Mwendabure
JF-Expert Member
- Mar 10, 2011
- 2,138
- 1,040
wataalam wa South Africa wamefeli, je wa JF wataweza?Ngoja tusubiri wataalamu waje wajibu.
Habari Wakuu!
Ni hivi karibuni serekali yetu imekiri kwamba wazamiaji wa kukodi kutoka Afrika Kusini wameshindwa kuifikia Meli iliyozama baharini na kusababisha vifo vya ndg zetu huko Zanzibar. Mimi binafsi kwa uelewa wangu mdogo kuhusu masuala ya bahari ningependa kueleweshwa vema haya yafuatayo.
1. Ni umbali (kina) gani unaweza kufikika kiurahisi na kwa kutumia vifaa gani?
2. Kuna tofauti gani ya hali ya bahari kati ya kina kidogo na kina kirefu?
3. Nimekuwa mara nyingi nikiona ktk sinema au hata baadhi ya vipindi vya TV wazamiaji au watafiti na wapiga picha za bahari wakifika hadi ktk sakafu ya bahari kwa kutumia vifaa kama vile mitungi ya gesi huwa wanaweza kufikia kina gani cha bahari kwa vifaa kama hivyo?
Natumaini nimeeleweka vema na nitapata majibu murua kwa faida yangu na wengine pia. Binafsi naamini hadi sasa serikali yetu haina mpango wa kutoa elimu au ufafanuzi wa kutosha hasa kwa Mtanzania wa kiwango cha uelewa kama wangu kuhusu kinachoendelea juu ya sakata hili na hatma ya miili ya wapendwa wetu waliopotelea baharini.
Nawasilisha!
Ha ha ha ha!!!!wataalam wa South Africa wamefeli, je wa JF wataweza?

Kwa hali ya kawaida binadamu anaweza kwenda chini ya bahari si zaidi ya mita 50 ingawa kuna ambao wanaweza kwenda hadi mita 60 -80 kwa kutumia Self-Contained Underwater breathing apparatus (SCUBA) yaani ni ile mitungi ya gesi na vifaa vingine vitakavyomfanya apumue chini ya bahari. Kadri unavyoenda chini ya bahari hewa ya oksijeni inapungua na mkandamizo (pressure) inaongezeka na ndio maana hata wakati wa diving ushauriwi kwenda haraka haraka, unahitaji kwenda step by step.
Wale unaowaona kwenye sakafu ya bahari wanakuwa eneo ambalo haliwezi zidi mita 50 na mara nyingi ni kwenye corals (matumbawe) ambayo yanakuwa kwenye maji ya pwani na ndio maana unayaona yale maji ni meupe maana yapo kwenye kina kifupi (sometimes less than 30 meters) ambapo mwanga wa jua unafikia yale matumbawe na hewa (oksijeni) inakuwepo ya kutosha.
Ilipozama ile meli ni kwenye mkondo (yaani kunakuwa na surface water na wakati huo huo chini yake kunakuwa na kama mto wa maji yaendayo kasi) na kina chake mara nyingi ni kirefu kutegemea na ukubwa wa mkondo na kwa pale Nungwi wamekadiria karibu mita 300. Hivyo kwenye kina hicho maji ni meusi (huwezi ona chochote), ya baridi sana, pressure ni kubwa na hakuna hewa ya oksijeni. Hivyo kwa kutumia SCUBA hakuna mtu atakayeweza kwenda kwani utapasua kila kitu kutokana na mgandamizo (pressure) na huwezi ona chochote. Unaweza kufika pale labda kwa zile mashine maalum kama robot ambazo pia mtu inabidi afungiwe ndani yake (haruhusiwi kutoka ndani ya hicho kijichumba) kwa hiyo kwa hali hiyo huwezi fanya chochote maana unakuwa confined.
Waokoaji wa South Africa walijaribu walivyoweza kwa kutumia vifaa vyao vya kitaalamu vya kuzamia. Kutokana na hali halisi ya kina kirefu na hali mbaya ya hewa ukitilia maanani ule ni mkondo mkali sana walishindwa kuifikia meli. Na kama ndivyo basi tayari wote walionaswa ndani ya meli walikuwa wameshakufa maji. Ama kwa majibu ya maswali uliouliza ni kwamba:-
1. Kwa kutumia chupa za hewa unaweza kucheza kati ya mita 20 hadi 35 kwa mjuzi. Kila chupa moja hewa humalizika kati ya dakika 30 hadi 45 kulingana na mtumiaji.
2. Tofauti ya kina kidogo na kirefu ni kuwa kila unapozidi kwenda chini hewa inaisha kwa maana ya kwamba kunakuwa na compression kali sana na kupona ni miujiza ya Mungu.
3. Zile movie unazoziona za madivers na samaki sio za kina kirefu zaidi hazipitishi mita 20.
Natumai nimetoa majibu
kwa ufupi ila ndio hali halisi na wengine watachangia.
Lakini ningependa kujua kile kina kina mita ngapi? Maana south afrika wana rekodi ya kufikia 927 feet (283 m) na
826 feet (252 m) mwaka 1994! Source Deep diving - Wikipedia, the free encyclopedia
asante kwa kunipa hiyo data. Ni kweli kazi ya uokoaji hapo haiwezekani tena. Labda kutoa hiyo meli tu.Pale wamakadiria kuwa na kina karibu mita 300, na sio kama hakufikiki. Kunaweza fikika lakini ni kwa kutumia Nyambizi (submarine) ambayo itachukua muda na hivyo kwa uokozi ni kama vile haina maana. Maana mtu mpaka afikie chini kina hicho (wale walioko kwenye meli) ni alishakufa muda mwingi tu. Ndio maana jamaa wakasema labda ije Nyambizi kwa ajili ya kuitoa tu ile meli baadae lakini kwa uokozi haina maana yeyote.
SIDE B: kila pahala penye mkondo wa bahari huwa na maji yenye virutubisho vingi hivo huwa na biodiverisity kubwa ukilinganisha na maeneo ya bahari ya kawaida. Mkondo bahari wa nungwi unasamaki wengi na waina mbalimbali ambao hawapatikani ktk maeneo mengine duniani: NEED TO FEED THEM FOR SUSTAINABILITY...................................
<br /><font color="#800080"><font size="4"><span style="font-family: comic sans ms">oohhh......</span></font></font>
slow downSIDE B: kila pahala penye mkondo wa bahari huwa na maji yenye virutubisho vingi hivo huwa na biodiverisity kubwa ukilinganisha na maeneo ya bahari ya kawaida. Mkondo bahari wa nungwi unasamaki wengi na waina mbalimbali ambao hawapatikani ktk maeneo mengine duniani: NEED TO FEED THEM FOR SUSTAINABILITY...................................