kwa wajuzi wa mambo....

bomouwa

JF-Expert Member
Jun 19, 2014
1,149
798
habari wanajamvi?
Nimekua nikijiuliza hivi ni nini hasa linasababisha mashirika mengi ya umma kukosa bodi kwa muda mrefu?
Kwa mfano tangu mwaka 2012 Chuo cha usimamizi na uhifadhi wa wanyamapori kilichopo mjini moshi bodi yake iliisha muda wake na tangu muda huo mpka sasa chuo kinaendeshwa na menejimenti ya chuo yaani mkuu wa chuo na maafisa waandamizi wengine.. Sasa najiuliza tu ni kipi hasa kinasababisha swala la uteuzi wa bodi mpya kuchelewa? Hili linaaenda sawiya na jambo la baadhi ya taasisi nyingi za serikali na mashirika ya umma kua chini ya ya makaimu wa nyadhifa za juu hata kufikia kipindi cha zaidi ya miaka mitano na unakuta utendaji ni mzuri lakini baadae unakuta anakuja kupewa mtu ofisi rasmi kama mteule wa rais wakati mtu aliekua amekaimishwa kwa muda mrefu ameendesha taasisi au sehemu husika kwa weledi wa hali ya juu..
je, ni tatizo la kimfumo?
je, ni ubize wa kimamlaka ambao husahau mahitaji ya taasisi zake?
je, ni katika kuendeleza mianya ya kizalimu na upigaji?
Nayasema haya maana nimekosa majibu kabisa tafadhali hebu mnijuze wataalamu.
nawasilisha.
 
Back
Top Bottom