Kwako mwanamke uliyezaa

Emoj

JF-Expert Member
Oct 9, 2015
838
1,302
Kwanza hongera kwa kuitwa mama maana kuzaa sio kitu rahisi. Ndio umezaa nje ya ndoa ila Mungu wako unaemwamini ni wa rehema na anasamehe.Najua watu wanakuona malaya, hufai,mkosaji ila tambua tu kwamba lipo kusudi la Mungu kukuleta wewe na huyo mwanao duniani,haijalishi kwamba amekuja nje ya ndoa lipo kusudi.
Kuzaa haimaanishi kwamba ndo mwisho wa maisha, usikatishwe tamaa na maneno ya watu wanaosema mwanamke akishazaa haolewi,mmwanamke aliyezaa ni malaya hadi ukafikia hatua ya kujishusha thamani No! wewe ni wathamani sana. Omba Mungu wako,usijiachie, jipende,jikubali, piga kazi,kuwa smart,vaa pendeza, achana kudate na wavulana.
USIKATISHWE TAMAA, simama kama SHUJAA. Usijirahisi tu ukidhania kwa vile umezaa basi ndo thamani yako imekwisha. wewe ni hot cake bado. hebu jiweke vizuri,haki yako kwa Mungu iko palepale, Kuolewa kupo palepale tena na yule mtu ambaye ulikuwa unatamani siku moja uolewe na mtu mwenye tabia ulizoziwekea priority.
Hebu jiulize mtaani kwenu ni wangapi hawajazaa ila kila siku wanalalamika umri unaenda hawaolewi? ok ni wangapi wamezaa na wameolewa?? sasa kwanini ujishushe thamani kwa kusikiliza maneno ya watu?.Simama mwanamke tena simamia kucha, usikubali kuyumbishwa na maneno ya watu kwa vile tu umezaa?
Kingine huyo aliyekuzalisha kama hana mwelekeo achana nae,usikubali sura yako ikunjamane kisa aliyekuzalisha. hataki kulea mtoto achana nae Simama mwenyewe lea mwanao, usitake kufatanafatana na huyo mvulana aliekuzalisha na maneno,mara umtafute kumweleza habari za mtoto mara akujibu vibaya, kama ana shida na mtoto amtafute mwenyewe achana kumtafuta.Ya nini kuanza kukunja sura uzeeke mapema kisa mwanaume asiyetambua thamani yako??.kuwa busy ,furahi, haina haja ya kukunjamana, relax!,haya ni maisha na Mungu ndo anapanga.
WEWE NI WA THAMANI SANA MWANAMKE ULIYEZAA KAMWE USIKUBALI KUYUMBISHWA KWA NAMNA YEYOTE ILE.UNA HAKI SAWA NA MWANAMKE AMBAYE HAJAZAA.TEMBEA KIFUA MBELE. MAJESTICALLY KABISA.
 
Kwakuzaa nyumbani kwa wazazi wako?hata tuipake rangi haibadilishi kua amekosea tyming ila sio chakujuuuta ushindwe kufanya mambo mengine na aangalie tu asije akazaa wapili
 
mpendwa kukosea kupo, hata wewe unakosea. cha kushukuru tu ni kwamba Mungu sio Lalamaliwato.
Hujaelewa maana yangu!unamtia moyo anahisi alifanya right thing at the end of the day anarudia tena!kweli kakosea ila haimaanishi kila siku ataonewa huruma kwa uzembe wake mwenyewe ,
 
Hujaelewa maana yangu!unamtia moyo anahisi alifanya right thing at the end of the day anarudia tena!kweli kakosea ila haimaanishi kila siku ataonewa huruma kwa uzembe wake mwenyewe ,
mpendwa hapo juu nimeeleza vizuri tu kwamba Mungu ni wa rehema anasamehe .haijalishi umefanya kosa mara ngapi Mungu anasamehe. na pia Haitaji huruma ya mwanadamu maana huruma mwanadamu ina mwisho ila huruma ya Mungu haina mwisho.
 
Hujaelewa maana yangu!unamtia moyo anahisi alifanya right thing at the end of the day anarudia tena!kweli kakosea ila haimaanishi kila siku ataonewa huruma kwa uzembe wake mwenyewe ,
Mpendwa kosa limeshatokea, tuendelee kuwalaumu for the rest of their lives? Hata sisi kuna dhambi tumefanya apart from kuzaa kabla ya ndoa lakini tunajitahidi kuua guilt zetu ili tupate amani na maisha yaendelee. Alichotaka kukisema Emoj ni sio kwamba waendelee kuzaa nje ya ndoa ila anataka wasiendelee kukaa chini na kujilaumu na kujiona hawafai kwa walichofanya, wala wasione kama maisha yao ndo kama yamefika mwisho. Kung'uta mavumbi simama maisha yaendelee, uzuri wote tunaishi kwa neema ya Mungu. Na hakuna mwenye haki sana na neema ya Mungu, yeye anaitoa bure tu kwa Kila mtu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom