mbalimbali,Mataifa kadhaa ya kiafrika yatasema tayari yanajitosheleza na hawahitaji tena kuungana na mtu yeyote,kwa tafakuri ya haraka,hakutakuwa na maelewano ya dhati ya resource allocation and distribution,tuangali nchi ya DRC Kongo na Sudan ya kusini ni shida sana,Kwa sasa kisiasa kila nchi ina vision tofauti kabisa, kiuchumi masuala ya resource allocations, kiutamaduni labda kidogo tunafanana fanana ingawa kuna mataifa mengine ya afrika yana mila na desturi ngumu sana sana kuziishi.

Nchi yenye utamaduni unaweza kuchukuliwa na yeyote ni Tanzania,Tanzania ni Bonge la nchi,nililijua hili nilivyopata kuishi Kenya ambapo kwa raia mgeni utaishi kama kunguru,Ukitaka kuamini nawe tembea nchi mbalimbali za Afrika utakubaliana nami,Big up kwa Baba wa Taifa letu, Julius Kambarage Nyerere,Big up kwa Baba wa Taifa la Ghana,Kwame Nkrumah,Wazo la Julius Nyerere tunaendelea nalo hata sasa,japo wazo la Kwame Nkrumah lilikufa baada ya kila taifa kupata Uhuru na kuogopa kutoa Uhuru wake kuungana na Nchi nyingine kuunda Afrika moja,wazo la Kwame Nkrumah lilikuwa zuri hata Julius Nyerere mwenyewe alikiri,akiwa Ghana na hata kwenye makala zake,kwamba Wazo la Kwame Nkrumah japo lilikuwa na changamoto nyingi lakini lilifaa zaidi.

-Mapato yapatikanayo Afrika.

Nchi za Kiafrika zilipata $ 162bn mwaka 2015, hasa katika mikopo, misaada na utoaji wa kibinafsi. Lakini mwaka huo huo, dola 203bn zilichukuliwa kutoka bara, ama moja kwa moja kwa njia ya mataifa mengine kurudia faida na kuhamisha fedha kinyume cha sheria kwenye sehemu za kodi, au kwa gharama zilizowekwa na wengine duniani kwa njia ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kupunguza.

Hii imesababisha upungufu wa kifedha wa $ 41.3bn kutoka nchi 47 za Afrika ambapo watu wengi hubakia katika umasikini, kulingana na Ripoti hiyo, Hesabu ya Uaminifu 2017,Wahamiaji walisema kuwa mtiririko wa kifedha halali, unaoelezewa kama harakati haramu ya fedha kati ya nchi, akaunti ya dola 68bn kwa mwaka, mara tatu zaidi ya $ 19bn Afrika inapokea kwa msaada.

Tukiangazia kwenye hili,kwanza kabisa,Afrika ni moja,Afrika is one,tunachokosa Africa ni Common interest,Common purpose,na Common identiy.Tungeanza na free movement na free trade labda tungechangamana vizuri na hii ndoto ya Afrika moja,ingefikiwa upesi,kuiunganisha Afrika sharti namba moja kuunga Uchumi wa Afrika, jambo ambalo likikua lifanywe na Gadaffi wa Libya , kipaumbele chake kilikua ni kutengeneza pesa Moja ya africa yenye nguvu zaidi,kama ilivyokuwa kwa dola,Euro na Pound.

Pia Regional Economic integration in kitu kizuri zaidi sababu data zinaonesha kwamba Bara la Afrika linafanya biashara kwa asilimia ndogo sana baina ya nchi ya kiafrika na nchi yenzake ya kiafrika inakadiliwa kama 15% uki compare na Europe kama 70% kwa hiyo Economic integration ni muhimu kuliko kuungana kwa mtindo wa Political intergration,

-Je Tukiungana ndo kukatakuwa na matatizo makubwa!?

Tuangazie Changamoto chache ambazo zinaweza kutokea,
1.Uhamiaji
Kutakuwa na Movements za watu within the continent,Watatatoka sehemu amabazo ni masikini kwenda kwenye zile nchi tajiri za kiafrika mfano watu wengi watakimbilia nchi kama South Africa,Egypt, Morocco,Nakuacha nchi zao zilizo Masikini,sasa Nani atapaswa kuziendeleza nchi Masikini zilizokimbiwa!?

2.Warabu hawatapenda Muungano japokuwa tunaishi na waarabu katika bara moja continent moja nazungumzia Algeria,Morroco,Misri hawatapenda kutambulishwa kama Wafrika wanapenda kujiita warabu au kuji identify. Na watu Middle East,Na nchi nyingine za Kuarabu,

3.Ukabila
Kuna nchi nyingi zina tatizo la ukabila sasa chukulia kama tukiungana itakuwaje watu watapenda kumchagua kiongozi wao kutoka kabila lao na sio vingine,

4.Nchi za Magharibi azitafurahi hata kidogo kutokana na huu kwa sababu Muungano huu utaa threaten interest zao wanaweza kufanya kama walivyofanyia Soviet Union,tukifika hapa kwa mtazamo yangu mimi sioni haja kuungana kabisa na tusije kujaribu kufanya hivyo,kutakuwa na matatizo makubwa,kitu ambacho tunaweza kufanya labda Economic integration kama EAC,SADC na ECOWAS.. kuungana labda Sub-Sahara kwanza na Sio na North Africans wanatuzarahu sana.

Nimalizie kwa kusema bado sijashindwa na ndoto ya Afrika kuungana bado ipo,tuanze na Jukwaa moja la Afrika nzima,yaani hiyo platform ijumuishe waafrika kutoka sehemu mbalimbali za mataifa ya Afrika,Linakuwa na Muundo wa kitu kama serikali,tayari tuna AU,model ya USA imetufaa,kuwe na Rais, Mawaziri na Ma gavana wa Majimbo mbalimbali kama Tanzania, Kenya, Nigeria,kwa urahisi zaidi, hilo taifa liundwe na Sub Sahara countries..Au Nchi za Waafrika weusi tu, Waarabu tuwaache kwanza,

Kisha kunakua na Mijadala mbalimbali. Mean while, inaundwa taasisi ya Kimataifa ya kupromote Good Governance and Development of Afrika,ambayo yenyewe itakua na Mission ya kuhakikisha tunashawishi Afrika iwe kitu kimoja,Yenyewe itakua Legal Entity ambayo itakua inachukua agenda na maoni mbalimbali yanayotolewa online kuyatekeleza offline,tuisapoti sana taasisi hiyo kiasi kwamba inapata heshma na kuwa na ushawishi sana,watendaji wake wanakua smart na watu wenye ushawishi,ambao pia wanapaswa kuwa true Pan Africanist kama mimi Msemakweli Chakubanga ambae najulikana pia kama Leslie Mbena,pengine kizazi cha Marcus Mbena kitakuja kuwezana na Muungano huu,nimetabiri tu,

The Pan-African Congress — following on from the first Pan-African Conference of 1900 in London — was a series of seven meetings, held in 1919 in Paris (1st Pan-African Congress), 1921 in London (2nd Pan-African Congress), 1923 in London (3rd Pan-African Congress), 1927 New York City(4th Pan-African Congress), 1945 Manchester (5th Pan-African Congress), 1974 Dar es Salaam (6th Pan-African Congress),[1] 1994 Kampala (7th Pan-African Congress),[2][3] and 2014 Accra[4][5] that were intended to address the issues facing Africa as a result of European colonization of most of the continent.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master's in Leadership and Management.

-Research; Assessing Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Hiyo stashahada ya pili sijui umeipataje,
Kwame nkurumah huyo unayemsema mwaka 1964 alitamka mwenyewe kuwa anataka kuwa rais milele na taifa la chama kimoja " president for life".
Aliyetaka Afrika iungane ili awe rais sio yeye Kwame,? Hakuna kiongozi ambae angetaka Afrika iungane bila kujiangalia maslahi yake binafsi.

Ebu fanyeni kazi nyingine hizi habari za kuleta mabandiko marefu ndani yenye ujinga muache, Viongozi hao unawasema wangeibadili Afrika kwa mitazamo yao si kweli, tofauti na Bob Marley ambaye hakuwa kiongozi wa kufanya mabadiliko alikuwa mtu maarufu mwenye maono juu ya Afrika lakini sio kufanya maamuzi.

Viongozi wa Afrika kwenye nchi nyingi wote walikuwa waroho wa madaraka na wenye ubinafsi wa kutumia mali chache zilizopatikana kuneemesha familia zao, hoja zao za kuungana ili wapate pakubwa pa kumega, kila aliyetaka Afrika iungane alitaka yeye ndio awe kiongozi wa hiyo Afrika, huoni huo ulikuwa na upuuzi.

Afrika hatuwezi kufika tunapofikiria kama wasomi wenyewe ndio nyie, mnaleta mabandiko yenye viingereza ndani ili tupate uvivu wa kusoma umeshindwa nini kuandika kwa kiswahili mwanzo mpaka mwisho au huko chuo mnaposomaga ndio mnaambiwa lazima muweke vizungu kwenye mabandiko yenu?
 
Hiyo stashahada ya pili sijui umeipataje,
Kwame nkurumah huyo unayemsema mwaka 1964 alitamka mwenyewe kuwa anataka kuwa rais milele na taifa la chama kimoja " president for life".
Aliyetaka Afrika iungane ili awe rais sio yeye Kwame,? Hakuna kiongozi ambae angetaka Afrika iungane bila kujiangalia maslahi yake binafsi.

Ebu fanyeni kazi nyingine hizi habari za kuleta mabandiko marefu ndani yenye ujinga muache, Viongozi hao unawasema wangeibadili Afrika kwa mitazamo yao si kweli, tofauti na Bob Marley ambaye hakuwa kiongozi wa kufanya mabadiliko alikuwa mtu maarufu mwenye maono juu ya Afrika lakini sio kufanya maamuzi.

Viongozi wa Afrika kwenye nchi nyingi wote walikuwa waroho wa madaraka na wenye ubinafsi wa kutumia mali chache zilizopatikana kuneemesha familia zao, hoja zao za kuungana ili wapate pakubwa pa kumega, kila aliyetaka Afrika iungane alitaka yeye ndio awe kiongozi wa hiyo Afrika, huoni huo ulikuwa na upuuzi.

Afrika hatuwezi kufika tunapofikiria kama wasomi wenyewe ndio nyie, mnaleta mabandiko yenye viingereza ndani ili tupate uvivu wa kusoma umeshindwa nini kuandika kwa kiswahili mwanzo mpaka mwisho au huko chuo mnaposomaga ndio mnaambiwa lazima muweke vizungu kwenye mabandiko yenu?
J.K Nyerere alitaka kuwepo muungano wa Tanzania na Kenya na yeye kumuachia ngazi ya urais Kenyatta.
 
J.K Nyerere alitaka kuwepo muungano wa Tanzania na Kenya na yeye kumuachia ngazi ya urais Kenyatta.
Kambarage Kambarage alikuwa mtu sana lakini katika kuandika kote wasomi wanaishia kusema alipenda ujamaa tu ambao wanasema ulifeli, kwenye mambo ya kuifanya Afrika kuwa moja hasemwi, leo huyu mtanganyika mwenzetu ameoma kina Gaddaf, Nkurumah na Bob Marley sio Nyerere.
 
Ni Mwalimu pekee ndiye alionesha nia ya dhani kuhusu kuungana ukilinganisha na wengine.

Na Mwalimu alitahadharisha kuwa kuacha kila Nchi kujitawala kwanza ndio uwaambie kuhusu Muungano ni ngumu, ndio maana alitaka kama inawezekana Uhuru wa Tanzania usubirie Kenya na Uganda ili tukishapata uhuru kwa pamoja iwe rahisi kuungana.

Na kama alivyoshauri na ndio ilivyo/inavyotokea, ni ngumu kuishauri Nchi ambayo tayari imeshajenga mfumo wa uongozi, nani anakubali ku share kupunguza au kuachia madaraka yake kwa sababu ya kuungana...wanaweza wachache lakini wakishakuwa wengi kazi inakuwa ngumu.

Na hata wazo la Nkhuruma Mwalimu alionya kuwa itakuwa ngumu ni bora waanzie kwa kanda(regions) kwanza na ikifanikiwa basi walau itakuwa rahisi kwenda mbele.

Sijui ni wangapi walimuelewa lakini kwa hali ilivyo mpaka sasa Mwalimu alikuwa na hoja.
 
Japo sijasoma uzi wote lkn bado Afrika nafasi tunayo ya kuujenga na kuimarisha umoja wetu . Wakati wa JPM nilipata kuamini kuwa laiti kama tungekuwa na Maraisi 10 hivi Afrika nzima wenye Hulka na Kariba ya Marehemu JPM Afrika tungevuka ng'ambo .
 
Kambarage Kambarage alikuwa mtu sana lakini katika kuandika kote wasomi wanaishia kusema alipenda ujamaa tu ambao wanasema ulifeli, kwenye mambo ya kuifanya Afrika kuwa moja hasemwi, leo huyu mtanganyika mwenzetu ameoma kina Gaddaf, Nkurumah na Bob Marley sio Nyerere.
Ni kweli kabisa mkuu, wabongo tunaonaga historia za watu zilizoandikwa kwa kingereza au zilizokuwa portrayed na hollywood kama ndo za maana sana kuliko za kwetu hapa.
 
Back
Top Bottom