Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,398
- 39,547
Jana Jumamosi habari zilianza kuenea katika maeneo mbalimbali nyumbani hasi miongoni mwa vigogo kuwa Balali amefariki. Simu zikapigwa na sisi wengine ambao tunaelewa hali ya mgonjwa tukashtushwa. Labda ni kweli mnataka afe ili aende kwa muumba na siri zenu. Bahati mbaya mpango huo hadi hivi sasa ahera madukani wameuharisha na akirudisha namba yake itakuwa ni kwa kibali cha Aliye Juu. Sasa acheni kumchuria msije mkalazimisha kutimiza unabii wenu wenyewe. Kule kwetu huo unaitwa uchuro! Nawashauri mtangulie nyinyi kwanza lakini baada ya kusema siri zenu! Na mtake msitake atarudi nyumbani na kama kuna mashtaka yoyote ambayo mko tayari kuyaandaa mjue kabisa hatasimama kizimbani peke yake! Mmelikoroga wenyewe, sasa mtalinywa! Tuliwaambia mkatuona siye tuna wivu..