Kwa wanaume wa ukweli!!

Kwa wanaume wa ukweli!!

Joined
Jan 3, 2017
Posts
14
Reaction score
21
KWA WANAUME WA UKWELI

Ni neno rahisi Lakini Muhimu Ambalo Mwanamke Anahitaji Kusikia Kila Siku kutoka kwa mume au mpenzi wake.

NAKUPENDA

Kupendwa ni mojawapo ya vitu ambavyo binadamu anahitaji sana. Chukulia mtoto mfano,toka tukiwa watoto kupendwa ni kitu kinachohitajika sana na kinapokosekana kuna madhara makubwa yanayotokea ikiwemo mtoto kutojipenda mwenyewe na kutojiona wa thamani. Kwa wanawake halikadharika,japo ni wakubwa tayari
1f602.png
1f602.png
1f602.png
1f602.png
lakini kasumba ya utotoni imo bado ndani yao na mahitaji ni yaleyale.

Ukiangalia vizuri mahangaiko yote ya mwanamke juu ya urembo na mavazi utaona kuwa ni kutaka kuhakikisha kuwa anapendwa. Au kujinyima na kuishi katika mwenendo ambao wewe kama mume unafikiri ni vizuri au jamii inafikiri ni vizuri ni kutaka kuhakikisha kuwa anapendwa. Basi kwa kumtamkia kuwa unampenda mara nyingi kadili utakavyoweza inampa kujiamini kwa jinsi alivyo na kwa yale anayoyafanya.

Kumwambia mkeo kuwa unampenda na kuonyesha kwa matendo kunamfanya naye akupende zaidi.

Neno hili likitumika kwa dhati na sio kusema tu, lina maajabu makubwa katika kuboresha mahusiano ya wenza wapendanao, Wanaume mliooa na ambao mpo katika mahusiano,Hebu weka mazoea ya kumtamkia mwenza wako neno NAKUPENDA ,maana kuna wanaume wengine tangu walipotamka siku ya Harusi mpaka leo hii
1f61b.png
1f61b.png
1f61b.png


Mwanaume wa Ukweli Mpende mkeo!!
 

Attachments

  • 18301365_1891188421169081_5775439234695225150_n.jpg
    18301365_1891188421169081_5775439234695225150_n.jpg
    64.1 KB · Views: 37
Ukishampenda? Ndio unakua tajiri au. Masikini wanaweza kupenda, tajiri wanaweza kupenda, ombaomba wanaweza kupenda pia n.k. weka bidii kwenye kufanya vitu tofauti kwenye maisha ambavyo ni ngumu kama kuwa na hela nyingi, kwenda sayari nyingine na kugundua vitu vipya. Sijaona mtu aliyefariki ikasomwa risala kuwa eti alikua anampenda mke wake saanaa.
 
Omba Mods wapeleke huu uzi kwenye lile jukwaa lenu, humu Weng wanajipenda wenyewe hawahtaj kupendwa
 
Wanasema duniani kila mwaka 25% ya wanawake wanao kufa .wanakufa kwa kukosa upendo.
 
sawa mkuu, wengine hio ndio salamu yetu ya kila siku
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom