kethika
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 630
- 472
Mimi ni mmoja wa watu waonyolea nywele saloon za kiume ila nakerwa na yafuatayo kwenye saloon hizo
1. Kuulizwa kila siku ninayoenda kunyoa kama nataka scrub. Ingekuwa ni mara ya kwanza au ya pili hata ya tatu na ya nne isingekuwa taabu. Mtu unaenda saloon hiyo hiyo mara hata ishirini na hujawahi ku scrub tena unawaeleza kwanini hutaki hiyo scrub lakini hawaishi kukuuliza utadhani ndio masharti waliyopewa na mganga wao. Isitoshe ukikataa wanakasirika.
2. Kusiginwa na matiti ya hao wasichana wanaokuosha. Kifupi niliamua nisiwe nakubali kuoshwa. Ila pia ukifanya hivyo wananuna na baadae wanaungana na hao wakaka wanaonyoa . Unajua sio wote tuoweza kueleza kuwa hatutaki kusiginwa na hayo matiti. Ila inakera. Isitoshe mtu anakuona kabisa kuwa umeoa lakina atafanya hivyo hata mbele ya mkeo uliyeenda nae saloon.
3. Vile vitaulo vya kukuoshea. Mm. Jamani msikasirike wengine tukikataa kuoshwa maana. Kitaulo kitaulo ??????. Mngekuwa mnavichemsha basi.
4. Hizo apron unazofunikwa wakati unanyolewa. Ni bandika bandua. Kama saloon ingekuwa mpya tungesema mtaji mdogo. Saloon ina miaka na miaka hujaweza kununua hata vifaa vya usafi? Apron hiyo hiyo ?????.
5. Hili tu ni swali najiulizaga. Hivi wale wadada wanaoosha watu na kuwafanyia scrub bila kuvaa vitu vya kuwalinda sio hatari kwa afya zao na za wale wanaowahudumia?
Njooni wengine na kero zenu hapa tuwaelimishe hawa ndugu maana yawezekana hawajui na wengi wao wamo humu.