Kwa wasiowaelewa

Vijitabia vyenyewe kwa mfano:simu yako imeita anataka apokee yy ukimkataza anaanza kununa,msg ikiingia kwenye simu yako anataka aanze kusoma yy,Kakupigia simu labda ulikua busy ukamwambia utamtafuta badae anasusa jumla,Kakwambia mkutane umepata dharura aelewi kama kuna ki2 kingine cha muhimu kumzidi yy.

Hayo ni machache2 bt kweli yanaboa sana.Nadhani suluisho ni kumpeleka kama anavyotaka pale inapowezekana uku ukijaribu kumuelewesha kupitia kila 2kio bila kusau kumuonyesha kua haupendezwi na tabia zake.Hapo labda itapunguza

mkuu kuna swali la muhimu hapa, je hivi vitabia alikuwa navyo toka umeanza nae au vimeanza lini? una hakika hakuna jambo ulilomfanyia lililopunguza kukuamini? na kama lipo ulichukua hatua gani kurekebisha hilo na kumwonyesha umerekebisha?
kwa nn nasema hivi!! inawezekana aliwahi kufuma sms zisizo nzuri huko nyuma na ilikuwa kwa bahati mbaya na si kuwa alikuwa ana tabia ya kukagua simu yako, au inawezekana unaruhusu watu wakupigie simu usiku tena zile zisizoeleweka kwa mwenzako (hapa nazungumzia simu toka kwa wanawake).

kama hayo yote hamna, basi inawezekana ikawa huko nyuma kabla yako aliwahi kulizwa mahali na ana wasiwasi kuwa yanaweza kujirudia.. SEMA NAE USUONE SOO, mtafutie siku mtoe out, mweke chini wakati mpo kwenye mood nzuri na mwambie unavyojisikia na mwombe akuamini.. nawe onyesha kwa vitendo kuwa unathamini kukuamini kwako uone kama yatatokea
 
Back
Top Bottom