kiraremapojoni
JF-Expert Member
- Nov 30, 2018
- 391
- 514
Napenda kuwapa darasa ndugu zangu ambao wanatarajia kufunga ndoa hivi karibuni au mwakani nila kuangalia kama unaoa au unaolewa. Ndoa ni jambo zuri sana na hasa likiwa lina baraka za wazee wa pande zote mbili na hili linafanikiwa zaidi endapo mnaanza utaratibu wa kuoana mkiwa bado nyumbani kwa wazee wenu( hili lisiwatishe sana kutokana na mabadiliko ya tabia mwili kwa vijana wa kileo)
Ndoa ni ufunguo wa riziki. Wapenzi wawili mnapoamua kufunga ndoa kwa minajili ya Mwenyezi Mungu basimilango ya riziki mwenu inakuwa iko wazi kwa kila jambo ambalo mnapanga linakuwa na wepesi na mafanikio yanakuwa mazuri. Msiogope kuoa kwa vile maisha ni magumu kwani kumbukeni hata mbuyu ulianza kama mchicha na mwisho wa siku ndo ukaawa mbuyu.
Ndoa ina unganisha koo mbili tofauti. Vijana mnapoanza maisha kama mke na mume basi una koo mbili tofauti ambazo zimeunganika na kuleta ujamaa na undugu kwa familia hizi. wahenga wanasema mbegu ikwa haba unaongeza mchanga kwani mkishaunganizha koo mbili tayari koo zinakuwa zimeshakuwa kubwa.
Vijana wa kileo tuache kuishi na wanawake ambao hatujawaoa kwani inapotokea changamoto inakuwa ni shida kidogo kupambanua kwani haileti picha pale unapopeleka kesi kwa baba mkwe wakati hakutambui kifamilia na akiwa mkorofi ndo anazidi kukuponda na kukuletea madharau ya kishua.