Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,814
- 34,195
Jamani huyo ni madudu anayekaa kwenye mboga za majani na huyo mtoto alikula mboga za majani na huyo mdudu alikuwa kwenye mboga na hafi kwa kupikwa.
Unashauriwa kuosha mboga za majani kwa chumvi na maji ya uvuguvugu maana ni mdogo anaganda kwenye mboga kama konokono na anaumbo dogo ila akiingia tumboni anakuwa haraka kwa sababu ya joto la tumboni.
Huyo mtoto alivimba tumbo baada ya kumla na amefanyiwa operation ila amefariki.
tuwe makini na mboga za majani hasa za kula kwa mamantilie na nyumbani tuzioshe vizuri mboga moja moja pekenyua vizuri ni hatari sana jamani.