Utotoni tulikuwa na kamchezo ka kuwinda vicheche.Vitendea kazi vilikuwa mbwa,rungu na vibuyu vya maji.Mara kwa mara zoezi hili tulikuwa tukilifanya pale kuku wetu walipokuwa wanashambuliwa na vinyama hivi.Tulipokuwa tunaondoka kwenda mawindoni kila mmoja lengo lilikuwa kuwatokomeza kabisa vicheche wala kuku wetu.Msako ukianza mashimo yote tuliyoyafahamu tuliyahakiki.Tukifika kwenye shimo tunalolitilia shaka,tulikuwa tunalizingira na mbwa wetu kisha tulikuwa tunamimina maji ya kutosha,halafu tunajipanga kando kidogo.Kama wamo humo ndani lazima watoke na wakifika nje iliwalazimu wajikung'ute maji kwanza.Kitendo bila kuchelewa rungu zilitumika kwa usahihi ,wale walionusurika na rungu,chisese aka mbwa walimalizia.Kwa utaratibu huu tulifanikiwa kufuga kuku kwa amani.MWENYE KUELEWA na AELEWE!