majikupwa
Senior Member
- Jan 26, 2014
- 178
- 36
Kwanza kabsa nachukua fursa hii kukusalimu,
Mh pole sana kwa majukumu makubwa ulionayo ya kulijenga taifa hili ambalo lina rasilimali nyingi lakini tumeshindwa kuzitumia ili kulinasua taifa letu katika umasikini.
Pia mh nakupa pole kwa jinsi UKAWA wanavyokuumiza kichwa chako ila najua wewe hukupenda mfikie hapo mlipofikishwa na UKAWA bali ni chama chako chenye mtazamo hasi ndio maana kinasababisha uumie kichwa
mh pia najua ya kwamba upo kwenye mchakato mkubwa wa bunge la bajeti ila naamini ujumbe huu utasogezewa na jirani yako hapo bungeni hivyo naamini utausoma tu.
Mh waziri mkuu napenda kukujulisha kilichonisukuma kukuandikia ujumbe huu ambao unatutesa sisi wananchi wa Kusini mwa Tanzania.
Mh waziri mkuu ulipokuja kusuruhisha mgogoro baina ya sisi wananchi wa Mtwara na serikali kuhusu gesi uliahidi kwamba ujenzi wa barabara ya kutoka Dar es salaam kwenda Kusini itakamilika mwezi Disemba 2013 lakini mh mpaka leo hakuna kinachoendelea zaidi ya kutudanganya na makatapila barabarani .
Mh waziri mkuu kama serikali yako unayoisimamia imeshindwa kujenga sisi wananchi wa Mtwara tupo tayari kuingia barabarani tuijenge wenyewe.
Kuhusu ujenzi wa barabara pia namuona mbunge wetu mh Muriji amekaa kimya au kwakuwa magari yake ndo mengi huku kusini? Au amekaa kimya ili aendelee kuona wananchi wa Mtwara tunalipa nauli kubwa kwenye mabasi yake?
Pia mh waziri mkuu uliahidi ajira katika kiwanda cha Dangote ila mpaka leo ajira zinatolewa kiukoo na kiujirani, je sisi ambao hatujulikani kwenye koo hizo tutaenda wapi?
Mh wazir mkuu ninaomba utoe tamko ni lini mambo haya utayafanyia kazi mapema maana sisi vijana wa Mtwara hatutaki ahadi za kichina au feki,uamuzi tunaofikia sasa ni kuhamishia kiwanda hicho maeneo za kuzimu.
Ni matumaini yangu ujumbe huu utaupata kama usipoupata nafahamu kamanda Lema atakufikishia.
Ahsante na ubarikiwe.