Kwako mkuu wa jeshi la polisi Tanzania IGP Mangu.
Salaam zetu kwako mkuu.
Naanza moja kwa moja na maumivu yaliyotufanya sisi tour operators wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro tukae na kukuandikia.
Ni muda mrefu madereva/guides wetu wamekuwa wananyanyaswa na polisi kitengo cha usalama barabarani na tumekuwa tukipeleka malalamiko yetu kwa ngazi husika bila kupatiwa ufumbuzi wowote.
Ni hivi; drivers wanakuwa na wajibu wa kuwapeleka wageni kwenye mbuga zetu za wanyama au kupeleka/kuchukuwa wageni wanaokwenda/kutoka kwenye milima yetu ya Kilimanjaro au Meru, wamekuwa wanakamatwa na kutafutiwa makosa ambayo hayapo kisha kupoteza muda mrefu kwa kulazimishwa kutoa rushwa, matokeo yake kuchelewesha wageni wanakopelekwa matokeo yake wageni wanatuandika vibaya kwenye mitandao maarufu duniani ambayo inasomwa na watalii wengi kabla hawajaja nchini ya 'Trip Advisor', 'Lonely Planet', 'Safari Booking' na nyinginezo as if either hatuna leseni au magari hayana bima na vitu kama hivyo while tumelipa kodi na ada zote.
Kwa hali inavyoendelea sasa wameshaanza kugundua kuwa sio kosa la tour operators ila ni tamaa za baadhi ya askari wa barabarani....hii licha ya kulichafua jeshi lako mkuu inachafua usafi wa nchi yetu kama mojawapo ya destination nzuri ya kutembelea.
Nina mifano michache nataka nikupe kuweka kumbukumbu sawa...Kuna madereva walikuwa wanapeleka wageni wawahi kuingia airport ya KIA ili warudi makwao lakini walipofika eneo la KIKATITI walisimamishwa kwa muda mrefu sana (huwa wanasimamisha hadi magari kumi na kuanza kukagua moja moja na ukiwalalamikia wanakuruka nakukagua ya nyuma yako)hali hiyo ilisababisha wageni wachelewe ndege yao na matokeo yake wakalipa extra charges ambazo ni unneccesary. Matokeo yake ndio kama nilivyokueleza pale juu.
Mfano mwingine mara tu baada ya wageni kutoka mjini wakielekea mbuga zetu, kwanza wanaanza kusimamishwa kuanzia maeneo ya mbele kidogo ya Meru Posta, then pale Ngarenaro, Majengo, Kisongo, Miserani (DUKA BOVU), Mti Mmoja, Makuyuni, Mto wa Mbu, Manyara Kibaoni kituo kidogo cha polisi (hapa ndio pabaya sana) Rhotia na Karatu.
Mkuu kila nilipopataja drivers wanasimamishwa na wanatumia sio chini ya robo saa hadi one hour...lunch box wageni wanakula wakiwa kwenye gari kabla hawajafika Ngorongoro, aibu iliyoje!!!!
Kuna siku walishusha wageni kwenye gari wakimtisha guide kuwa asipowapa shilingi laki mbili hawatoachia gari, wageni walipiga simu ubalozini kwao baada ya muda ubalozi ulinipigia simu nikaenda kituo kikuu cha Arusha nikawapa wakaongea na balozi ndipo walipowapigia kituo husika cha Manyara Kibaoni wakarudisha ile laki mbili kwa guide na kuwaachia wageni ikiwa ni takribani baada ya masaa matatu!!!
Tuna mengi tu ambayo tunayo ila tumekujulisha hayo kwa leo kwa kuwa hata guides wana mpango wakugoma kuhusu uonevu huu.
Ombi letu kwako ni kuwa magari yakaguliwe na yawe na karatasi ya ukaguzi pale mbele inayoonekana kabla ofisa yeyote hajalisimamisha gari husika na zoezi hili lifanyike kwa wakati ambao sio wageni wakiwa kwenye gari. Pia magari yote yaliyobeba watalii yasiwe yanasimamishwa kiholela kama inavyofanyika sasa na mwisho fuatilia na wahusika wanaofanya haya ambao ni baadhi ya maofisa waliopewa dhamana hiyo waadhibiwe/waonywe ili kuondoa hali hii.
Tumeandika hapa kwani tunajua wewe ni mfuatiliaji na hakika utalipatia ufumbuzi wa kudumu tatizo hili.
Tunatanguliza shukrani. Ni sisi
Jamii ya Utalii mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.