Boutafrica
JF-Expert Member
- Dec 11, 2014
- 1,260
- 2,744
Anaandika:Khatib Imran Abu Khalil.
NARUDI MJINI.
KWAKO MZEE YUSSUF.
Kama ilivyo kawaida yangu kuyafanyia kazi agizo la Mtume saw la kunasiana. Basi namie nakunasihi kama Muislam mwenzako, juu ya maamuzi yako ya kurudi katika kueneza uchafu kwa kupitia muziki wa kishetani, kama ulivyoita urejea huo kurudi mjini. Makala hii itaangazia sehemu tatu.
1. Ulikotoka.
2. Ulipo.
3. Unapoelekea.
4. Hitimisho.
ULIKOTOKA.
Ulikotoka unakujua vyema wewe unakujua kuliko mimi na ndio maana uliamua kuacha muziki na kuja kulingania kheri. Lakini hata kwa Yale yaliyowatokea wenzako mliokuwa nao katika muziki huo ingelitosha kuwa ni ukumbusho wa kufanya usitamani tena kurudi kwenye muziki huo. Matukio yaliyotokea katika hiyo kazi ya mziki wa kishetani uliokuwa nao na mkichuana Sana katika kazi hiyo, lakini wametangulia mbele ya haki katika mazingira hata bila ya kupata muda wa kufanya toba. Na kazi zao zinaendelea kuhanikiza katoka kumbi za starehe.
Na mmoja katika hao ni Omar Kopa maana mpaka hatua za mwisho za maradhi yaliyopelekea kukatishwa kwa maisha yake akiwa yamemzidia nguvu Hana, lakini alikuwa akijikongoja kwenda kutumbuiza. Kiasi kwamba mauti yanamkuta wapenzi wake walihanikiza maziko kike kiume mguu kwa mguu mpaka fuoni malaloni. Haya matukio sio mgeni kwako Mzee Yusufu.
Na wengine ni wanamuziki wa bendi ya Five stars waliokufa katika ajali ya Gari mkoani morogoro wakitoka kutumbuiza na wakiharakia Kuja Kutumbuiza na waliokufa ni Issa Kijoti, Nasoro Madenge, Mapande, Fembe Juma, Omary Hashim, Tizo ,Omari Tall, Ngeleza Hasan, Hamisa Omari, Maimuna , Haji Msaniwa na mcheza show wa kundi la Kitu Tigo Ilala. Na wengine wengi.
Kwa matukio hayo na mengine nilidhani ndio yalikusukuma kuachana na mziki huo wa kishetani na kumrejea Allah na kufanya kazi ya ulinganizi wa Uislamu
Badala ya kuwa mlinganizi wa shetani kwa kutumia mziki huo. Ni wewe Huyo huyo ulikiri kuwa mziki wako ulisababisha majanga mengi katika jamii, ikiwemo ulevi, uzinifu ndoa za Watu kuvunjika.......
Ulipojiondosha kwenye muziki huo wa kishetani membari za kheri zilihanikiza kukupa hongera kwa moyo wa ujasiri Uliouonyesha na wakakuombea dua za kheri. Na walikukaribisha katika mimbari zao ukazungumza hivyo hivyo kwa mapenzi tu ijapokuwa huna maarifa hayo ya kufanya ulinganizi sahihi wa Uislamu. Kwani baada ya kuachana na muziki hukutumia muda wako kusoma Uislamu. Bali ilikuwa ni hamasa za kheri.
Ni takriban miaka minne toka mwaka 2016 niliposikia Habari ya wewe kutangaza kuacha muziki, ukikiri hilo katika nyumba ya Allah. Na baada ya miezi kadhaa iliyopita ni kaanza kusikia Habari za kuwa unarudi mjini. Na ulipoulizwa unarudi vipi mjini majibu yako haya kuwa wazi. Ila zaidi ya wiki Sasa ndio umefumbua fumbo hilo liliokuwa Lina wakanganya wengi wema kwa waovu. Wema Wakijua labda unakusudia kuimba nasheed na wehu Wakijua unarudi ili mwendelee kuivuruga jamii kwa kula Bata mpaka kuku waone wivu.
Kumbuka pia ulipata fursa ya kwenda hijja ikiwa ni kama ishara ya kutaka yote ya nyuma yafutwe na uanze upya. Umemlilia Allah kwenye mihadhara na hata kwenye kasida kutokana na yale uliyoyafanya. Lakini yote hayo umeyapuuza kwasababu ya starehe za muda mafupi za kidunia.
2. ULIPO.
Maamuzi ya wewe kurudi kwenye muziki mke wako ana ushawishi mkubwa Sana kwani Tunasema hivyo kutokana na sababu mbili kubwa.
1. Kutokana na kumuacha kwako kwenye muziki Hali ya kuwa wewe ulitoka kwenye muziki hiyo ilikuwa ni upenyo mkubwa ambao ibiliisi aliutumia kukurejesha kundini ukamfanyie kazi yake.
2. Ni kutokana na yale yaliyo nukuliwa katika vyombo vya Habari mke akisema mengi kuhusu masaiba ya kimaisha yanayokusibu baada ya wewe kuacha mziki. Ikiwemo kutapeliwa kibiashara kiasi nyumba yako kuwa hatarini kuchukuliwa na benki. Akionyesha kuwa maamuzi yako ya kuacha muziki yalikuwa sio sahihi. Hapa nipende kukumbusha kauli ya Allah.
(یَـٰۤأَیُّهَا ٱلَّذِینَ ءَامَنُوۤا۟ إِنَّ مِنۡ أَزۡوَ ٰجِكُمۡ وَأَوۡلَـٰدِكُمۡ عَدُوࣰّا لَّكُمۡ فَٱحۡذَرُوهُمۡۚ وَإِن تَعۡفُوا۟ وَتَصۡفَحُوا۟ وَتَغۡفِرُوا۟ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورࣱ رَّحِیمٌ)
[Surat At-Taghabun 14]
"Enyi mlioamini
Nimependa hakika miongoni mwa wake zenu na watoto wenu ni adui zenu tahadharini nao........"
Ama kuhusu na changamoto za maisha ndio zimekurejesha katika ulinganizi mbaya wa ibiliisi, na kuacha ulinganizi wa kheri. Ndugu yangu nikukumbushe kitu hakuna ambaye anaweza kukimbia mitihani ya Allah na kutahiniwa ni lazima na wala kurudi huko huwezi kukimbia hilo, Bali ni kubadilika Aina ya mitani. Na kitendo cha kurudi kwenye ulinganizi wa Haki mitihani ilikuwa ni lazima ili Allah aupime ukweli wako. Kama afanyavyo kwa waja wengi. Labda nikukumbushe hilo ndani ya Qur'an.
(أَحَسِبَ ٱلنَّاسُ أَن یُتۡرَكُوۤا۟ أَن یَقُولُوۤا۟ ءَامَنَّا وَهُمۡ لَا یُفۡتَنُونَ وَلَقَدۡ فَتَنَّا ٱلَّذِینَ مِن قَبۡلِهِمۡۖ فَلَیَعۡلَمَنَّ ٱللَّهُ ٱلَّذِینَ صَدَقُوا۟ وَلَیَعۡلَمَنَّ ٱلۡكَـٰذِبِینَ)
[Surat Al-Ankabut 2 - 3]
"Hivi wa nadhani watu kuwa wataachwa tu wasipewe mitihani hakika walipewa mitihani wale waliopita kabla yao ili Allah awafahamu wa kweli na awafahamu waongo"
Na huenda Allah alikupa mtihani katika mali hiyo ambayo huenda ilikuwa na uharamu mwingi ndani yake ili akupe mali ya halali na yenye kheri kwako lakini umeshindwa mtihani.
Kwa hayo maamuzi ya kurejea unajenga sura mbaya juu ya Uislamu na Jamii kwa ujumla. Na sura hiyo iko hivi.
1. Unaonyesha kulingania Uislamu ni udhalili na anaekamatana na ulinganizi huo ni mtu dhalili na kila anaejikita katika Uislamu basi ni dhalili. Hii inawezekana ni kutokana na wale waliokupokea katika ulinganizi wa Uislamu kwa kukuonyesha kuwa Uislamu unamlipa mlinganizi, tofauti na usahihi kuwa mlinganizi anapaswa aifanye daawah kama faradhi nyingine kama swala, funga..... Sasa ukiswali ili ulipwe fedha ni uwendawazimu. Bado tunarudi pale pale kuwa anaeingia katika kufanya ulinganizi wa kiislam akitarajia Uislamu utamlipa ni moja katika matatu imma awe tapeli kupitia ulinganizi huo, kama walivyo baadhi ya walinganizi, kiasi cha kufikia kuona kufanya utapeli katika njia ya daawah ni halali au atatumika dhidi ya waislamu wenzake kwa Ajili ya maslahi au utamshinda. Uislamu unatumikiwa kwa mali na nafsi.
2. Unawashajihisha vijana wenye sauti ya kuimba wajiingize kwenye muziki na kuachana na harakati za dini kwa kuona kuwa muziki unalipa na harakati hizo na majanga matupu.
3. Kwa tukio kama hili inawezekana kabisa wenye chuki na Uislamu wakalitumia kutukana Uislamu na kuwakashifu walinganizi wa Uislamu, kuwa ni Dini yenye dhiki ndio maana ulinganizi wake umekushinda.
UNAKOELEKEA.
Unakokoelekea ni kule ambako ulitoka. Maana umekula matapishi yako. Ndugu yangu Mzee kukupa nasaha hizi haina maana sisi hatukosei laa hasha Hakuna ambaye hana makosa, hasa maisha ndani ya mfumo wa kishetani wa demokrasia na ubepari wake. Mfumo ambao unaamrisha uovu na kupinga wema. Bali Kuna makosa ya mja na Mola hayo kila mtu anafanya imma ni makubwa au madogo. Lakini Kuna kufanya makosa na kuna kufanya ulinganizi wa Watu kufanya makosa. Kama wafanyavyo wanasiasa wa demokrasia na wanamuziki. Kurudi kwako kwenye muziki ni muendelezo wa ulinganizi wa Watu kufanya kila Aina ya maasi, kulewa, kuzini, kutukana...... Kama ulovyowahi kukiri hapo kabla.
Mbaya zaidi katika ulimwengu wa leo wa teknolojia yote hayo yemesajiliwa kwenye simu, kwenye mitandao..... Kila uchao yanaendelea kuipotoa jamii. Na itabakia hivyo hata baada ya kufa kwako. Je mzigo huo unaweza kuubeba?
Umekuwa na ujasiri wa kiasi wa kumsaidia ibilisi kazi hiyo ya kuamrisha machafu na maovu, tena ukianza na siku tukufu ya Eid, hebu nikukumbushe kwa kauli ya Allah anasema.
(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ وَمَنْ يَتَّبِعْ خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ فَإِنَّهُ يَأْمُرُ بِالْفَحْشَاءِ وَالْمُنْكَرِ ۚ وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ مَا زَكَىٰ مِنْكُمْ مِنْ أَحَدٍ أَبَدًا وَلَٰكِنَّ اللَّهَ يُزَكِّي مَنْ يَشَاءُ ۗ وَاللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ)
[Surat An-Nur 21]
"Enyi mlioamini msifuate nayo za shetani na mwenye kufuata nyayo za shetani Hakika anamrisha uchafu na uovu. Na laiti kama sio Fadhila za Allah na rehema zake asingeliokoka yoyote Katika nyinyi milele. Lakini anamtakasa anaetaka utakaso na Allah ni msikivu mjuzi.
Nasaha hizi pamoja na kuzielekeza moja kwa moja kwako ndugu yangu Mzee Yusufu, pia zinawahusu vijana, wazee na wakina mama waislamu waliopo kwenye muziki huo wa kishetani. Kama wakina Khadija Kopa, A'isha Mashaizu, Zuchu, Nasibu Abdul maarufu Daimond na Genge lake, Alikiba na Genge, Rajabu Abdul maarufu Harmonize na Genge, na wengine wengi ndugu zanguni haya maisha ni matamu sana lakini ni mafupi sana na tuendako ni kwa milele. Ni bora ukarejea kwa Allah mapema. Wako wengi waliokuwa huko lakini wakaacha kwa khofu ya Allah jifunzeni kwa wakina Ismail (Suma Lee). Na wengine wengi huko duniani kama Nepolion, Loon ambaye kwasasa anaitwa Amir Junaid Muhaddith Nepolion na wengine wengi ambao kwasasa wanafanya ulinganizi wa Uislam.
Nimeamua kuandika kwakuwa siwezi kuonana na wewe na wenzako kwa namna moja au nyingine. Lakini kwakuwa unayafanya hadharani basi ngoja tutoe nasaha hizi hadharani kama nilivyo wanaishi wenzako tena nikikufanya kama mfano wa kuigwa. na Imani zitakufika kwani unawafuasi wengi sana kwasasa.
Najua hata kama zitakufikeni nasaha hizi ni ngumu sana kunielewa maana huo ushakuwa ni ulevi kwenu na ulevi wa aina yoyote ule unataka maamuzi magumu kuuacha. Na kwakuwa mnaaimani ya kuwa Kuna malipo baada ya kufa basi hamna budi kufanya maamuzi magumu Kurejea kwa Muumba wako kabla ya kuondokewa uhai wenu. Fahamu kuwa kila madhambi yatendwayo Katika matamasha, majumbani na mijumuiko mbalimbali mnayoikusanya nanyi au muziki kutumika kuwakusanya au kuyafanya machafu mbalimbali na nyie mnafungu lenu. Allah anasema.
(لِيَحْمِلُوا أَوْزَارَهُمْ كَامِلَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۙ وَمِنْ أَوْزَارِ الَّذِينَ يُضِلُّونَهُمْ بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ أَلَا سَاءَ مَا يَزِرُونَ)
[Surat An-Nahl 25]
"Watabeba mizigo yao kwa ukamilifu na mizigo ya wale wanaowapoteza pasina na elimu ni ubaya ulioje kwa wanayoyabeba"
Hivyo basi kuwa makini sana ndugu yangu katika. Watasema mengi watakaosoma nasaha hizi wapo watakaotukana hasa wale wanaokupenda kwenye kazi hiyo. Lakini kiasili hawakupendi kama ninavyokupenda. Zaidi ya kukuhamaisha zaidi kwa pesa zao na ndimi uzame zaidi. Ila anaekupenda ni yule anaekuzindua Katika njia ya potofu ili ujiepushe na hasira za Muumba.
Tunatekeleza agizo la Allah pale alipotuambia.
(وَذَكِّرْ فَإِنَّ الذِّكْرَىٰ تَنْفَعُ الْمُؤْمِنِينَ)
[Surat Adh-Dhariyat 55]
"Na kumbusha Hakika ukumbusho utawafaa waumini".
HITIMISHO.
Rudi katika njia ya Sawa kwani mitahani ya Allah hakiepukiki unaweza ukawa na pesa lakini ukakosa amani au afya.... Na wala kurudi kwako kwenye muziki si kwamba ndio utaikimbia mitihani hiyo. Tena huenda ikazidi. Rudi katika njia ya Haki Allah hajaribiwi maana naona unarudi kwa kishondo kutangaza uovu siku tukufu ya Iddi. Siku ambayo Allah amewataka waja wake wamtaje zaidi. Rudi katika njia ya kabla ya muda haujapita.
Tunamuomba Allah atusamehe makosa yetu tunayofanya hadharani au sirini na atuingize jannah pamoja na Mtume saw.
0714244930 WhatsApp.
Tusaidiane kushare.