Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,998
Jana Jumamosi habari zilianza kuenea katika maeneo mbalimbali nyumbani hasi miongoni mwa vigogo kuwa Balali amefariki. Simu zikapigwa na sisi wengine ambao tunaelewa hali ya mgonjwa tukashtushwa. Labda ni kweli mnataka afe ili aende kwa muumba na siri zenu. Bahati mbaya mpango huo hadi hivi sasa ahera madukani wameuharisha na akirudisha namba yake itakuwa ni kwa kibali cha Aliye Juu. Sasa acheni kumchuria msije mkalazimisha kutimiza unabii wenu wenyewe. Kule kwetu huo unaitwa uchuro! Nawashauri mtangulie nyinyi kwanza lakini baada ya kusema siri zenu! Na mtake msitake atarudi nyumbani na kama kuna mashtaka yoyote ambayo mko tayari kuyaandaa mjue kabisa hatasimama kizimbani peke yake! Mmelikoroga wenyewe, sasa mtalinywa! Tuliwaambia mkatuona siye tuna wivu..
Balali ni nani?
Balali ni nani?
Wewe Mwanakijiji badala ya kusheherekea heppi besideyi, unachimbua rumours. lol.
Heppi Besideyi.
Kwa kifupi Balali hayuko mahututi na ameshatoka hospitali na anaendelea na matibabu vizuri na mazoezi ya viungo at "undisclosed location". Amepoteza uzito sana na bado anakula kwa msaada lakini hali yake ni bora kuliko wiki tatu zilizopita. Kupata kwake nafuu siyo habari njema kwa makumi ya watu.
Gavana wa Benki kuu Tanzania[/QUOT
Honestly speaking!! Was this a seriouse question???
...kumbe kuna bethidei ya kusheherekea..haya Hapi Bethidei Mwanakijiji.
Honestly speaking!! Was this a seriouse question???[/B]
Gavana wa Benki kuu Tanzania[/QUOT
Honestly speaking!! Was this a seriouse question???
Mimi sioni sababu ya kumshumbulia huyu maaana kuna watanzania waliozaliwa nje sasa wanataka kujua maswala ya home.
Pili sio watanzania tu wanaongea kiswahili inawezekana Mkenya, Ruandees, Congo,Ethiopia Somalia, Zambia na hata wapo wazungu wengi tu wanazangumza hii lugha so mtu anapouliza swali si just mpe jibu then endelea na mada unless liwe ni halina maana yeyote.
Mfano leo kuna mtu kauliza "Kumkoma nyani Giladi" maan yake nini mtu kauliza hakujibiwa. wakati mwingine tutapoteza watu kwa sababu wanahisi hawathaminiwi pale wanapoomba clarification
Mkuu kama hujali sana, hebu tuweke sawa kuhusiana na ugonjwa wake, yaani kwanza ni nini anaumwa, alianza lini, na wapi, na kama ana mpango wa kurudi bongo, maana kwa maelezo yako asiporudi nitaelewa ni kwa nini hatarudi, maana hii ishu yake inaaanza kuelekea kuwa sawa na ya Marehemu Waziri Kibona!