mapenzi ni safari ngumu pengine kuliko zote hasa kwa kizazi hiki. Ni vigumu kujua hatma yenu kabla ,lakini viashiria vya hatima yenu vinaweza kuonekana mapema. Mfano hebu fikiria una rafiki yako au niseme mtu unayetaka kuanzisha naye mahusiano,halafu inatokea anasafiri kwenda mji mwingine lakin kabla hajafika huko aendako, ni lazima apite mahali wewe upo. Rafiki yako huyo hasemi hadi anafika na unampompigia anakwambia ilikuwa ni dharula na ndo mana sikukwambia na wakati wa kurudi anapita kimya ukimuuliza atakwambia nilikuwa na haraka na mambo mengine kama hayo. Au una mahusiano na mtu anakwambia ninataka mtaji angalau kiasi fulani, kisha una mpa baada ya hapo anakuwa kimyaa,hadi umuulize je unaendeleaje na mradi wako? Anaanza kukwambia unajua nilikuwa sina hela ya kula, mara nikaenda kijijin kusalimia kwa hiyo ile hela nimetumia,na wakati huo unajua kabisa anafanya kazi japo si ya kipato kikubwa kama chako. Hivi ni viashiria tu kuwa hamuwezi kufika mbali.
yaani mtongozane leo leo ,mkubaliane leo leo na siku ya ndoa itangazwe leo leo?
Umenichekesha..teh! kwa hiyo kama sio mahusiano inaitwaje?kuna ile unatoka na mtu, ukikumbuka mlivyoanza mapenzi yenu hakuna aliemtongoza mwezie, mkajikuta tu mpo wapenzi, mara miezi na miaka ikapita, mnaendelea kibubu tu, hata hujui mnakoelekea ni wapi, ukaamua kujikaza na kuuliza hivi huu uhusiano wetu unaelekea wapi? mara jamaa anakujibu hatupo kwenye mahusiano,
tumia akili.hapana smile naamaanisha yaani kama upo kwenye mahusiano na mtu, basi ujue mwisho wake labda mi kula gud time tu na kusepa, au ndo mungu akibariki awe mume/mke, yaani ieleweke tangu mwanzo kwa nini mpo pamoja, kuepusha kuaumiana, unaweza shangazwa baadae umewekeza akili na moyo wako wote kumbe mwenzio hana mpango na wewe kabisa
usemee moyo wako, lol!Hamna penzi jipya wala nini, wote tumetumika sana tu, yaani maskrepa, pia tumeumizwa sana mioyo, na pia tumewaumiza wenzetu.
Mapenzi yamefulia mioyoni mwetu
kuna ile unatoka na mtu, ukikumbuka mlivyoanza mapenzi yenu hakuna aliemtongoza mwezie, mkajikuta tu mpo wapenzi, mara miezi na miaka ikapita, mnaendelea kibubu tu, hata hujui mnakoelekea ni wapi, ukaamua kujikaza na kuuliza hivi huu uhusiano wetu unaelekea wapi? mara jamaa anakujibu hatupo kwenye mahusiano,