Kwa Wapendanao

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
219
Mpenzi

Habari za huko ulipo ?

Najua wewe ni mzima sana , maisha yako ni mazuri tu , hata kama yanautata kidogo nafikiri unajitahidi kuyafanya yawe mazuri zaidi na kama yanatetereka naamini unajaribu kuyanyoosha yawe katika msitari katika siku zijazo .

Ni matumaini yangu kwamba pia moyo wako unaendelea vizuri , honey si unajua mioyo yetu imeungana kwa sasa ? bila moyo wako mimi sina kitu , sina mali sina chochote , bila ya kupata chochote toka kwako mimi sio mimi sina maisha sina changu .

Nimetembea mitaani na kuona maduka mengi yana kadi za salamu , mengine mauwa mengine zawadi mbali mbali na vitu vingine vya rangi nyekundu nikajiuliza ni nini vile wakati christmass imeshapita , ingekuwa kwa wachina basi ningesema ni mwaka mpya wa kichina .

Nilipojaribu kudodosa nikatambua kwamba ni siku ya wapendanao ambayo ni siku ya 14 mwezi wa 2 katika kila mwaka , hata sijui historia yake imeanzia wapi , na hata walioanzisha walifikiria nini au walikuwa na malengo gani mimi sijui hivyo .

Lakini kwanini watu wanachagua siku maalumu kwa ajili ya kuonyesha hisia zao za kimapenzi , kupendana au kuonyesha mahusiano yao ? hivi kuna ubaya gani kumwonyesha mpenzi wako kwamba kila siku ni siku nzuri , ni siku ya kumpenda zaidi ni siku ya kushirikiana nae zaidi ?

Sherehe hii vijana ndio haswa wanaosheherekea na wengi wao huishia pabaya katika ugomvi kugombana na mambo mengine ambayo sio ishara nzuri mbele ya jamii ya walimwengu wastaarabu lazima tuyakemee .

Niliwahi kuwa na rafiki yangu Fulani , mwaka jana alipania sana siku ya valentine kumwonyesha mapenzi moto moto mpenzi wake , basi siku hiyo ilivyofika , ilikuwa ni siku ya kazi , muda ukaenda mpenzi wake anamsubiri hatokei jamaa amebanwa kazini , saa 2 imefika jamaa bado hajatoka kazini , mpaka saa 3 jamaa hajamaliza kazi ya watu .

Kule katika ahadi mwanamke amechanganyikiwa anafikiri kidume chake kiko na mtoto mwingine , yule jamaa akachelewa sana kwenda kwa mwanamke wake alifika katika saa 5 hivi za usiku wakati watu wameshamaliza hii sherehe wengi wako majumbani vitandani na mambo kam ahayo .

Kwahiyo uhusiano wao uliishia hapo hapo , yule rafiki yangu alivyogonga mlango wa yule dada akarushiwa vitu vyake nje , akaambiwa amechelewa arudi huko alipokuwa kwa saa zote hizo .

Rafiki yangu akajaribu kujitetea kwamba alikuwa kazini ilimlazimu kumalizia kazi husika lakini alikuwa ameshachelewa sana , kuelezea mkasa mzima siku nzima alikuwa wapi kwanini hakusema kwamba atachelewa ?

Huo ni mfano halisi wa kuandaa siku maalumu kwa ajili ya kuonyesha mapenzi , unaweza kuchelewa katika ahadi ikawa kasheshe katika maisha yako ya mapenzi na mahusiano ikakuumiza wewe na wengine wengi tu .

Ukiangalia kwa makini utaona siku ya wapendanao rangi nyekundu ndio alama kuu ya kuonyesha kile kinachoendelea , ukiwa barabarani taa nyekundu ikiwaka maana yake simama au punguza mwendo kuna jambo linaloendelea .

Rangi nyekundu pia ni alama ya hatari , lazima tuangalie pande zote mbili kwa nini waanzilishi wametumia rangi hii , au kwa sababu moyo unarangi hii ? lakini hii ni rangi ya hatari

Unaweza kufukiri labda ni rangi ya uwa waridi , lakini uwa waridi hukua kisha hufa , je unapenda mapenzi yako nayo yawe hivi hivi ? yakuwe yawe na rangi nzuri kisha yaanze kunyauka kidogo kidogo mpaka kifo ?

Sasa kwanini uandae siku maalumu ya kuonyesha mapenzi yako kwa Fulani na isiwe kila siku ni siku ya mapenzi moto moto kwa mpenzi wako ? ukiahidi usipotokea kama rafiki yangu hapo juu itakuwaje ?

Mimi ni mtu ambaye sipendi kuongelea masuala yangu ya mahusiano mapenzi na vitu kama hivyo lakini naamini nimefanya yale ya msingi kuhakikisha yule wangu wa karibu anakaa kwa amani , raha , starehe na kufurahia maisha yake akiwa na mimi .

Hata kama nikiwa mbali nae , sina wasi wasi najua kuna vitu vinavyotuweka karibu , na kukumbushana kuhusu ahadi yetu ya kupendana , kuthaminiana , kuaminiana na kuombeana amani wakati wote wa maisha yetu .

Na leo naishia hapa , nakukumbushia mapenzi yako hewani hewa iko sehemu zote za dunia hii , kwahiyo mapenzi ni popote , wakati wowote , katika eneo lolote ili mradi usivunje miiko na maadili ya sehemu husika kwa sabababu jamii zingine zina maadili tofauti na wewe hii ndio tofauti yetu .

Kuna nyimbo moja inaitwa MY LOVE imeimbwa na Julio Iglesius & Steve wonder kuna msitari unasema KAMA MTU AKIKUULIZA NANI MPENZI WAKO , MWAMBIE NAKUPENDA , WACHA UPENDO UTAWALE DUNIA NZIMA JUU YA MLIMA HATA VILIMA , MITO NA BAHARI .

Lakini huyu Steve Wonder ameimba nyimbo nyingine inayoitwa PART TIME LOVER , katika dunia ya sasa jitahidi usiwe au usijaribu kuwa part time kwa sababu dunia imekuwa karibu zaidi kuna vitu vinaunganisha watu kama simu , tovuti na kadhalika .

Ni rahisi wewe kujulikana na kusambaziwa uchafu wako kwa njia ya mtandao na hata kuwekwa picha zako na taarifa zako zengine ukicheleza akili za watu kwahiyo siku zote jua hata ukuta utasikia

Uwe mwaminifu kwako na kwa mpenzi wako , jaribu kuwa karibu na mpenzi wako mimi huwa nasema TRY TO KEEP YOUR MAN watu wengi hawana hili desturi ya ku KEEP THEIR MEN , wengi ni PART TIME LOVERS

Kwanini usiwe , NOW THAT LOVE IS ON OURSIDE AGAIN , LET THIS FEELING FLY AWAY .
 
hizi ndio thread za wakogwe wa JF eti wanaojivuna walikuwa bora zaidi katika kuleta thread kuliko tunavyoleta leo.
 
Back
Top Bottom