yamoyoni mwangu
Senior Member
- Oct 25, 2013
- 106
- 31
Habari zenu enyi pambo la ndani kama watu wawaitavyo...!
Awali ya yote niwape hongera nyingi kwa kufanikiwa kupata jiko, famlia huku wengine mkiwa na watoto, wenye afya na amani tele. maana sikuhizi kuolewa sio kazi bali kazi ni kupata aliyekuoa anayejua nini maana ya mke, kukutunza,kukuthamini,kukujali,nakujua nafas yako katika famlia kama mama.?
Sasa ewe mke mwema ,uliwahi kujiuliza ni kwanini mmeo anachelewa sana kurudi nyumbani siku hizi tofauti na kipindi cha hapa awali? au kwanini mmeo hakujali hakuiti dear ,honey, na majina mengine kama hayo? nadhani kuna wengine huwanga mnafikiria kwenda kwa waganga au kufunga kwa ajili ya mmeo, ni sawa sikatai lakini kubali au kataa moja kati makosa haya umeyafya,na unaendelea kuyafanya bila kujua.
1:kununa pasipo sababu ya msingi.
Wanawake wengi wanatabia ya kununa pasipo sababu ya msingi, leo nataka nikuambie kuwa si wote uwaonao wanafurahia ndoa yako, wapo wengine wanapenda ukwaruzane na mmeo na hatimaye kuachana kabisa ili pengine nafas uliyonayo wewe waipate wao au wakuone unavyotapata nakuranda randa ovyo. unapo sikia maneno juu ya mmeo et anatembea na fulan, yachunguze kwa kina,usipaniki kuwa mpole ,endapo itauwa kweli, tafuta namna nzuri ya kumwambia mmeo, wanawake wengi wanakoseaga sana pale wanapoanza kuwagombeza kwana kutoa lugha chafu kama hii(ashakum si matusi) MALAYA WEWE NA UTANIAMBIA HUYO MALAYA WAKO, RUDI HUKOHUKO KWA HUYO MALAYA WAKO AKAKUPIKIE, AKUFULIE NGUO NA UKUPE MAJI YA KUOGA, MSHENZI MKUBWA..! kwa namna kama hii na nyinginezo lazima mwanaume akufundishe adabu atakutwagwa makofi,mateke na magumi bure, au atafanya kama ulivyo mwambia kurudi aliko toka. mwambie taratibu kwa upole tena mkiwa chumbani wawili tu, msifaidishe majirani mweleze madhara ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi nje ya ndoa yake. mtolee mifano hai mchache ambayo umewahi kuiona kutokana na suala hilo, akionekana kutoelewa muache usimulazimishe akuelewe mda huohuo, ataelewa tuu, jitahidi kutumia hisia zaidi , siri kubwa ya mwaume anapenda kunyenyekewa na kubembelezwa.
2:kutokumjali mmeo..
Wanawake wengi hawana ubunifu kwa waume wao, mfano,mwanaume anapotoka kwenye mzunguko ya ke anahitaji kupokelewa, kupozwa kwa maneno matamu hata kusikilizwa shida zake, mfano wanawake wengi wamewaachia ma house girl kufanya kazi zao, utakuta mwanamke anafuma kitambaa, huku akisogoa na mashost zake huku mumewe akiwa ndani mwenyewe, hili ni kosa kubwa, jitahidi kubuni mtindo mbalimbali kwa mmeo,ili akuone mpya kila siku.
3:kutokuwa mtii.
baadhi yenu mmekosa utii kwa waume zenu, mfanmo mmeo amekukataza tabia ya kutoa vitu pasipo kumshirikisha, amewakataa mashoga zako kwa kutoa sababu zinazo eleweka kabisa mfano, wao hawajaolewa, hawana kazi maalumu wambea, kukicha tu wao ni kusutana hata mabarabarani, pengine mmeo hapendi baadhi ya nguo unazo vaa na alikwisha kukuambia, labda hapendi unavyo paka wanja, inna, ama hapendi kabisa mkewe aweke makorokoro kichwani hasa wigi, hapendi mkewe awe anaazima vitu ovyo kwa majirani hata kama si vya lazima, na mengine mengi nadhani we mwenyewe unajua juu ya mumeo na itikadi zake. sasa baadhi yenu mna vichwa vigumu, hamsikiagi hata akuambie vipi.. uamuzi ataouchukua ni kuanzisha mahusiano sehemu nyingine ambako wanamsikliza anaposema kitu chenye manufaa kama baba. yawezekana keli akawa na mapungufu yake lakini mshauri sio kutumia kiburi, utaendelea kujiuliza et unamkosi gani shauri yakoo..
HILI NI DARASA HURU NAOMBA NIISHIE HAPO... kuna wadada na wakaka wataisoma hii thread wakati haiwahusu daa uliyo yaona yaache humu humu, zipo sababu nyingine kibao nadhani kwa leo hizi zinatoshaaaa............!