KING ASSENGA
JF-Expert Member
- Oct 8, 2016
- 929
- 1,499
Nakuja kwako Mungu, shingoni yamenifika,
Naongea kwa uchungu, na machozi kadhalika
Wajua moyoni mwangu, hauwezi kufichika
Nisaidie Rabana, shingoni yamenifika,
Magonjwa yanitikisa, maumivu kadhalika
Nisamehe kwa makosa, kweli nimeadhibika
Huku usije nitosa, wanafiki wakacheka
Nisaidie Rabana, shingoni yamenifika
Elimu nadharaulika, kiuchumi kadhalika
Siniache nateseka, nani atanikumbuka
Kwako ninajisimika , Tumaini la hakika
Nisaidie Rabana, shingoni yamenifika
Malengo nikiyaweka , leo kesho yatibuka
Shida ghafla zaibuka, na magonjwa kadhalika
Kwa juhudi napigika, sio uzembe hakika
Nisaidie Rabana, shingoni yamenifika
Kuoa kwa tamanika, Eva bado namkumbuka
Kwa uchawi asifika, uchumba ukakatika
Hakubali kuachika, wanilinde Malaika
Nisaidie Rabana, shingoni yamenifika
Naongea kwa uchungu, na machozi kadhalika
Wajua moyoni mwangu, hauwezi kufichika
Nisaidie Rabana, shingoni yamenifika,
Magonjwa yanitikisa, maumivu kadhalika
Nisamehe kwa makosa, kweli nimeadhibika
Huku usije nitosa, wanafiki wakacheka
Nisaidie Rabana, shingoni yamenifika
Elimu nadharaulika, kiuchumi kadhalika
Siniache nateseka, nani atanikumbuka
Kwako ninajisimika , Tumaini la hakika
Nisaidie Rabana, shingoni yamenifika
Malengo nikiyaweka , leo kesho yatibuka
Shida ghafla zaibuka, na magonjwa kadhalika
Kwa juhudi napigika, sio uzembe hakika
Nisaidie Rabana, shingoni yamenifika
Kuoa kwa tamanika, Eva bado namkumbuka
Kwa uchawi asifika, uchumba ukakatika
Hakubali kuachika, wanilinde Malaika
Nisaidie Rabana, shingoni yamenifika