Kwa walimu wazoefu wa uhamisho

beneli

Member
May 1, 2013
86
7
Habari zenu wanajukwaa, naomba msaada kwa walimu ama mtu yeyote mwenye uelewa, kuna kijana alimaliza form two miaka mitatu iliyopita na matatizo ya kifamilia yakamfanya ashindwe kuendelea na shule.

Kwa kuwa alikua anasoma shule ya serikali iliyokua mbali na nyumbani gharama zilimzidi na hasa baada ya kufiwa na mzazi wake , kuweza kujikimu kukashindikana kupelekea kuacha shule pasi ya kumaliza kidato cha nne.

Je , kuna uwezekano wa yeye kuhamia shule ya serikali iliyokaribu na kuendelea na kidato cha tatu kwa kutumia matokeo yake ya form two.

Natanguliza shukrani zangu kwa msaada wenu.
 
Andika barua kwenda kwa afisa elimu mkoa ya kuomba huyo kijana akariri kidato maana afisa elimu mkoa ndo mwenye mamlaka ya kutoa kibali cha kukariri kidato cha kwanza hadi cha tatu,ndani ya barua elezea sababu zilizomfanya ashindwe kuendelea na shule wakati alipoacha.
 
Back
Top Bottom