Kwa wazee, akina mama wenye watoto na wajawazito wanaotumia daladala

Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
13,096
22,627
Habarini

Tunaishi katika nyakati za maisha yanayohitaji uelewa, upeo mkubwa wa kufikiri na kujiongeza kwa kasi ya radi.

Naelekezea huu uzi kwa wazee, raia yoyote mwenye matatizo ya kiafya ama changamoto ya kimwili ambayo haimruhusu kusimama katika daladala, akina mama na wadada wajawazito na waliokwisha jifungua, ambao hutumia usafiri wa public alimaarufu kama daladala.

Jamii hii ya watu wamekuwa na tabia ya kufanya makusudi ya kupanda gari ambayo imekwisha jaza na hakuna nafasi ya kuketi ila kusimama wakitarajia kuonewa huruma na watu wastaarabu na wapishwe siti waweze kuketi. Haya ni matumizi mabaya ya huruma za watu.

Hivi kiukweli ni gharama kiasi gani kwa mtu wa jamii hii kuzunguka na daladala au kuunganisha daladala za route fupi na ukafika unapokwenda bila kuabuse watu ambao hujisikia vibaya wewe mwenye hali hiyo ukiwa umesimama?!

Route nyingi za daladala katika kugeuza na kuzunguka na daladala huwa hazizidi shillingi 400 au 300 ambayo hata mtoto wa primary huwa anaweza imudu. Na hata ukikosa kulingana na hali yako mara moja moja ukiomba msaada kwa wasalia wema watakusaidia bila hiyana maana ni pesa ndogo sana.

Nyakati za jioni na asubuhi ni muda ambao raia wengi wanakuwa wanarejea kutoka ama kwenda makazini na ndio ni muda kuna abiria wengi vituoni na daladala ni za kugombania.Watu ni aidha wamechoka au wanastress za kazi au wanataka tu comfort ya kusafiri wakiwa katika hali ya utulivu.

Kwa watu wasioweza purukushani za kusimama au kubanana na kugombania usafiri huwa wana namna mbili za kusafiri bila usumbufu. Moja ni kusimama upande daladala zinakuja kuelekea direction ya kituo chenye abiria wengi huku kukiwa hamna watu daladala ikiwa tupu ili wageuke nayo na kupata siti bila kugusana na mtu.

Au kupanda route fupi ya kuunganisha mfano mimi ninakaa tabata mawenzi, then naweza panda daladala za kutoka posta buguruni, then nikifika buguruni napanda zinazoanzia buguruni hadi tabata mawenzi bila kupigana vipepsi.

Sasa unakuta mdada na mtoto au na tumbo lake yupo upande wa kituo chenye abiria wengi na yeye anasubiria gari zinakuja zikiwa zimejaa na yeye huyo anapanda, akiingia siti hakuna anasimama kabanwa. Mtu kama mimi nilitumia busara yangu ya kugeuka na daladala nimepata siti vizuri nimetulia nataka kusafiri kwa amani na utulivu wenye msawaziko wa raha na utukufu wa roho mtakatifu nikiona mzee, mwanamke mjamzito au mwenye mtoto amembebelea, au mgonjwa huwa siwezi kufanya ukauzu roho huwa inanisuta na hujisikia vibaya sana kukausha najikuta nasimama tu ili nikupishe uketi ila huku moyoni nikiwa na masononeko ya kuingia gharama ya bure kuzunguka na daladala na bado nikaishia kukupisha wewe uketi sababu tu umekuwa na kiburi cha kuabuse huruma za abiria wenye kujali.

Jamani, kabla haujafanyiwa utu hebu na wewe kuwa na utu basi......hebu tuongeze idadi ya watu wenye roho nzuri katika jamii kwa kutokuwaabuse hawa wachache ambao tunawalazimisha kufanya huruma kwa kuwablackmail kwa makusudi. Naona siku hizi abiria wameanza kuwa wagumu kujitolea kupisha siti kwenye daladala sababu wamegundua wahusika wanafanya kusudi wakijua wataonewa huruma.


Naomba tusaidiane kuelimisha jamii ili hii changamoto itoweke jamii iwe na watu responsible.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom