Kwa watumiaji wa CDMA (mobile internet)

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
ANGALIZO WATUMIAJI WA CDMA ( MOBILE INTERNET )

Kwa siku za karibuni watu kadhaa wamekuwa wakilalamika kwamba wanapojaribu kujiunga na mtandao inakaa kwa sekunde au dakika chache halafu ina jikata ( disconnect ) wengi wao wanatumia CDMA MODEM ambazo zinapatikana kwa wingi kutoka kampuni za Zantel na Zain za Jijini Dar es salaam .
Kuna vitu 2 vya kuangalia hapa , kuna ile ambayo unaweza kujiunga ( connect ) lakini huduma ya internet hupati au unajidisconnect yenyewe kama vile wewe ndio umeamua na kuna ile unajiunga lakini MODEM yenyewe ndio inajidisconnect na kuanza install upya kama vile ndio umenunua kifaa hicho kwa mara ya kwanza
Hicho cha kwanza cha modem kujiondoa katika system yako na kujiunganisha yenyewe moja kwa moja , hilo ni tatizo la modem yako , unachotakiwa ni kufika katika duka ulilonunua na kuomba ubadilishiwe kuna baadhi ya modem ziko hivyo ingawa maduka mengi huwa wanahusisha hii na virus au ubovu wa computer yenyewe hili si kweli wanatakiwa kubadilisha .
Ukipata tatizo hilo hata unapounganisha kifaa hicho na computer zingine itakuwa ina connect na disconnect itaanza kudetect hardware ( hiyo modem ) upya kwa swala hili ni la dukani uliponunua kifaa chako
Ninachoongelea mimi ni pale unapounganisha modem yako na computer , halafu unajaribu kujiunga na internet baada ya sekunde inajikata ( disconnect ) , lakini ukipeleka katika computer nyingine inaweza kufanya kazi kama haijawa infected .
…………………………………………………………
CHA KUFANYA
Unatakiwa uwe na antivirus ambayo inaweza kuscan katika Dos Mode pale tu computer inapowaka inascan kabla ya login ( kabla winlogin ) haijaanza kufanya kazi katika hizo antivirus nimetumia Avast antivirus 4.8 Profesional .
1 ) Ikiingiza Antivirus hii katika computer yako itakuuliza kama unataka kuscan computer yako wakati inaanza ( start ) unatakiwa ukubali , ila usirestart hapo .
2 ) Maliza kuinstall weka licence key zake ( licence key huwa inaingiza unapoclick – kufungua hiyo antivirus kutumia icon yake iliyoko kwenye desktop )
3 ) Update – nakushauri udownload update yake kutokea tovuti yake avast! - Download antivirus software for spyware and virus protection in ukubwa wa kama 24 mb , kwa modem za kawaida cdma utaweza kutumia pesa nyingi kidogo na kama connection yako iko chini utapata tabu kwahiyo ni bora uende katika internet café .
4 ) ukishapata update install katika computer yako kisha Restart au zima na kuwasha computer yako
UKISHAWASHA ITAANZA KUSCAN COMPUTER YAKO YOTE MAELEZO MENGINE CHA KUFANYA INAPOKAMATA VIRUS NI KUBONYESHA 1 KWA KUCLEAN AU 2 KWA DELETE ALL , 3 KWA DELETE , 4 KWA MOVE , UTASOMA MAELEZO ZAIDI .
…………………………………………………..
Wakati inascan computer yako utaona inascan sehemu kama C:/SYSTEM RESTORE hiyo ni HIDEN FOLDER ambapo virus huyo hujificha , kwahiyo huwezi kufanya system restore kwa sababu ana disable pamoja na kuweka profile nyingine wakati unapologin ndio maana unatakiwa kuiscan kabla ya kuingia katika operating system yako au kabla winlogin haijaanza kufanya kazi .
Kama wewe ni mtazamaji mzuri computer yako ikiwa na tatizo hilo angalia wakati unawasha tu inapo login katika windows juu kulia utaona kibox kinajiandika INSTALLING NEW PROFILE bila idhini yako , hiyo ndio haitakiwi .
KUMBUKA HAYA NI MAWAZO YANGU ---- NAFUNGUA MJADALA KUHUSU SUALA HILI TUNAWEZA KULIJADILI ZAIDI KAMA KUNA MASWALI NA MICHANGO ZAIDI

YONA F MARO
oldmoshi@gmail.com
BidiiForums - Karibu Tujenge Nchi - Index KARIBU TUJENGE NCHI
USIKU MWEMA
 
Ningependa kutoa mawazo tofauti kidogo kuhusiana na Modem za internet ambazo nina uzoefu nazo na kila siku nafanya troubleshooting ya data kwa kila provider wetu (Vodacom, Zain, TTCL & Zantel)
1. CDMA internet ni Zantel na TTCL ambao wako kwenye soko
2. WCDMA (3G,HSPA) internet ni Zain & Vodacom pekee
hili swala la kudesconnect nimejaribu kulifuatilia sana kwa makini nikaja kugundua kuna baadhi ya wateja wa malipo kabla (pre-paid) ndio inafikia muda inadisconnect data Downlink/uplink lakini kwenye computer yako inakuonyesha wazi upo connected lakini hufungui page yoyote lakini ukidisconnect na kuunganisha tena inafanya kazi. lakini hili sijawahi kuliona kwa watumiaji wa Post-paid hata siku moja maana nilishafanya test na Data centre wa Vodacom bila mafanikio kwenye post-paid lakini pre-paid lipo nadhani itakuwa ni issue ya Billing kwenye IN server.
Swala la kuingiza modem kwenye computer na kudai kuinstall upya kana kwamba ndio inaanza kuitambua modem, kweli kutakuwa na tatizo mojawapo katika Computer yako au Modem sababu modem zetu zote ni Plug and Play yaani kuna system configuration file ambalo linakuwa kwenye windows folder baada ya kuinstall computer, linafanya compatibility ya Installed software kwenye computer yako na ile kwenye ROM drive ya modem yako na kuiwezesha kutambua drivers za modem kama modem port na Dialup port ambapo kwa pamoja zinakuwezesha kupata access ya Internet connection. Hivyo basi endapo computer yako inakumbwa na Virus huwa wanapenda kulishambulia hili file sababu ni ni auto plug and play configuration ni rahisi sana kuonekana na virus na ndipo ukichomeka tu inakudai kufanya installation upya.
Kwa upande wa pili utakuwa kwenye modem ROM drive software (dashboard software au customer UI application software) hii huweza kupata demage endapo mteja kuwa na tabia ya kuchomoa modem yake bila kutumia njia/taratibu sahihi za kuondoa removable plug & play devices kama flashdisk (unself-removal) hupelekea ile ROM drive kufa hivyo kuna uwezekana wa files kupotena na kushindwa kulandana na yale yaliyokuwapo kwenye computer yako na kukufanya kila mara inataka kuinstall upya.


ni hayo tu kama kuna mwenye swali anakaribishwa.

KWA WATUMIAJI WA CDMA ( MOBILE INTERNET ) - Bidii - Karibu Tujenge Nchi | Google Groups
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom