Kwako Comrade Nape siku ya kufanya mkutano jimboni Mtama

mabuba

Senior Member
Dec 5, 2006
133
90
Kwako Comrade Nape

Nakusalimu kiongozi, pole na hongera majukumu ya kulitumikia Taifa.

Kiongozi ninakuandikia waraka huu lengo ni kutaka kujua kweli inayosambaa mitandaoni kuwa mnamo tarehe 8 Aprili, 2017 utakwenda jimboni kwako, na moja ya shughuli utakayoifanya ni kuongea na wapiga kura wako. Mimi sina shaka na wewe kuongea na wapiga kura wako hata kidogo, kwani ni kawaida kwa mbunge kuongea na wapiga kura wako. Kama ni kweli umepanga kufanya hivyo naomba uzingatie yafuatayo:

i. Naomba nikusihi sana tumia busara katika kuongea, kama busara itakushinda usiongee. Kuna tetesi kuwa endapo utafanya hivyo, ama ni wewe mwenyewe au jirani zetu, wameandaa kikundi cha kushangilia na kikiwa na mabango ambayo sio mema sana kwa chama chetu. Kama ni wewe jiulize mara mbili mbili.

ii. Umesema unakwenda kusema kweli, hakikisha kweli iwe kweli, kweli kweli, hata upande wako useme kweli yako, yaani udhaifu wako, usiseme udhaifu wa watu wengine tu, ukidhani wewe huna mawaa.

iii. Siku unaongea na waandishi wa habari uliowaandaa, ulisema umekipigania Chama, hili mimi sina shaka nalo hata chembe. Naomba nikukumbushe tu, ukirudia kusema hili, pia waambie hiyo ndio ilikuwa ajira yako katika Chama, na ulikuwa unalipwa ili ukipiganie Chama chetu. Kukipigania chama kwako wewe kunatofautiana sana na mabalozi ambao walipigana kufa na kupona ili chama kishinde, pasi malipo yoyote, lakini wewe ulikuwa unalipwa mshahara na stahiki zingine. Ingelikuwa ajabu kweli kweli kama Katibu wa Itikadi na Uenezi asikipiganie chama chake.

iv. Comrade, nakukumbusha tu wakati kulikuwa na dalili za wewe kuanza kupishana na Mwenyekiti wetu, kuna kundi la watu lilitokea likawa “linakutia hasira” kundi hili lilidiriki hata kukuambia ujiuzulu. Kundi hilo hilo ulipotolewa katika nafasi ya uwaziri, lilianza kukuzomea, likikuambia kwamba wewe ulikuwa mtesi wa wengine sasa nawe yamekukuta. Lilishadadia kusema Bunge live, sheria ya mtandao, mafisadi kukatwa 2015 ni wewe ulisababisha hivyo, ngoja uonje joto la jiwe. Kundi hili hili tena ndilo linaloeneza hiki unachotaka kufanya, nadhani hapa uwe mbayuwayu.

v. Nakusihi sana, mimi bado naona kuna nafasi ya kuwekana sawa, kama ulivyosema siku ile wakati unatolewa, kwamba hukuulizwa wakati wa kupewa Uwaziri, ni sawa. Lakini ulipopewa hukuitwa waandishi wa habari wala hukufanya maandamano jimboni kwako. Tumia busara Comrade, sasa kama kila kiongozi akitolewa katika nafasi yake akaitisha vyombo vya habari, itakuwaje? Kumbuka ulipokuwa mwenezi, ambapo ulipowatambua mawaziri mizigo, wengine walitolewa, lakini hawakuitisha vyombo vya habari.

Sina mengi Comrade, ni mimi mmoja wa watu waliokipigania chama na bado nasonga mbele kukipigania Chama pasi malipo yoyote kaka, tofauti na wewe uliyepigania chama wakati unalipwa mshahara mzuri tu na marupurupu.

Wasalaamu

Kisena Mabuba

Mwanamtaa
 
Ukiona mwana chama kile mwenye umri kama mimi anakitetea sana chama kile ilihali hana chochote ujue basi ana matatizo ya akili ama kaishia middle school tu ama vyote kwa pamoja
Nashukuru chama hichi kunipa vyote nilivyonavyo huku wengne wakibakia washabiki
 
Umeandika vizuri sana mkuu 100%
 
Nape hana adabu, hana akili, Nape sio jasiri, Nape anadeka, Nape anajikomba kwa watu ambao hawana msaada kwake, paja la wema sepetu aliona lna faida kuliko familia yake na taifa

1. Nape hakutakiwa kuunda kamati/tume iliyosheheni waandishi wa habari kuchunguza tukio la waandishi wa habari kuvamiwa!! na kati ya hao kuna zezeta anaitwa Balile ambaye wiki yote hiyo gazeti lake liliandika negative tu za bwana Makonda. Kamati yake ilitakiwa kuundwa na watu mbalimbali sio wa kada moja tu

2. Nape alitakiwa kuunda tume kwa go ahead ya rais ( kwa sababu kawekwa pale kumsaidia rais) , kibaya rais alipiga stop ya swala hili!!!! kijana Nape ( mwili mkubwa) hakuona anakosea, angekuwa na akili angemsukumia swala hili katibu mkuu wake!! au angeihamishia polisi -nilisema ana akili ndogo

3. Nape akiwa mwanaserikali, Makonda mwanaserikali na kaka yao/bosi wao Magu kwa serikali hiyo hiyo...Nape hakuwa na akili ya kupiga simu??friendly? maana msuguano wa wazi wa Nape na Makonda ulikuwa wazi

4. Kamati ya Nape ilisema, ilithibitisha na ilieleza WAZI WAZI kuwa Makonda hakuhusika na ile habari, ile habari iliandaliwa na shilawadu then wao wakamuita Makonda....sijaona hata leo HII, SI KAMATI, SI JUKWAA LA WAHARIRI AMBAO waliionya clouds kwa kile walichokifanya, HATA LEO SIJASIKIA mtu yeyote ambaye anaonyesha pia kuwa clouds nao wana makosa...si wahariri, si nape, si hiyo kamati............

5. Magufuli alilikataza, Nape basi angepata go ahead hata ku seek advice ya PM kama alikuwa anamchukia MAGU, Kuwa na mawasiliano mabaya na bosi wako, ni dalili ya chuki pia

6. Nape na kikundi chake cha wazee wa CCM, ambao wanajulikana kwa wauza unga, wauza meno ya tembo, waliitengeneza hii move hii ifike pabaya rais atetereke, Magu kakipiga kichwa hiki, Nape alifanya upumbavu au ufala( kwa sauti ya Halima mdee)... Movie ya Makonda ya kutangaza na kuchafua ingeendeea hata leo, Kinana angekuwa ndani, nanilii yule angeuwa ndani.......hao akina Gwajima, ni vi dealer vidogo vidogo tu,

7. Makonda ni TISS, ambaye alikosea njia akaingizwa kwenye siasa! Nape alitakiwa ajue hili vizuri kuliko yeyote yule!!!
 
Unamtisha nape? Andaeni vijana kwa sasa muwape AK 47, wamumalize maana pisto ilishindwa hio nazani itawapa matunda muyatakayo

Zidumu fikara za mwenyekiti na bashite
 
Tunahitaji watanzania walio huru kusema ukweli hata kama vyama vyao vinakasirika Nape aseme ukweli kwa maslahi ya taifa kwa ujumla(na iwe kweli).Lakini asiende kutafuta huruma kwa wananchi kwa kusema uongo.
 
Issue ya kutumia vizuri mdomo ni shida kwa kaka etu huyu.Hajui aseme nini wapi na kwa wakati gani.Akibadilika katika hili hata aite waandishi laki moja hatokuwa na la kujali.
 
  • Thanks
Reactions: UCD
Mbona Kitwanga aliongea na wapiga kura wake? Kwann Nape asiongee na wapiga kura wake? Mnaogopa nn? Kuna nn chini ya kapeti ambacho hamtaki Nape akifunue tukione?
 
Nape hana adabu, hana akili, Nape sio jasiri, Nape anadeka, Nape anajikomba kwa watu ambao hawana msaada kwake, paja la wema sepetu aliona lna faida kuliko familia yake na taifa

1. Nape hakutakiwa kuunda kamati/tume iliyosheheni waandishi wa habari kuchunguza tukio la waandishi wa habari kuvamiwa!! na kati ya hao kuna zezeta anaitwa Balile ambaye wiki yote hiyo gazeti lake liliandika negative tu za bwana Makonda. Kamati yake ilitakiwa kuundwa na watu mbalimbali sio wa kada moja tu

2. Nape alitakiwa kuunda tume kwa go ahead ya rais ( kwa sababu kawekwa pale kumsaidia rais) , kibaya rais alipiga stop ya swala hili!!!! kijana Nape ( mwili mkubwa) hakuona anakosea, angekuwa na akili angemsukumia swala hili katibu mkuu wake!! au angeihamishia polisi -nilisema ana akili ndogo

3. Nape akiwa mwanaserikali, Makonda mwanaserikali na kaka yao/bosi wao Magu kwa serikali hiyo hiyo...Nape hakuwa na akili ya kupiga simu??friendly? maana msuguano wa wazi wa Nape na Makonda ulikuwa wazi

4. Kamati ya Nape ilisema, ilithibitisha na ilieleza WAZI WAZI kuwa Makonda hakuhusika na ile habari, ile habari iliandaliwa na shilawadu then wao wakamuita Makonda....sijaona hata leo HII, SI KAMATI, SI JUKWAA LA WAHARIRI AMBAO waliionya clouds kwa kile walichokifanya, HATA LEO SIJASIKIA mtu yeyote ambaye anaonyesha pia kuwa clouds nao wana makosa...si wahariri, si nape, si hiyo kamati............

5. Magufuli alilikataza, Nape basi angepata go ahead hata ku seek advice ya PM kama alikuwa anamchukia MAGU, Kuwa na mawasiliano mabaya na bosi wako, ni dalili ya chuki pia

6. Nape na kikundi chake cha wazee wa CCM, ambao wanajulikana kwa wauza unga, wauza meno ya tembo, waliitengeneza hii move hii ifike pabaya rais atetereke, Magu kakipiga kichwa hiki, Nape alifanya upumbavu au ufala( kwa sauti ya Halima mdee)... Movie ya Makonda ya kutangaza na kuchafua ingeendeea hata leo, Kinana angekuwa ndani, nanilii yule angeuwa ndani.......hao akina Gwajima, ni vi dealer vidogo vidogo tu,

7. Makonda ni TISS, ambaye alikosea njia akaingizwa kwenye siasa! Nape alitakiwa ajue hili vizuri kuliko yeyote yule!!!
Bashite camp wekeni akiba ya maneno. Nape hastahili matusi mepesi Kama hayo.
 
Kwako Comrade Nape

Nakusalimu kiongozi, pole na hongera majukumu ya kulitumikia Taifa.

Kiongozi ninakuandikia waraka huu lengo ni kutaka kujua kweli inayosambaa mitandaoni kuwa mnamo tarehe 8 Aprili, 2017 utakwenda jimboni kwako, na moja ya shughuli utakayoifanya ni kuongea na wapiga kura wako. Mimi sina shaka na wewe kuongea na wapiga kura wako hata kidogo, kwani ni kawaida kwa mbunge kuongea na wapiga kura wako. Kama ni kweli umepanga kufanya hivyo naomba uzingatie yafuatayo:

i. Naomba nikusihi sana tumia busara katika kuongea, kama busara itakushinda usiongee. Kuna tetesi kuwa endapo utafanya hivyo, ama ni wewe mwenyewe au jirani zetu, wameandaa kikundi cha kushangilia na kikiwa na mabango ambayo sio mema sana kwa chama chetu. Kama ni wewe jiulize mara mbili mbili.

ii. Umesema unakwenda kusema kweli, hakikisha kweli iwe kweli, kweli kweli, hata upande wako useme kweli yako, yaani udhaifu wako, usiseme udhaifu wa watu wengine tu, ukidhani wewe huna mawaa.

iii. Siku unaongea na waandishi wa habari uliowaandaa, ulisema umekipigania Chama, hili mimi sina shaka nalo hata chembe. Naomba nikukumbushe tu, ukirudia kusema hili, pia waambie hiyo ndio ilikuwa ajira yako katika Chama, na ulikuwa unalipwa ili ukipiganie Chama chetu. Kukipigania chama kwako wewe kunatofautiana sana na mabalozi ambao walipigana kufa na kupona ili chama kishinde, pasi malipo yoyote, lakini wewe ulikuwa unalipwa mshahara na stahiki zingine. Ingelikuwa ajabu kweli kweli kama Katibu wa Itikadi na Uenezi asikipiganie chama chake.

iv. Comrade, nakukumbusha tu wakati kulikuwa na dalili za wewe kuanza kupishana na Mwenyekiti wetu, kuna kundi la watu lilitokea likawa “linakutia hasira” kundi hili lilidiriki hata kukuambia ujiuzulu. Kundi hilo hilo ulipotolewa katika nafasi ya uwaziri, lilianza kukuzomea, likikuambia kwamba wewe ulikuwa mtesi wa wengine sasa nawe yamekukuta. Lilishadadia kusema Bunge live, sheria ya mtandao, mafisadi kukatwa 2015 ni wewe ulisababisha hivyo, ngoja uonje joto la jiwe. Kundi hili hili tena ndilo linaloeneza hiki unachotaka kufanya, nadhani hapa uwe mbayuwayu.

v. Nakusihi sana, mimi bado naona kuna nafasi ya kuwekana sawa, kama ulivyosema siku ile wakati unatolewa, kwamba hukuulizwa wakati wa kupewa Uwaziri, ni sawa. Lakini ulipopewa hukuitwa waandishi wa habari wala hukufanya maandamano jimboni kwako. Tumia busara Comrade, sasa kama kila kiongozi akitolewa katika nafasi yake akaitisha vyombo vya habari, itakuwaje? Kumbuka ulipokuwa mwenezi, ambapo ulipowatambua mawaziri mizigo, wengine walitolewa, lakini hawakuitisha vyombo vya habari.

Sina mengi Comrade, ni mimi mmoja wa watu waliokipigania chama na bado nasonga mbele kukipigania Chama pasi malipo yoyote kaka, tofauti na wewe uliyepigania chama wakati unalipwa mshahara mzuri tu na marupurupu.

Wasalaamu

Kisena Mabuba

Mwanamtaa
Ndugu Kisena Mabuba umenena vema sana! Kuna watu wamekipigania sana CCM tena bila malipo kuliko hata huyu Nape Nnauye! Kinachomuumiza Nape ni kuona Rais Dr.Magufuli an "outsider" amemtumbua kwenye Uwaziri! Nape atambue kuwa asipokuwa makini na hizi movement zake yeye na Ndugu yake Shyrose Banji baada ya 2020 wanaweza kurudia zama zile ambazo Nape alikuwa anaendesha kiji-stationery na Shyrose Banji akiwa Kamanda wa Vijana wa CCM Kijitonyama!

Nape asikubali kudanganywa na akina Kangi Lugola,hao ni WACHUMIA TUMBO tu waliokosa nafasi na sasa wanataka kutumia mgongo wa Nape kuonyesha hisia zao dhidi ya Rais Dr.Magufuli!
Wanasiasa wetu wengi ni watu wenye NJAA na WACHUMIA TUMBO tu ! na Rais wetu Dr. Magufuli analijua hili!

Kama kuna Mtu anabisha hili basi amtafute Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe amuulize kama bado anazo zile ajenda za kumwadhibu Rais Magufuli kupitia Bunge?,au hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kama ishara ya kutaka kuiangusha Serikali yake ? Na yote hii ni baada ya Rais Magufuli kumteua mshauri mkuu wa Zitto na Chama chake cha ACT Profesa Kitila Mkumbo! A pure political blackmail !

Nape usikubali kudanganywa na WACHUMIA TUMBO kwamba wanaweza kukutumia kumzuia Dr.Magufuli kugombea Urais kupitia CCM come 2020! Subiri utaona kuanzia 2019 jinsi wabunge wa CCM watakavyoanza kumpamba Rais Magufuli ili tu Majina yao YARUDI kwenye kugombea Ubunge!

Anguko lako mimi nililiona mapema,rejea makala yangu humu JF yenye kichwa JE WATANZANIA TUNAMFAHAMU PAUL MAKONDA?.
 
Tunahitaji watanzania walio huru kusema ukweli hata kama vyama vyao vinakasirika Nape aseme ukweli kwa maslahi ya taifa kwa ujumla(na iwe kweli).Lakini asiende kutafuta huruma kwa wananchi kwa kusema uongo.
Chacha Wangwe aliposema ukweli kilitokea nini!?
 
Du! Kisena,natamani kuirudia kuisoma thread yako kila wakatini tamu kinyama.

Huo ndo ukweli ambao Nape anatakiwa kuufahamu,hujapepesa neno,big up man
 
kunako tarehe 23/03/2017 in Lindi kulizagaa taarifa ya kuwa Nape anaenda Mtama na watu waliandaa magari ili wampokee.......lakini hakutokea.............
 
Nape anamuona rais ni mpita njia ila yeye ndio mwenye chama,kisa alikuwa katibu uenezi.
 
kwa kuongezea,Nape bado ana nafasi kwenye serikali ya Awamu ya tano.
kinachotakiwa ni yeye kua mpole,na kumsapoti mkulu.

Rejea Ana Kilango.
Akijifanya ngangari ndo anapotea hivyo.
Ushauri wangu aachane kulumbana na mkulu,kama ulivyosema,anajazwa gas ili mkulu ampoteze kwenye ulingo wa siasa,na anaweza kweli
 
Kwako Comrade Nape

Nakusalimu kiongozi, pole na hongera majukumu ya kulitumikia Taifa.

Kiongozi ninakuandikia waraka huu lengo ni kutaka kujua kweli inayosambaa mitandaoni kuwa mnamo tarehe 8 Aprili, 2017 utakwenda jimboni kwako, na moja ya shughuli utakayoifanya ni kuongea na wapiga kura wako. Mimi sina shaka na wewe kuongea na wapiga kura wako hata kidogo, kwani ni kawaida kwa mbunge kuongea na wapiga kura wako. Kama ni kweli umepanga kufanya hivyo naomba uzingatie yafuatayo:

i. Naomba nikusihi sana tumia busara katika kuongea, kama busara itakushinda usiongee. Kuna tetesi kuwa endapo utafanya hivyo, ama ni wewe mwenyewe au jirani zetu, wameandaa kikundi cha kushangilia na kikiwa na mabango ambayo sio mema sana kwa chama chetu. Kama ni wewe jiulize mara mbili mbili.

ii. Umesema unakwenda kusema kweli, hakikisha kweli iwe kweli, kweli kweli, hata upande wako useme kweli yako, yaani udhaifu wako, usiseme udhaifu wa watu wengine tu, ukidhani wewe huna mawaa.

iii. Siku unaongea na waandishi wa habari uliowaandaa, ulisema umekipigania Chama, hili mimi sina shaka nalo hata chembe. Naomba nikukumbushe tu, ukirudia kusema hili, pia waambie hiyo ndio ilikuwa ajira yako katika Chama, na ulikuwa unalipwa ili ukipiganie Chama chetu. Kukipigania chama kwako wewe kunatofautiana sana na mabalozi ambao walipigana kufa na kupona ili chama kishinde, pasi malipo yoyote, lakini wewe ulikuwa unalipwa mshahara na stahiki zingine. Ingelikuwa ajabu kweli kweli kama Katibu wa Itikadi na Uenezi asikipiganie chama chake.

iv. Comrade, nakukumbusha tu wakati kulikuwa na dalili za wewe kuanza kupishana na Mwenyekiti wetu, kuna kundi la watu lilitokea likawa “linakutia hasira” kundi hili lilidiriki hata kukuambia ujiuzulu. Kundi hilo hilo ulipotolewa katika nafasi ya uwaziri, lilianza kukuzomea, likikuambia kwamba wewe ulikuwa mtesi wa wengine sasa nawe yamekukuta. Lilishadadia kusema Bunge live, sheria ya mtandao, mafisadi kukatwa 2015 ni wewe ulisababisha hivyo, ngoja uonje joto la jiwe. Kundi hili hili tena ndilo linaloeneza hiki unachotaka kufanya, nadhani hapa uwe mbayuwayu.

v. Nakusihi sana, mimi bado naona kuna nafasi ya kuwekana sawa, kama ulivyosema siku ile wakati unatolewa, kwamba hukuulizwa wakati wa kupewa Uwaziri, ni sawa. Lakini ulipopewa hukuitwa waandishi wa habari wala hukufanya maandamano jimboni kwako. Tumia busara Comrade, sasa kama kila kiongozi akitolewa katika nafasi yake akaitisha vyombo vya habari, itakuwaje? Kumbuka ulipokuwa mwenezi, ambapo ulipowatambua mawaziri mizigo, wengine walitolewa, lakini hawakuitisha vyombo vya habari.

Sina mengi Comrade, ni mimi mmoja wa watu waliokipigania chama na bado nasonga mbele kukipigania Chama pasi malipo yoyote kaka, tofauti na wewe uliyepigania chama wakati unalipwa mshahara mzuri tu na marupurupu.

Wasalaamu

Kisena Mabuba

Mwanamtaa
Siamini Nape anaweza kwenda jimboni kwake akaongee mambo yanayokishambulia chama huyo sio Nape nimjuaye. Nape kama kiongozi na mbunge lazima aongee na watu wake waliompigia kura pia lazima awaeleze nini kilitokea sioni ni kosa hata kidogo anatimiza wajibu wake
 
Back
Top Bottom