Civilian Coin
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 2,305
- 4,379
Ndugu wana Jamii forum na wote wapenda Ukweli, pokeeni hii hasa kwa Wanasiasa.
FURSA YA MSAMAHA & UPENDO.
Mathayo 5:43-46.
Nachukua fursa hii kuomba msamaha kwa wale wote ambao kwa namna moja au nyingine tumekwazana kwa miaka mingii na kwa wale wote ambao nimewakwaza kwa maneno yangu makali katika makala zangu mitandaoni na hata katika mawasiliano mabovu.
Ikumbukwe kuwa msamaha sio sheria, kukusamehe kama rafiki au ndugu au mpenzi sio kwamba ndio nitakuamini, Bali msamaha wangu ni ishara ya kuonesha kiasi gani ninaweza kujali na kumpenda adui wa karibu, na kama ni kumsamehe mpenzi wangu basi Mimi nimeshasamehe lakini sitaweza kumrudia, maana msamaha wangu ni ishara ya Upendo na Utu. Kuonesha upendo ni hulka na kusamehe ni silka.
Pia natumia nafasi hii kwa Wanasiasa mbalimbali wa Taifa letu kuwaomba msamaha pale nilipowakosea, Upendo wangu ni thamani ya kukiri mapungufu yangu.
Nawatakia siku njema ya Wapendanao,
Ndimi:
Deogratius Nalimi Kisandu.
Mwanza-Tanzania.