Kwanza nikupe pole kwa majukumu ya kila siku, pili nikupongeze kwa yale uliyoweza kuyafanya katika utawala wako na kwa yale uliyoshindwa ujitathmini na kuchukua hatua. Binafsi sijawahi kuleta maoni yangu ya aina yoyote kwako hivyo kupitia mtandao huu najua utaletewa taarifa.
Mimi ni mdau mkubwa sana wa elimu. Nina furaha jinsi ambavyo nchi hii ilikuwa karibu ya mwisho kwa kuwa na idadi ndogo ya vyuo vikuu Afrika mashariki lakini leo hii Tanzania inaongoza kwa kuwa na idadi ya zaidi ya vyuo vikuu 28, zaidi ya vyuo vikuu vishiriki 19, na 'centers' za vyuo vikuu zaidi ya 14. Na pia vipo vyuo vingine vingi vinavyosimamiwa na nacte vinatoa elimu ya juu haya ni maendeleo.
Zipo nchi duniani zimwekeza katika huduma ya elimu. Kwa Tanzania pia tunaweza kuwekeza katika elimu na kujitangaza katika nchi za Afrika kupata wanafunzi kuja kusoma kwa kulipa ada kama ambavyo Uganda imekuwa na mafanikio kwa kupata wanafunzi wa nchi mbalimbali maana zimeanza kuonekana dalili kuwa baadhi ya vyuo vinakosa wanafunzi kwa sababu idadi ya wanafunzi wa ndani ni ndogo.
Kwa kuangalia mbele na idadi ya wanafunzi inavyoongezeka kutoka shule za kata bado tunahitaji idadi kubwa ya wasomi wa vyuo vikuu na vyuo vya kati/ufundi.
Napendekeza Muheshimiwa Raisi agiza wakuu wote wa mikoa kutenga maeneo kwa ajili ya vyuo vikuu vya serikali angalau kila mkoa uwe na chuo kikuu chake. Zitengenezwe kamati za wananchi kusimamia uchangiaji kwa kushirikiana na serikali na pia wapewe uwezo na mamlaka ya kushirikiana na vyuo vikuu vya nje kusimamia na kuendeleza taasisi.
Au la vialikwe vyuo vikubwa duniani wapewe maeneo kwa ajili ya kujenga vyuo hapa Tanzania. Baada ya miaka kumi hadi 20 Tanzania itakuwa ni education hub ya Afrika na wananchi tutakukumbuka kwa hili pia.
[/COLOR]
Itakuwa education hub ya Africa wakati sehemu kubwa ya wanaosoma wanatoka nje.!!! inaonekana mwenzetu hulioni wimbi la wanafunzi wengi hasa katika shule za kata kupata division 5 hao ndio watakao jaza hivyo vyuo ? wanafunzi wanao chaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wapo wengine hawajui kusoma wala kuandika majina yao. hawa watajaza vyuo hivyo hasa baada ya kumaliza elimu ya sekondari ? je! unajua kuwa zaidi ya nafasi 3000 za kujiunga na masomo ya kidato cha tano zilibaki wazi baada ya kukosa wanafunzi walio qualify ,pamoja na kuwa baadhi ya combinations wanafunzi walipelekwa na pass za DDC? mwanzo wa maoni yako nilifikiri una mshauri Raisi amalize mgogoro na walimu, kwa kuwalipa madeni na kupandisha madaraja yao ili waanze kufundisha kwa moyo mkunjufu na hatimaye kupunguza kama sio kumaliza wimbi la wanafunzi kupata division 5 .
Hata angemshauri tatizo la baadhi ya shule za msingi wanakaa chini,so anaporuka kwenda huko nnchi zenye miti ya kutosha awaombe msaada wa kutufadhili madawati maana huku kwetu ni jangwa.Tunaandaa sherehe kubwa kubwa wakati shule nyengine zina walimu wawili tu.Kwasababu mazingira ya kaz ya ualimu kijijin hayamtamanishi kijana kwenda.Kata zipo zipo tu upande wa sayansi zinasikitisha heri ungemshauri ziwe na maabara bora.Akiufanyia kazi ushauri wako mi sitakuwa tayari kuishi katika nnchi iliyo na wahitimu vilaza wa elimu ya juu ntabeba familia yangu tutaenda ishi uamishoni.Maana ntakataa kuish na maabunuwasi wanaofikir namna ya kuezeka paa,baada ya kufikir namna ya kujenga msingi.Tanzania inatakiwa kuboresha elimu ya msing na sekondari kwanza hususani kata then ndio tuende huko utakako mkuu

Mawazo yako ni kweli lakini ata aliyetoa maoni haja kosea ,kwani wakati hivyo vyuo vinakamilika elimu itakuwa imeboreshwa kwahiyo wanachuo watapatikana wazuri.Pili ingawa wengine wanabeza hizi shule wajue kuwa zina wabadilisha kiupeo watoto wengi jiulize kwanini siku hizi kupata dada wa kazi ni shida.Ujue vijana wakimaliza hata kama hajafaulu vizuri kunabsdiliko makubwa ameyapata hata vyuo itakuwa hivyo hivyo vijana wengi watapevuka kimawazo na kufanya shughuli zao vizuri zaidi kuliko kama wasinge pata elimu hiyo.
Lete ushauri wa kuboresha ngoma na sherehe bwana! Elimu wizara ipo, wazaramo na majirani zake hatuhusiki nayo
Huo ndio ukweli mchungu. Watanzania tuna tabia ya kudharau mambo yetu, shule za kata watu wanaziponda sana lakini kwa taarifa tu nyingi zimeanza kufanya vizuri kwenda sekondari zamani ilikuwa ni ndoto siku hizi ni jambo la kawaida. Hao hao wazaz na watu wanaolalamika sana lakini wao wenyewe hawafanyi jitahada zozote kuwasaidia vijana wao wasome kazi ni kulaumu serikali...
Je hivyo vyuo wataenda wahitimu wenye div. V?
Kuweka msingi mzuri kwenye jambo lolote elimu ikiwa mojawapo, ni muhimu sana.
Babu zetu walikuwa na elimu ya darasa la VIII lakini walikuwa na uwezo kiakili na maarifa kuliko asilimia kubwa ya kizazi chetu.
Go figure what's wrong with quality of education today.
Kwanza nikupe pole kwa majukumu ya kila siku, pili nikupongeze kwa yale uliyoweza kuyafanya katika utawala wako na kwa yale uliyoshindwa ujitathmini na kuchukua hatua. Binafsi sijawahi kuleta maoni yangu ya aina yoyote kwako hivyo kupitia mtandao huu najua utaletewa taarifa.
Mimi ni mdau mkubwa sana wa elimu. Nina furaha jinsi ambavyo nchi hii ilikuwa karibu ya mwisho kwa kuwa na idadi ndogo ya vyuo vikuu Afrika mashariki lakini leo hii Tanzania inaongoza kwa kuwa na idadi ya zaidi ya vyuo vikuu 28, zaidi ya vyuo vikuu vishiriki 19, na 'centers' za vyuo vikuu zaidi ya 14. Na pia vipo vyuo vingine vingi vinavyosimamiwa na nacte vinatoa elimu ya juu haya ni maendeleo.
Zipo nchi duniani zimwekeza katika huduma ya elimu. Kwa Tanzania pia tunaweza kuwekeza katika elimu na kujitangaza katika nchi za Afrika kupata wanafunzi kuja kusoma kwa kulipa ada kama ambavyo Uganda imekuwa na mafanikio kwa kupata wanafunzi wa nchi mbalimbali maana zimeanza kuonekana dalili kuwa baadhi ya vyuo vinakosa wanafunzi kwa sababu idadi ya wanafunzi wa ndani ni ndogo.
Kwa kuangalia mbele na idadi ya wanafunzi inavyoongezeka kutoka shule za kata bado tunahitaji idadi kubwa ya wasomi wa vyuo vikuu na vyuo vya kati/ufundi.
Napendekeza Muheshimiwa Raisi agiza wakuu wote wa mikoa kutenga maeneo kwa ajili ya vyuo vikuu vya serikali angalau kila mkoa uwe na chuo kikuu chake. Zitengenezwe kamati za wananchi kusimamia uchangiaji kwa kushirikiana na serikali na pia wapewe uwezo na mamlaka ya kushirikiana na vyuo vikuu vya nje kusimamia na kuendeleza taasisi.
Au la vialikwe vyuo vikubwa duniani wapewe maeneo kwa ajili ya kujenga vyuo hapa Tanzania. Baada ya miaka kumi hadi 20 Tanzania itakuwa ni education hub ya Afrika na wananchi tutakukumbuka kwa hili pia.
[/COLOR]Hayo yote yamefanyika, kila mkoa una maeneo ya vyuo vikuu, ni wewe tu kwenda kuomba eneo na kuanza kazi.
Vyuo vikuu vya nje vimeshaalikwa sana tu, na kuna vingine tayari vina matawi Tanzania ya vitengo aina moja ama nyingine na kila siku zinavyokwenda vinazidi kuongezeka.
Vyuo ni elimu lakini pia ni biashara mtoa mada ameona fursa ya Tanzania kuwa education hub Africa kinachotakiwa ni ku chukua fursa hiyo, watu huwa hawaelewi wanadharau div 4 na 5, wanaamini kuwa ni wajinga lakini kumbe hawa ni watu wakipata elimu hata ya ufundi au ya mambo mengine wanaweza kufanikiwa kuliko unavyo dhani nina mifano hai katika hili.
Serikali ya Majimbo hapa yaweza kuwa suluhisho!