Kwako Mheshimiwa LUKUVI

Marabou

New Member
Mar 14, 2019
1
0
Taarifa ninayokutumia inahusu eneo lililopo Manispaa ya Ilemela, Kata ya Pasiansi, Mtaa wa Bwiru Press. Mwezi wa 10 mwaka 2018 Manispaa ya Ilemela ilitoa tangazo la uuzaji wa viwanja katika eneo hili na kuwahusisha Wananchi juu ya uwekaji wa Barabara za Mtaa huu.
Pamoja na Wananchi kuitikia wito huo utekelezaji haukufanyika kwa maeneo ambayo barabara inapita. Cha kushangaza ni kwamba, jana 14/3/2019 Greda limeletwa kumega viwanja vya watu kwa nia ya kuweka barabara sehemu ambayo haikupaswa kuwa na barabara kama ramani ya Manispaa iliyotolewa mwaka jana mwezi October wakati wa zoezi la uuzaji wa viwanja. Kinachofanyika ni kwamba, barabara inahamishwa kutoka eneo iliyopaswa kuwa na kumega viwanja vya Wananchi, ili vipatikane viwanja ambavyo Maafisa wa Ardhi watajimilikisha ambavyo kimsingi havijulikani na uongozi wa Manispaa ya Ilemela, 'ulafi wa ajabu kabisa'. Na ni nani anayelipa fidia kwa uhalifu huu. Kwa kufanya hivyo Mhe. Waziri wamekiuka
1. Agizo la Mhe. Rais kwamba, maeneo ya watu yasimegwe na wapimiwe. Sasa tunajiuliza jeuri ya kumega maeneo ya watu wanaipata wapi?!!
2. Pamoja na kwamba, Idara ya Ardhi ilipima eneo hilo na kuweka 'beacon' utoaji wa hati umekuwa ni shida. Awali walisema ramani imepelekwa Wizarani, lakini sasa wanasema fedha zilizochangwa na Wananchi hazijulikani ziliwekwa katika akaunti gani. Kwa maana hiyo Wananchi wachange tena. Kwa suala hili la fedha tunaomba TAKUKURU ishirikishwe

N.B: sketch waliyotumia kuhalalisha uhalifu imeambatabishwa
 

Attachments

  • VID-20190314-WA0024.mp4
    10.7 MB · Views: 7
  • VID-20190314-WA0023.mp4
    6.5 MB · Views: 6
  • IMG_20190314_211206_331.JPG
    IMG_20190314_211206_331.JPG
    174.2 KB · Views: 11
Back
Top Bottom