Kwa wale msiotumia pombe. Mnatumia kinywaji gani kupooza makoo yenu?

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,701
9,779
Tokea mke wangu aniende kwa mtaalamu pasi na mimi kujua, pombe imenikataa kabisa

Niliamua kutafuta mbadala ya pombe. Nilijaribu soda, juisi za viwandani hadi juisi za kienyeji. Zote ziligonga ukuta

Nowdays ninaporejea nyumbani, napitia energy drink moja, ndani tayari nina kipakiti changu cha Panadol za Kenya. Kabla ya msosi natupia vidonge viwili kwenye chupa ya kinywaji changu cha energy, nangoja dk2, kisha nakunywa taratiibu huku namtazama shemeji yenu kwa hamu

Muda huo chumba kizima nimefungulia boringo za akina Iyondo Sister au midundo ya akina Msondo Ngoma. Stimu ninayoipata ni kama ya mnywaji wa bia

Kwenu msiotumia bia, unatumia kinywaji kipi kama kiburudisho?
images.jpg
stock-photo-yogyakarta-indonesia-august-panadol-known-as-paracetamol-medicine-tablets-to-cure-...jpg
 
Back
Top Bottom