Naishauri CHADEMA ianzishe chombo kinachoitwa "Mabaraza ya Wazee" kwa kila ngazi nchini

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
4,049
3,698
Mimi ni mfuatiliaji mkubwa wa masuala ya kisiasa hapa nchini.
Nimeona zoezi la maandalizi ya uchaguzi wa viongozi Serikali za mitaa lilivyoanza na linavyoendelea.

Pia nimesikiliza matamko ya viongozi wa CHADEMA kuhusu mwenendo wa zoezi hilo. Niwe muwazi, kuna mambo baadhi hayajajulikana na wengi kuhusu kitu kinaitwa "dosari" za ujazaji fomu za wagombea. Kwa utafiti wangu niliofanya kwa kuona, kusikia, na kuambiwa, nimejiridhisha kwa yafuatayo;-.

1. Baadhi ya walioitwa wameenguliwa kwa dosari za ujazaji ni "MAMLUKI" walioingizwa makusudi au kwa RUSHWA ndogo tuu ili waharibu fomu na kutoa fursa mgombea fulani apite. Hawakuwa na credibility kwa CHADEMA.

2. Viongozi wa CHADEMA kwa sasa walioko hasa ngazi za kata na Wilaya wamepoteza imani kwa Chama chao. Wapo kimaslahi kuangalia upepo unavyovuma. Na wanayumbishwa kirahisi na vyama vyenye nguvu maeneo waliko. Hivyo ni rahisi kununulika kwa vile hakuna overseer wa karibu.

3. Viongozi wa Juu wa CHADEMA wanalishwa taarifa nyingi na baadhi zisizo na uhalisia kutoka ngazi za chini kwa vile tayari viongozi wa chini wanaotoa taarifa wako kwenye kundi linalofanya niliyoeleza na 1 na 2 hapo juu.

Matokeo yake viongozi hao ngazi ya Taifa wanakuwa na mitizamo tofauti na yenye migongano ya hapa na pale, mwishowe CHADEMA inaonekans kuyumba sana kipindi hiki kuelekea Uchaguzi.

Nini kifanyike kwa hayo machache niliyoeleza?

1. Kama CHAMA kina nia ya dhati ya kusonga mbele, kiunde "MACHINERIES" za Wazee tena wawe "INTELECTUALS" wenye fani mbalimbali hivi kwa kila ngazi za chama. Hao kikatiba wawe na nafasi zao za kushauri,kuelekeza mambo mbalimbali ya Chama. Pia wawe overseers wa mambo ya jumla ya chama ikiwemo uandikishaji wa wanachama, wapiga kura, teuzi za wagombea, ujazaji fomu,uwasilishaji, upigaji kura nk.

2. Ngazi ya Taifa, liwepo Baraza la Wazee wabobezi wa Chama. Hawa wawe na majukumu ya kusimamia sera na mienendo ya viongozi na Chama ngazi ya Taifa. Hili kama sijakosea lilikuwepo,sina uhakika kwa sasa kama lipo.

3. Mabaraza haya ya Wazee, yapewe ofisi zilizojitenga na watendaji wa kawaida wa Chama ili waweze kutekeleza majukumu yao bila upendeleo.

Maoni yangu haya ni kama utangulizi, yanaweza kuboreshwa zaidi ili CHADEMA iwe na muonekano na ukubaliki zaidi kuliko ilivyo sasa.
 
Mimi ni mfuatiliaji mkubwa wa masuala ya kisiasa hapa nchini.
Nimeona zoezi la maandalizi ya uchaguzi wa viongozi Serikali za mitaa lilivyoanza na linavyoendelea.
Gentleman,
kwahiyo umeamua kushauri mambo ambayo yapo tayari ndani ya Chadema right? ua kuna jambo unalitafuta kutoka kwa wafuasi wa Chadema 🐒
 
Gentleman,
kwahiyo umeamua kushauri mambo ambayo yapo tayari ndani ya Chadema right? ua kuna jambo unalitafuta kutoka kwa wafuasi wa Chadema 🐒
Una uhakika? Hayo yako level zipi na wanafanyia wapi kazi zao? ?
 

Attachments

  • images.jpeg
    images.jpeg
    7.6 KB · Views: 2
Gentleman,
inamaana humjui huyu right?🐒
Mkuu umeelewa maswali yangu ya msingi? Huyu ndiye anahudumu kuanzia ngazi za kata hadi Taifa? Naomba uniwekee hierachial order ya hilo Baraza la Wazee na kazi zake? Nje ya hapo, my thread still holds water!
 
Back
Top Bottom