kwa maneno mafupi yasiyo ya kumumunya naomba niwaulize swali watanzania wenzangu tulio na uchungu na nchi yetu je hatuoni ni wakati sasa tuanza kupigania rasilimali zetu kila kukicha kashfa za ufisadi na rushwa mwisho wa siku zinapotelea juu kwa juu sasa nafikiri ni vizuri watanzania tuanze kudai haki yetu zaidi ya kusuburi 2015 kwani tuaachiwa nchi ikiwa haina kitu haina rasilimali yoyote kwani kila kitu wamasafirisha MPAKA TWIGA!!!!!!(mnyama wa taifa, fahari ya tanzania) deni la taifa linakuwa kubwa kila kukicha je hatuoni kuwa ikifika 2015 kwa kukaa kimya kwetu tutasababisha mzigo kwa watoto wetu na vitukuu wetu, hatuoni kuwa watatuona waajabu sana kunyonywa na mkoloni mweusi na bado kila siku tunawachekea na kusimama kwenye jua kipindi cha kampeni kuwasikiliza wanavyotuambia hadithi za uongo zisizo tekelezeka WAKATI UMEFIKA BILA KUANGALIA ITIKADI YA CHAMA AU DINI WA KILA MTANZANIA KUAMKA NA KUTETEA HAKI NA RASILIMLI ZA TANZANIA BILA UOGA na mabadiliko hayo yawekatika historia ya kujikomboa kwenye ukoloni wa mtu mweusi